It is very easy to know who is close to God and the likelihood of someone to become a tool to be used by God in His endeavours. Wanajituma sana lakini wanayo hofu juu ya Mungu hata kama wanatenda mabaya. Wanamuziki wengi wanaookoka ukifuatilia nyimbo zao kabla hawajaokoka utajifunza kitu hicho. Marijani Rajab, Enock Chidumule, Remi Ongala, Mzee Makassy, na sasa Chamelion na wengine wengi. Nyimbo zao za enzi za kale zinaelekeza watu kujifunza utu wema na uaminifu, sio matusi matusi ya kukurupukia. Wanakwepa sana kuhimiza tabia mbaya au ukatili. Nyimbo zao hata leo ukisikiliza bado ni bomba kimaadili. Hata Paulo japo alikuwa anawatesa wakristo wa enzi zile, alikuwa anafanya kwa nia ya kutimiza anachotumwa na wakubwa wake lakini ndani yake alikuwa na hofu juu ya Mungu kwa sana. Badala yake, angalia Murvin Gay (??) aliyekuwa mtoto wa mchungaji na akaamua kuimba sexual healing wimbo maarufu hadi leo. Asiuwawe nini? Tena na babake?
Sifa kwa Bwana kwa kusafisha njia ya Mr and Mrs Chamellion.