Baba Ndubwi
JF-Expert Member
- Sep 27, 2013
- 1,275
- 2,060
Ndugu namvumi king kwenye hili andiko lako kama ni lako kweli basi umepotosha mambo mengi sana..aidha kwa kujua ama kutojuaUzi mfupi**
Wachawi wanapatia changamoto nying wanapotaka kukuroga, kwanza inabidi atafute pesa ya kununulia Vifaa Vya kazi
Kununua Vifaa Vya kazi ni gharama kubwa na Muda mwingine itamlazimu kusafiri ata nje ya Mkoa ili akanunua kifaa icho cha kukurogea
Kwa mfano Kuna uchawi mwingine ili ufanyike mchawi ataitaji maji ya maiti
upatikanaji wa maji ya maiti ni mgumu sana,
Yani inabidi uwe na koneksheni ya kufa mtu ili upate maji ya maiti na maana muda mwingine unaweza uziwa maji feki
Kwaiyo katika hali kama iyo mchawi inabidi atoe pesa ndefu ili kufanikiwa
Mchawi ni mtu mbishi sana yana hakubali kushindwa kabisa
Kitu ambacho kinamuumiza sana mchawi ni pale anapotumia nguvu nying kukuroga alafu ww unaleta dharau
Yani yeye anapokuroga anataka kuona matokeo yani anataka kukuona umepaniki
Mchawi Anaskia raha sana pale anapoona kwamba umepaniki alafu umekimbilia kwa mganga
Changamoto kubwa kwa mchawi ni kuona kwamba badala ya kupaniki lakini ww ukamua kufanya ibada yan ukasimama na MUNGU
Mda mwingine mchawi inabidi akijifunze teknolojia ambayo itamsaidia kukuroga
Hapa inabid aende kozi iyo maalumu na inabidi alipie pesa kwa ajili ya kupata utaalamu
Upatikanaji wa Vifaa Vya kurogea imekuwa changamoto kubwa kwa Wachawi
Maana katika maduka ya kawaida ya asili havipatikani
Madalali wanaouza Vifaa Vya kurogea wamekuwa wakiwauzia wachaw Vifaa ivyo kwa bei juu sana
Kwa mfano mchawi ili aingie kwako lazima awe na testa ili aone kama kuna mtego au hamna
Testa ya kichawi inauzwa bei juu sana maana bila ya testa unaweza jikuta unaingia mtegoni
Kama ulishawai ona mchawi Kanasa juu ya bati au ameanguka basi jua uyo ameingia bila testa
Wachawi wanatumia pesa nyingi sana kununua Vifaa Vya kurogea pande za mahospitali na makaburini
Mara nyingine mchawi anajikuta anamadeni mengi sababu anataka afanikiwe kukuroga
Akishakuroga itambidi afatilie mara kwa mara maendeleo yako ili aone kama uchawi unafanya kazi
Muda mwingine inabidi afanye update yani kama vile Ana update windows
AsanteniView attachment 1495584
Ndugu namvumi king kwenye hili andiko lako kama ni lako kweli basi umepotosha mambo mengi sana..aidha kwa kujua ama kutojua
Kwanza na declare interest...MIMI NI MCHAWI tena ni mchawi by professional...na katika maisha yangu nimefanya sana ushirikina(uchawi + uganga) sasa hivi sifanyi tena na unaweza kuniita mstaafu nakula pensheni
Mchawi hana changamoto ya pesa hata mara moja kwakuwa kabla ya kufikia kuwa mchawi ni lazima ufaulu kozi ya kuwa mwanga..hii ndio basic ambapo kazi yake kubwa ni kuweza kuingia mahali na kutoka bila wahusika kujua
Ukishafaulu hapo ndio sasa unaingia hatua ya pili nayo ni uwezo wa kuchukua utakacho bila kustukiwa...kwahiyo ishu ya ukata wa fedha hapa haipo
Mchawi hana faida wala matumizi na fedha kwakuwa anapata akitakacho at a click bila kutumia fedha
Wale wa chumaulete ni wanafunzi wa uchawi ndio maana huwa wanafanyia mtaani kwao kwa watu wanaowafahamu
Mchawi kama mchawi hana matumizi na malighafi kama maji ya maiti ...hiki ni kitendea kazi cha mhitaji kwenye shughuli maalum na hiki hakipatikani kwa njia ya uchawi lazima kiwe fresh
Pesa wanazotoza waganga ni kwa ajili ya kiingilio cha madhabahu za giza (nitaweka link ya post) na commitment binafsi kuwa unakubali kufanya hayo utakayo na yatakayofanyika
Wachawi kati ya vitu wanavyoogopa sana ni Jina la Yesu, vitu vya ugwadu na chumvi...[nitaendelea]
Kiingilio cha madhabahu za giza
Unapoenda kwa mganga wa kienyeji unaenda kutengeneza maagano Ukifika pale lazima yatatokea haya 1. Atavaa mavazi rasmi ya kazi (inaitwa kuvaa miongozo) 2. Mtakuwa kwenye chumba chenye madhabahu inayoendana na shughuli zake(kilinge) 3. Utajieleza ama atakueleza matatizo yako! 4. Utatoa pesa...www.jamiiforums.com
Mshirikina halisi haachi...wachawi hawa wepesi ndio huacha na kubaki salamaUmbuje Kwani huwa inawezekana mtu kuwa mchawi au mganga wa kienyeji kisha akaweza kuacha bila kupata madhara yatokanayo na visasi vya kimaagano?
Manake nasikia huwa watatishiwa kuuawa!
Naonaga wale wachache sana ambao hujisalimisha kwa wachungaji kwa kupeleka matunguri yao ya uchawi kuchomwa!
Naomba ufafanuzi tafadhali
Sasa boss wangu wewe umesema ulikua mganga mshikina na mchawi, umeweza vipi kuacha bila ya athari zinazotajikana kukupata.Mshirikina halisi haachi...wachawi hawa wepesi ndio huacha na kubaki salama
Kwa hio hapa na wewe uliwahi kufanya hivyo kwa watu wenye nasaba na wewe. Vipi kwa Sasa unajisikiaje ndani ya dhamiri Kama uliwahi kufanya.Muda mwingine inabidi afanye update yani kama vile Ana update windows[emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Updates za kichawi ni kafara la damu na halifanyiki kiholela ...ni kila mwaka mara moja au mbili
Usipotoa kafara unnajiweka kwenye risk ya kupungukiwa na nguvu na uwezo wa kutenda kichawi ama kujikinga na kujilinda
Ni ngumu kufunguka hapa upenuni..nitauza siriSasa boss wangu wewe umesema ulikua mganga mshikina na mchawi, umeweza vipi kuacha bila ya athari zinazotajikana kukupata.
I did my own special way ..ndio maana leo niko huru kabisaKwa hio hapa na wewe uliwahi kufanya hivyo kwa watu wenye nasaba na wewe. Vipi kwa Sasa unajisikiaje ndani ya dhamiri Kama uliwahi kufanya.
I did my own special way ..ndio maana leo niko huru kabisa