KAMPALA UGANDA MWANAMUZIKI maarufu nchini uganda, jose chameleon, ameamua kubadili kutoka dhehebu la kikatoliki na kuwa muislam. kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari, tukio hilo lilifanyika juzi jijini hapa na kushuhudiwa na mamia ya waumini wa kiislam. mara baada ya kusilimishwa, mwanamuziki huyo nyota nchini uganda, alishiriki swala ya ijumaa katika msikiti wa kibuli.
Kuanzia sasa ataitwa Gadafi Chameleon. katika tukio hilo la kubadili dini, chameleon alisindikizwa na marafiki zake ambao nao ni wanamuzhki Haruna mubiru na Grace sekamate. chameleon aliyekuwa mkatoliki na kufunga ndoa na Atim Daniella katika kanisa katoliki la mbuya miaka kadhaa iliyopita, amewashtua wengi kwa uamuzi wake. gazeti la mzalendo, Habari za michezo