ntemi masali
Senior Member
- May 20, 2013
- 136
- 26
Katiba ni roho ya taifa lolote duniani,Watanzania tuko kwenye mchakato wa katiba mpya na hatua ya mabaraza ya wilaya na mabaraza yenye malengo na mitazamo inayofanana kujadili rasimu na kutoa mapendekezo na maoni yao kuhusu rasimu hiyo ya kwanza ya katiba mpya ,katika hali ya kushangaza ccm wamekuwa wakibeza namna chadema walivyokuwa wakijadili rasimu hiyo pamoja na wanachama wao kwa kutumia mikutano ya nje ya ukumbi ninachokijua mimi ni kwamba tofauti ni mahali tu kuwa wengine wameweza kukaa ukumbini ndani kwa kuwa ni wachache na wengine wamekosa ukumbi kwa uwingi wao ndio tofauti ya ccm na chadema je? wanajamvi mnasemaje,