Elimu ni ufahamu na ufunuo juu ya mambo husika, yaani kuna elimu ya ; darasani, dini, barabarani, n.k
Katika mtazamo wa elimu ya darasani yaani chekechea, msingi, sekondari na chuo. Nitaangazia baadhi ya changamoto zilizopo na baadhi ya namna ya kuzitatua.
Elimu ya Tanzania mbali na kuzalisha wasomi wengi Sanaa na wataalamu mbalimbali katika nyanja tofautitofauti bado inakabiliwa na vikwazo vingi katika utekelezaji wake yaani utoaji wa elimu Kwa wanafunzi.
Changamoto katika elimu
1) Ukatili wa kijinsia.
Wanafunzi wote wakike na wakiume wanakabiliwa na Ukatili huu haswa kingono. Hii hutendeka aidha baina ya wanafunzi wawili, mwalimu Kwa mwanafunzi au mtu yeyote Kwa mwanafunzi. Hii husabisha mimba Kwa watoto wa kike na athari za kisaikolojia Kwa jinsia zote ke na me.
2) Mazingira yasio rafiki Kwa wanafunzi wa kike.
Wanafunzi wa kike waliofikisha umri wa balehe hulazimika kukwepa siku za masomo pindi wawamo ktk siku zao.
3) Njaa mashuleni
Hii huwakumba haswa wanafunzi katika shule za serikali kwani wengi wao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapatia fedha kumudu Milo anayohitaj mwanafunzi awapo shuleni.
4) Wanafunzi kukaririshwa.
Katika shule nyingi nchini ikiwemo niliyosoma Mimi sekondari. Wanafunzi hulazimika kukariri hoja zinazotelewa na mwalimu wa Somo husika na Si vinginevyo hii hupunguza ubunifu na uwezo wa kufikiri wa wanafunzi na kuishia kukariri na sio kufikiria.
5)Muda wa masomo uliopitiliza
Suala hili lipo katika shule nyingi hapa nchini haswa za bweni. Ambapo waalimu huongeza muda wa vipindi na ratiba za masomo kiwabana wanafunzi. Kama vile vipindi kuanza Saa 11-12 alfajiri hadi saa11-12 jioni.
6)Uhaba wa miundombinu.
Hii inaendelea kuwa changamoto kubwaa katika shule nyingi hapa nchini licha ya jitihada kubwa inayofanywa na serikali na baadhi ya taasisi kutokomeza tatizo hili
Naam chagamoto tajwa ni ngumu kuziondoa zikapotea Kwa kipindi Cha muda mfupi na haziwezi kuisha kwakuitegemea serikali pekee, ila tu ushirikiano wa jamii nzima na Taifa kiujumla.
Baadhi ya athari ya changamoto hizi ni;
1) Kusitisha kuendelea na masomo
2) Kushuka kwa ufaulu
3) Utoro mashuleni
4) Mimba Kwa watoto wakike na athari za kisaikolijia Kwa wakiume.
NINI KIFANYIKE ?
1) Taifa kwa ujumla tuungane kupinga na kukemea matendo ya Ukatili wa jinsia. Kwa kuendelea kutoa semina na mafundisho mbalimbali yakihusisha sababu zake, athari zake na njia za kuyaepuka na kujikinga dhidi ya matendo hayo, kwa jamii nzima hususani wahangwa ambao ni wanafunzi wote ke na me.
2) Kuendelea Kuunda ushirikiano zaidi kati ya jamii na wanafunzi ili kutengeneza mazingira rafiki kwa wanafunzi wanaopitia changamoto mbalimbali ikiwemo ya ukatili na ambao wapo mbioni kukumbwa na changamoto hio kufunga na kurahisha kupatiwa msaada na udhibiti wa matendo zaidi ya Ukatili wa kijinsia.
3) Mpaka Sasa suala la kuboresha mazingira rafiki Kwa watoto wakike limepokelewa kwa uzito wake katika jamii na tunaona taasisi kama Flaviana matata foundation n.k zipo mstari wa mbele kupigania hili Kwa kutoa michango ya taulo za kike na kuwezesha upatikanaji wa maji safi na salama katika vyo Ili kuwapa unafuu watoto wakike wawapo katika siku zao. Lakini muamko katika jamii bado ni mdogo na pia tasisi hizi haziwezi kuhudumia shule zote nchini hivyo ni wajibu wetu kama jamii kusimama nao pamoja kuwezesha taasisi hizi kuwafiki wanafunzi wengi iwezekanavyo. Kusudi mtoto wa kike naye apate elimu bila bugudha.
4) Tatizo la njaa Kwa wanafunzi sio suala linalo zungumzwa Kila siku lakini Kwa baadhi waliokumbwa na Tatizo hili hususani shule za Serikali za na wameona athari yake na sio salama Kwa afya ya Mwanafunzi Tatizo hili linaweza kupatiwa ufumbuzi na kupunguza uhitaji wa mabilioni ya fedha kutoka serikalini Kwa kuanzisha miradi kilimo cha mazao ya chakula na ufugaji wa mifugo michache katika maeneo ya shule. Ambayo itaweza kusimamiwa na kuendelezwa na waalimu na Wanafunzi wenyew bila utegemezi. Hii ni kama kupiga ndege wawili Kwa jiwe Moja Kwa maana mbali na kuwapatia wanafunzi chakula vile vile wanafunzi hujifunza kuhusu kilimo hi yaweza kuwasaidi kukabiliana na changamoto ya ajira Kwa kua Kuna maisha baada ya shule
5) Kusoma sio vita" ni maneno ya mwalimu mmoja hivyo badala ya kuwakalisha wanafunzi madarasani Kwa kipindi Cha muda mrefu iwepo Ratiba mbadala kuruhusu muda wa michezo clubs mbali mbali kuongeza ubunifu na Ufanisi katika nyanja mbalimbali kama ambavyo shule chache hapa nchini hufanyaa na kiwango cha ufaulu kimekua kuzidi miaka ya awali.
6) Waalimu nchini kote wawe na utamaduni wa kuwaruhusu wanafunzi kufirikia na kubuni njia na mbinu mmbadala za kupata majibu katika masomo hii itawajenga kutatua matatizo katika maisha ya kawaida. Kwa upande mwingine pongezi Kwa baraza la mitihani necta Kwa kuwa siku hizi Kwa kuwa mitihani mingi maswali yanaulizwa Kwa njia isiyo ya Moja Kwa moja hii inawalazimu waalimu wengi kuwatengenezea mazingira ya kufikiria wanafunzi wao wawapo madarasani.
7) Mafunzo ya kisasa. Mazingira ya elimu nchini yanatakiwa kwenda na mabadiliko ya teknolojia, hivyo badala ya kuendelea kuhangaika kuwamezesha wanafunzi riwaya na tamthilia zilizochapishwa itakuwa bora zaidi endapo riwaya na tamthilia hizi zitafundishwa kidigitali zaidi kupitia video. Kwani kizazi hiki Cha digitali teknolojia inaushawishi mkubwa Kwa watoto na akili zao hunasa Kwa haraka picha kuliko maandishi.

Upvote
3