Changamoto wanazomutana nazo Kampuni Changa

Joined
Feb 12, 2020
Posts
72
Reaction score
87
Wakuu naleta swali kwenu,
Naomba kuuliza hivi
1).ni sababu gani hasa zinaifanya kampuni Changa kufa Hali yakuwa mmiliki ndie CEO
2). Hivi inatokeaje yaani owner wa kampuni also, ni CEO lakini anakuwa fired out Katika board of Directors
- ni sababu zipi zinaweza kupelekea CEO also owner akawa fired out Katika bodi???
 
No. 2 hapo inatokea pale ambako CEO Ni ana hisa nyingi kulinganisha na directors wenzake lkn haohao directors(minority shareholders) ikitokea waka-join nguvu pamoja na kua na share nyingi kumzidi (51% and above) kumzidi huyo CEO then wanaweza kumpindua vzr tu pamoja na Kwamba yeye ndie founder.
 
What if, yeye ndie Shareholder mkubwa??
Means kama watamfire out katika board anauwezo wa kutumia external force ya kuwa yeye ndie Shareholder Mkuu Na akarefuse maamuzi ya bodi
 
What if, yeye ndie Shareholder mkubwa??
Means kama watamfire out katika board anauwezo wa kutumia external force ya kuwa yeye ndie Shareholder Mkuu Na akarefuse maamuzi ya bodi
Kama yeye ndie Major shareholder mwenye >51% hawawezi kumfukuza.Lkn Kama Ni major shareholder na ana less than 51% wanaweza kumfukuza tu pamoja na Kwamba Ni major shareholder.
 
Nguvu ya umoja si kigezo cha kuwa na shares nyingi. Shares ni umiliki mwenye 51 ndiye mmiliki kubadili hilo ni kuchukua shares toka kwa zile 51 haijalishi njia gani itatumika.
 
Clients wengi wanapenda huduma kulingana na matakwa Yao ....Kuna vitu vingi kma kampuni changa inakuwa bado haijavipitia .... Ndo maana tenda nyingi wanapewa experienced companies
 
Kwa kampuni changa, 'family business' ni bora mke/mume na watoto ndio wawe wana 'share'
 
1. Kufa kwa kampuni hakuogopi iwapo majority shareholder ndiye CEO. Kufa kwa kampuni huwa na sababu nyingine kama vile kukoma kwa biashara, kuamua kufunga shughuli za kampuni, hasara ama kukosa shuguuli za kufanya, nk.

2. Katika kila kampuni niblazma kuwe na shareholders kuanzia wawili na kimsingi ni lazma kuwe na board of directors ambao hupaswa kuwa kuanzia wawili na hawa wanatakiwa kuwa ni shareholders pia.
Kisheria, huwa hatusemi 'mtu anamiliki kampuni' bali huwa tunasema kuwa fulani ana hisa nyingi za umiliki wa kampuni kwani hata wewe leo ukiwa major shareholder ni muda wowote katika kampuni yako ukageuka kuwa minor shareholder.

Sasa kuna wakati huyu uliyemuita CEO. Huyu mtu anakua kwa lugha nyepesi ni MWAJIRIWA katika kampuni hiyo hapo sahau kuhusu yeye kuwa mwanahisa na director wa kampuni hiyo, hivyo hicho cheo cha kuwa CEO ni kwamba amepewa nafasi na bodi ya wakurugenzi kuwa mtumishi wa kampuni kwa nafasi ya CEO sawasawa na ambavyo bodi hiyo inaweza kuajiri mfagizi wa vyoo vya ofisi hivyo nayo JOB DESCRIPTION anayotakiwa kuicuata na akishindwa basi kampuni inaweza kusitisha ajira yake ya uCEO.

Tukija kwenye kipengere kuwa inawezekana vipi major shareholder director kutolewa kwenye nafasi husika?
Ipo hivii, katika katiba yenu ya kampuni lazma muweke utaratibu wa namna ya kumpata director wa kampuni na utaratibu upi utazinhatiwa katika kupata na kumuondoa ama yeye kutoka kwenye nafasi hiyo hata kama atakua akimiliki hisa 99.99% za kampuni hiyo.

Lakini kuna masuala mengine ambayo yanaweza kuwa sababu yenye mashiko ya kumchomoa mtu toka nafasi ya mkurugenzi wa kampuni iwe ni major shareholder ama minor shareholder nazo kwa kiasi kikubwa zimejikita katika kipengele cha kimaadili kama ifuatavyo;
i. Kutoa nje sifi za kampuni/ofisi
ii. Ufisadi ama uhujumu wa mali ama rasilimali za kampuni.
iii. Kukiuka katiba ya kampuni.
iv. Muda wake wa kuwa mkurugenzi kuisha kama ilivyotajwa katika kampuni
v. Kuixanganya board ama kufanya maamuzi ya uongo au ya kiwaki juu ya kampuni, nk nk
 
What if, yeye ndie Shareholder mkubwa??
Means kama watamfire out katika board anauwezo wa kutumia external force ya kuwa yeye ndie Shareholder Mkuu Na akarefuse maamuzi ya bodi
Kama ameondolewa kwa sababu zenye mashiko basi HAWEZI KUJIRUDISHA HATA KAMA ANAMILIKI 99%ya hisa za kampuni husika
 
Kama yeye ndie Major shareholder mwenye >51% hawawezi kumfukuza.Lkn Kama Ni major shareholder na ana less than 51% wanaweza kumfukuza tu pamoja na Kwamba Ni major shareholder.
Mkuu nadhani hapa umejielekeza tofauti kidogo. Kama director ametolewa kwa sababu zenye mashiko basi hawezi kupindua maamuzi hayo eti tu kwa sababu ana hisa nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…