Changamoto gani umeziona katika biashara ya kuchangiana? Partner business

Wang Shu

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2014
Posts
2,562
Reaction score
3,715
Mtaji,maarifa na uzoefu ni vitu vitakufanya uiyone biashara ni rahisi kufanya.

Kuna wakati unajalibu kusimama peke yako katika biashara unajikuta unayumba katika vitu kadhaa.

Unatamani ungekuwa na mtu (partner) wa kushirikiana nae kwa kila kitu.

Kushirikiana kiuwendeshaji, kuweka pamoja mtaji ukawa mkubwa na kimawazo..

Swala linakuja je utaendana na partner wako kibiashara bila biashara husika kufa??

Haya ni machache kidogo nimeyaona kwa biashara ambazo zina share za zaidi ya mtu 1

⏩Matumizi,
Kila mtu ana matumizi yake, musipowekeana mipaka ya kiasi gani cha kujikimu kwa siku, wiki au mwezi kila mtu atajichukulia atakavyo bila kuzingatia faida na hasara.

⏩Uaminifu,
Ni kitu kigumu kwa partners kuwa na imani sawa na biashara ikishakua kubwa mmoja kati yao fikra zinatakuja anawezaje kujinufaisha binafsi atawaza kuchota pesa akaanzishe biashara mpya.

⏩Kujimilikisha,
Kuchangiana ni kuzuri sana maana mnaweka nguvu pamoja na kufanya kazi kwa pamoja, lakini yule ambae amezidi mchango atajiona yeye ndio mmiliki halali wa biashara ataindesha atakavyo huna la kumwambia amekuzidi share tatizo linaanzia hapo.

⏩Mengine wachangiaji watatupa uzoefu wao biashara za partners wameona nini?

Nawasilisha
 
Mengi ni kama uliyoandika, kupata mshiriki wote mkawa na fikra, matamanio na mipango sawa ya biashara yenu ni nadra sana na ikatokea ukampata hapo njia itakua nyepesi sana hata changamoto mtazitatua kiurahisi..

Kuna wale wa kukata tamaa, yaani yeye changamoto kidogo tuu anakata tamaa,
Na ndio maana inatakiwa unaye fanya naye share awe kweli ameridhia sio kumbembeleza/lazimisha,

Yaani itokee wote mnatafutana mkakutana au umemuwahi na yeye alikua na uhitaji huo,

Japo kuna wale ambao hawakua wanatafuta wala uhitaji lakini ukakutana naye ukamshirikisha, akashawishika akatumia fursa, bila kuanza kukuhoji juu ya uhakika wa wazo lako maana anajua biashara ni kujaribu na changamoto,
Ila sio hawa anakuambia

"una uhakika na wazo/biashara yako?, ngoja tujaribu"

huyu ni wa kumkimbia, Anakutengenezea tension kubwa ya kumuwaza yeye na sio biashara,

Ndio wale siku kimebuma
haishi lawama
"wewe ndio umesababisha yote haya"

Pia kushirikiana mawazo na nguvu kazi, sio sababu mimi nimekushirikisha basi mawazao yote na jitigada za ziada nje ya pesa nitoe mimi,

Mnakaa wote, mnapanga, mnakosoana, mnapatana mnafanya jambo kwa muafaka na mnakubaliana na matokeo, huyu anayekuachia wewe anaweza atumie hio kama kinga ya kukulaumu pindi mambo yakienda sivyo.
 
Uzoefu unaonyesha partners ambao hushiriki kwa kutoa mtaji na si wazoefu wa biashara si wastahamilivu pale biashara inapokumbwa na changamoto.

Lawama za kupotoshwa na kuibiwa hutawala.
 
1.Wengi sio waaminifu unakuta anakuzunguka labda kitu cha buku atakuambia buku mbili kiufupi unakuwa umenunua wewe

2.kutokubaliana kimawazo
Labda wewe ungependa mfanye hivi au msimamie biashara hivi yy anaona hapana
Mfano mnalima wote yy anaweza shauri tuweke mtu tu asimamie lkn ww utataka nyie wenyewe mkasimamie msipoelewana kwa kufata njia sahihi mnapoteza

3.wengine wanakuwa janjajanja nyingi ndio maana wanasema mtu unayetaka muwe washirika umjue vizuri tabia yake na ni vizuri muongelee mambo mapema kabla hamjaanza na msisahau kuandikishiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"2.kutokubaliana kimawazo"

Nimeikubali hii
 
Uzoefu unaonyesha partners ambao hushiriki kwa kutoa mtaji na si wazoefu wa biashara si wastahamilivu pale biashara inapokumbwa na changamoto.

Lawama za kupotoshwa na kuibiwa hutawala.
Ni kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…