Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Kampuni kubwa ya kifahari ya Chanel ya Ufaransa imeacha kuuza bidhaa zake kwa watu wanaonunua na kuzipeleka Urusi, baada ya kufunga maduka yake nchini humo.
Moscow na baadhi ya wateja wameishutumu kampuni hiyo kwa kupinga Urusi, na kutishia kususia chapa hiyo.
Chanel inasema inazingatia tu vikwazo vya Umoja wa Ulaya (EU), ambavyo vinapiga marufuku kuiuzia Urusi bidhaa za anasa za bei ya zaidi ya €300 ($327; £250).
Makampuni mengi ya Magharibi yalisimamisha shughuli nchini Urusi baada ya vita vya Ukraine kuanza.
Chanel aliambia BBC kwamba vikwazo vilivyowekwa na EU, pamoja na Uswizi, pia vinapiga marufuku uuzaji wa vitu vya anasa kwa watu binafsi wanaonuia kuvitumia nchini Urusi.
Kampuni hiyo ilisema "inatii sheria zote zinazotumika kwa shughuli zetu na wafanyikazi ulimwenguni kote, pamoja na sheria za vikwazo vya biashara".
"Hii ndiyo sababu tumeanzisha mchakato wa kuwataka wateja ambao hatujui makazi yao kuu kuthibitisha kuwa bidhaa wanazonunua hazitatumika nchini Urusi," Chanel ilisema katika taarifa yake.
"Kwa sasa tunashughulikia kuboresha mbinu hii na tunaomba radhi kwa usumbufu utakao jitokeza," kampuni hiyo iliongeza.