flulanga
JF-Expert Member
- Jul 1, 2016
- 4,860
- 6,390
Yatima kwa tafsiri ni mtoto aliyefiwa na wazazi wote wawili yaani baba na mama muda huo huo umri wake ukawa chini ya miaka 18.
Habari ndugu zangu, uzi wangu utaelezea hadha wapitiazo watoto yatima kimalezi na makuzi au watoto waliotelekezwa na wazazi wao (sio wote wanapitia ila naamini ni wengi).
Kama wewe ni kati ya watu waliopewa/kuachiwa jukumu la kulea mtoto/watoto wa ndugu yako basi unaweza kujifunza kitu hapa.
Twende pamoja sasa;
Mimi nikijana kwa majina naitwa Henerico. Ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto watatu. Mama yangu alijaaliwa kuzaa mara mbili yaaani mimi ndio wakwanza na wadogo zangu wawili wanaonifuata ni mapacha yaaani Kulwa na Doto wote hawa ni wanaume.
Kwa upande wangu mimi kama mtoto wa kwanza kwa mama yangu baba yangu aliikataa mimba yangu kwa mujibu wa maelezo ambayo nayasikia toka nikiwa mtoto. Wadogo zangu pia wenyewe wana baba yao ila hawajaishi nae alipozaa tu na mama yangu baba yao aliondoka na hakujulikana kaenda wapi kwa hiyo wote tukabaki na malezi ya upande wa mama.
Kwa bahati mbaya me nikiwa na umri wa miaka 6 na wadogo zangu wakiwa na miaka 3 mama yangu alifariki dunia. Kwa wakati huo sikuona kama kuna shida au sikuhisi kama uyatima umeingia bali niliona ni kitu cha kawaida nadhani ni kutokana na umri wangu ulikuwa bado mdogo ila kumbukumbu kichwani kwangu bado ninazo mpaka msiba ulivyoendeshwa. Msiba ulipita na maisha mengine yakaendelea tukiwa tunaishi na bibi yetu na mama zetu wadogo na wakubwa.
Mwaka mmoja baada ya msiba niliweza kupelekwa shule darasa la kwanza, bibi yangu na mama zangu wakubwa ndio walikuwa wahusika wakubwa.
Mpaka naanza shule nilikuwa bado sijaona pengo la mama. Nilipofika darasa la tatu ndio nilitambua pengo la mama lipo wapi.
Nilikuwa nafanya mafundisho ili nibatizwe na mafundisho niliyafanya kwa muda wa miaka mitatu toka nikiwa darasa la kwanza mpaka nilipofika darasa la tatu ndio nilikuwa nahitajika nibatizwe. Kwa bahati mbaya nilikuwa sijalipa hela ya zaka mpaka ile siku ambayo usiku wake ndio nilikuwa nahitajika nibatizwe mpaka kufikia saa 10 jioni bado sijapata hela ya zaka, mda huo katekista ananiambia 'ujalipa hela ya zaka uwezi kubatizwa', nikifikiria mafundisho nimefanya kwa muda wa miaka mitatu halafu leo hii nisibatizwe aiseee NILILIA.... Bibi yangu angekuwa na hela angenipatia ila wakati huo na yeye alikuwa hana pesa. Nikienda kwa mama zangu wakubwa wanatupiana mpira ukienda kwa huyu anakwambia nenda kwa yuleeee... NILIMWAGA CHOZI na ndiyo siku hiyo nilipoanza maombolezo ya mama yangu.
Ilipofika jioni mama yangu mkubwa alipojihakikishia nimekosa kwa ndugu wote ndipo aliponipatia pesa (7,500) nikaenda chapu kulipia nikarudi nyumbani kujiandaa kwenda ibadani kubatizwa. Ila hapo macho yamenivimba kwa kulia na kiukweli nisingebatizwa ile siku nilikuwa najiandalia safari niende ovyo nikawe mtoto wa mtaani.
Usiku wa ubatizo ulipofika nilikutana na msimamizi wangu wa ubatizo nikiwa nimevaaa yale majaketi makubwa ili kuficha shati langu la ndani, lilikuwa limechanika, yeye hakutambua lile koti kubwa vile nimelivaa la nini, Akaniamuru nilivue, nilipolivua ndipo alipogundua kuwa nimelivaa koti kwasababu gani Ikabidi awe mpole akaniambia basi nilivae tu!! Ibada ya ubatizo ilienda vizuri. Tukarudi nyumbani kuendelea na maisha.
Ile usiku wa ubatizo hadi leo naikumbuka jinsi wenzangu walivyokuwa wamependeza, wanapiga picha na kuvishwa mataji na ndugu zao. Huwa nacheka sana na kuuona Ukuu wa Mungu maana kwa wakati huo wala sikuwa na akili ya kuwaza au akili ya kutamani wenzangu walivyopendeza, akili yangu yote iliwaza nibatizwe.
Baada ya ile siku ya ubatizo ndipo nilipoanza kutambua thamani ya mama. Toka siku hiyo nilianza kuwa namlilia mama yangu, sikuwa naamani tena moyoni mwangu, maisha ya upweke ndipo yalipoanzia hapo. Nilianza kujiona ni mtoto mwenye mapungufu makubwa sana tofauti na watoto wenzangu.
Nilimaliza darasa la saba kiugumu sana maana shule nilianza kuichukia sana.
Kabla sijamaliza shule alikuja mtoto wa mama yangu mkubwa tukaungana nae darasa moja alitokea kijijini, tukawa tunaishi kwa bibi na watoto wengine wa mama zangu wakubwa pamoja na wadogo zangu. Ila kiukweli maisha hayakuwa mazuri sana wala mabaya sana. Tukafaulu shule moja mimi na huyo ndugu yangu yaaani kidato cha kwanza.
Ulipofika muda wakufanya maandalizi ya kwenda shule ndipo ilikuwa kimbembe sasa. Mama yangu mkubwa anashindwa kumpeleka mtoto wake shule kwasababu yangu mie, jamii itamuonaje ampeleke mtoto wake shule halafu mimi nibaki kitaaa!! Mama yangu mkubwa alipitia kipindi kigumu sanaa nilitamani nimwambie ampeleke tu kwanza mwenzangu ambae ni mtoto wake mimi nisiwe sababu ya mwenzangu kutokwenda shule ila nikabaki na mgogoro na nafsi yangu nikawa najiona na hatia yaani sikupenda niwe chanzo cha mwenzangu asiende shule. Ila nashukuru Mungu mwisho wa siku walijipiga piga na wote tukaenda shule. Wabarikiwe kwa hilo. Japo nilisoma huku najiona kabisa ni mzigo kwa ndugu zangu.
Maisha yalisonga na masomo yalisonga ila changamoto zilikuwa zipo nyingi sanaaa. Mtoto wa mama yangu mkubwa alikuwa hapendi shule, alikuwa anaenda shule kutimiza wajibu tu. Kwahiyo nilipokuwa nahitaji kusoma twisheni ilibidi niwe namtumia huyu mwenzangu kwa kumbembeleza amwambie mama yake ambaye ni mama mkubwa kuwa tunataka tusome twisheni atulipie ikawa ndio maisha yangu ya uchawa kwa ndugu yangu ili maisha yaende. Ila mwisho wa siku alinigomea kuwa chawa wake. Ikabidi twisheni iishie hapo ila bado nikawa nikiwa na shida ya mahitaji ya shule nilikuwa nasubiria mpaka mwenzangu nae apate shida kama yangu yaaani nikawa naishi kwa kusafiria nyota. Nilikuwa sipendi kuonekana mimi ndio na mahitaji mengi kuliko mtoto wake.
Wadogo zangu muda huo nasoma na wenyewe pia walikuwa wanasoma ila kwa bahati mbaya wadogo zangu walikuwa watukutu sana toka wakiwa wadogo, walikuwa hawapendwi kutokana na tabia zao. Kuna siku nilimsikia mama yangu mkubwa anawaambia 'kamtafuteni baba yenu' niliumia sana..., niliingia ndani nililia sana nikafikiria baba yao hata hawamjui inakuwaje wanatamkiwa kauli kama ile? Nilikosa majibu zaidi niliishia kulia tu!! Ila hakuna aliyejua kama nililia.
Nilimaliza shule vizuri. Na kwa bahati mbaya matokeo yalipotoka hayakuwa mazuri. Na moja kwa moja niliyaanza maisha rasmi maana pale nyumbani nilipachukia kwa hiyo nilihitaji kuwa na maisha yangu.
Katika malezi niliyolelewa kwa kiasi fulani ndio matokeo ya maisha yangu ya sasa Kama vile;
Walezi/wazazi fanyeni hivi ili kupunguza watoto wa mitaani;
- Walezi/wazazi tunapoamua kulea watoto/mtoto ambae sio wako tujitahidi kuweka usawa na hata kama msipoweka usawa basi mjitahidi msioneshe moja kwa moja. Hii hali iliniathiri kwa kiasi fulani nakupelekea kuichukia shule.
- Wazazi/walezi tuchungeni kauli zetu sio vizurii kuwaropokea watoto kauli tata ambazo zitampelekea mtoto maumivu na kutamani kujitenga na nyumbani. Hali hii ilipelekea mdogo wangu kuhasi nyumbani na kuwa mtoto mitaani.
- Wazazi tujitahidi kuwafundisha watoto wetu ili upendo, pindi wachanganikapo na watoto wengine ambao wazazi wao hawapo basi waweze kuishi nao bila ubinafsi. Hii ilinitokea mimi, ilifikia hatua mtoto wa mama yangu mkubwa ananiambia 'usitumie kitu fulani kwani kanunua mama yako?' Hali hii inaweza pelekea mtoto kujizira nakupelekea hata kujizuru au kwenda mitaani.
- Walezi tujitahidi kuwa na moyo wa kutoa mahitaji kwa watoto yatima, kutimiza ndoto zao. Tukifanya hivyo mtoto atajihisi na thamani wala hawezi kuwaza yeye ni yatima, hawezi kutamani maisha ya kwenda kuishi mitaani. Mfano mimi nilipokosa hela ya kutoa zaka kanisani nibatizwe, nilijisemea katika moyo wangu 'nisipobatizwa basi bora niende ovyoo'.
HITIMISHO; Wazazi tuombe sana MUNGU atujaalie uhai mrefu na tujiepushe na visababishi ambavyo vitapelekea kufupisha uhai wetu au kupunguza umri wetu wa kuishi duniani ili tulee watoto wetu.
Uyatima sio mzuri, mwanao unavyomlea usifikirie na mwingine atamlea hivyo, atamvumilia kama vile wewe unavyomvumilia hapana sio rahisi hasa kwenye hizi familia zetu za kipato cha chini.
Tuishi kwa maangalizo pindi pale tunapopata nafasi basi tujitahidi kuwekeza kwa watoto wetu upendo, elimu, na rasilimali ambazo zinaweza kuja kuwafaa badae endapo kama kifo kitabisha hodi.
MWISHO.
WENU MTIIFU HENERICO.

- kutojiamini,
- hasira na chuki,
- kutokufanya vizurii katika masomo,
- kuathirika kisaikolojia,
- Kuathiri mwenendo mzima wa maisha ya baadae hasa kifamilia.

Upvote
7