Restitius Respicius
New Member
- Jul 6, 2020
- 1
- 9
Kila changamoto inapokuja kwenye maisha huwa inakuja kwa sababu maalumu na siyo kwa bahati mbaya, kwa hiyo hutakiwi kuikimbia changamoto inayokukabili na badala yake unapaswa kuikabili changamoto yako kwa akili, hekima na utashi wa hali ya juu sana kwa sababu;
1. Kila changamoto inakuja kutufundisha jambo jipya maishani mwetu na siyo kutuletea maumivu
2. Kila changamoto inapokuja huwa inakuja kutuonesha ni wapi tulikoteleza ili kutusaidia kutoanguka tena katika sehemu hiyo
Kwa hiyo kila changamoto inayokuja, ione kama darasa la wewe kujifunza jambo jipya maishani, maana hakuna sehemu nzuri ya kujifunza kama kupitia changamoto zetu na hata za wale wengine wanaotuzunguka maana changamoto zintuonesha makosa yaliyopo ili tuyapatie ufumbuzi tupige hatua mbele katika kulifikia kusudi la kuumbwa kwetu hapa duniani.
Katika kuhitimisha napenda nikukumbushe tu kwamba kuna siku niliwahi kusema "siyo kila baya ni baya, kuna mabaya yenye uzuri ndani yake" , kwa hiyo siyo kila changamoto ni maumivu au mateso, hapana ni darasa tu Mungu ametupa ili tujifunze kwa hiyo kuwa mwepesi wa kushukuru na mwerevu kujifunza kutokana na hiyo changamoto yako.
Restitius Respicius 2020