jicho la mwandishi
New Member
- Jul 25, 2022
- 2
- 1
Kwenye kutazama tazama huku na kule jicho la mwandishi limetua kweneye suala hili linaloikumba sana jamii yetu ya Tanzania. Na suala leyewe lililogusa jicho la mwandishi si jingine ni suala la elimu na ajira katika nchi yetu pendwa ya Tanzania..
Picha kutoka mtandaoni
Elimu katika nchi yetu imekuwa na changamoto nyingi sana toka nchi yetu imepata uhuru na mwanzoni changamoto ilikuwa kwenye jinsi yakuipata lakini changamoto sasa imepanuka kwani kadiri miaka inavyosonga mbele Elimu yetu imeshindwa kusonga mbele hivyo basi kufanya wanufaika kati ya wanaohangaika kuipata kuwa wachache.
Katika hatua iliyofikia inabidi sisi kama jamii tukiongozwa na viongozi wetu inabidi tupige hatua moja kando na kulitazama hili suala kwa jicho la tatu ili kujua wapi tunakwama, changamoto ni zipi na ni kwa jinsi gani tunavyoweza kusonga mbele ili kuhakikisha elimu yetu nayo inasonga mbele na kuzidi kuwanufaisha watanzania.
Baba wa taifa mwl. Julius Kambarage Nyerere aliona tatizo kwenye nyanja ya elimu tuliorithi kutoka kwa wakoloni kwenye kuchochea suala la maendeleo katika nchi yetu baada ya uhuru na ndio maana akaleta mageuzi kwenye mfumo wa elimu na kuzindua shule za ufundi, kwanini hata sasa tusifanye mageuzi.
Elimu yetu inachangia kuleta changamoto kwenye suala la ajira hasa kwa kuzingatia elimu rasmi inayotolewa kwenye shule zetu na vyuo vyetu ni elimu inayowaandaa wanafunzi wengi kuajiriwa hivyo basi wanafunzi wengi wanapohitimu gadhabu kwenye suala la kujiajiri kwani sio kitu walichopandikizwa masomoni.
Imekuwa kawaida kwa kila mwaka kwa taasisi zetu za elimu kutoa idadi kubwa ya wahitimu huku kukiwa na idadi ndogo ya nafasi za ajira soikoni. Hali hii imefikia mahala ambapo nchi yetu ina idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanakimbiza vyeti ambavyo ni makaratasi tu badala ya kukimbiza maarifa yliyotakiwa yatokane na hio elimu kwani aslimia kubwa ya wahitimu hukosa ajira kabisa au huapta ajira lakini sio katika fani walizozisomea.
Picha kutoka mtandaoni.
Kukosekana kwa ajira kwa wahitimu kumeleta wingu la kauli kutoka kwa watu mbalimbali kwamba wahitimu hao wajiajiri . Na watu ambao hutoa kauli hizo wenvgi wao ni waajiriwa hasa katika ofisi za serikali. Kama kujiajiri ingekuwa rahisi hivyo kama wengi wao wasemavyo kwanini wasiache ofisi walizozishikilia kwenda kwa damu changa za vijana mbalimbali zinazotemwa na taasisi za elimu nchini.
Kujiajiri aidha katika fani wahitimu walizosomea au biashara mbalimbali pia kuna changamoto zake ambapo changamoto kuu ni mtaji ambao ni mtihani kutokana na hali za kiuchumi za familia za wahitimu wengi. Bodi ya mikopo kwa elimu ya juuinatoa mikopo kwa wanafunzi vyuoni wasioweza kumudu gharama za maisha na masomo kipindi wapo masomoni.
Je, kama kwenye masomo tu inabidi hao vijana wawezeshwe hao vijana watawezaje kufungua ofisi zao wenyewe ili waweze kujiajiri katika fani walizosomea au muda wote na juhudi walizotumia wakiwa masomoni ilikuwa ni bure na wanatakiwa watelekeze vyote walivyovipata wakiwa kwenye taaluma zao na kwenda kufanya shughuli zingine na je, hizo shughuli watakazoenda kufanya zitawawezesha kulipa hilo deni ambalo chanzo chake ni hiyo elimu.
Hili sio suala la kufumbiwa macho kwani tumeona waajiriwa wengi maofisini wakihangaika kwa muda mrefu kulipa deni hilo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu. Endapo kwa fikra hiyo mhitimu akaamua kuachana na ndoto na malengo yake na kuzama katika biashara ndogo ndogo suala ambalo hakulipangia mikakati, je, biashara hizo ndogo ndogo zitaweza kumsaidia mhitimu huyo kulipa hilo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu, deni hilo ambalo riba yake huongezeka kila mwaka?
Hayo ni miongoni mwa mambo machache tunayotakiwa kujiuliza sisi kama jamii kabla ya kumwambia mhitimu ajiajiri boila kumshika mkono pindi ambapo sisi wenyewe tupo maofisini tukipokea kipato kila mwisho wa mwezi na tukisubiri mafao baada ya kustaaafu.
Kabla hatujatoa kauli ya kujiajiri kwa wahitimu inabidi tujitazame kwenye kioo , je kama ni wewe ungeweza?
Changamoto nyingine kwenye kujiajiri tofauti na mtaji hasa kwenye biashara ndogo ndogo ni lukuki zikiwemo misimu ya biashara. Na sio kwamba kila mtu anaweza akafanya biashara ndogo ndogo hasa kwa watu waliojikaza masomoni wakitegema kumaliza na kuajiriwa kwani hukosa mikakati sahihi kwenye biashara na biashara zao huyumba bila wao kuelewa tatizo ni nini.
Tukirudi kwenye suala la elimu, Elimu yetu imeishia kutoa kizazi cha kukariri kilichopo kwenye vitabu ili wajibu kilichopo kwenye mtihani bila kujua kiza kilichopo mbeleni mwao wakishafunika vitabu vyao hivyo sisi kama jamii ni jukumu letu kuwapatia kurunzi hio ili kuwasaidia mbele ya safari yao.
Kwa mtazamo huo je imefika wakati wa kubadilisha mifumo yetu ya elimu ili kupunguza changamoto za elimu na ajira kwenye nchi yetu.
Huenda umefika wakati wa kutanua wigo la elimu yetu mpaka kwenye vipaji kwa kuzindua shule mbalimbalii kama vile shule za filamu, shule za mziki, shule za mpira na kadhalika kwani fani hizi zimekuwa kwa kasi na huingiza kipato vcha kutosha na hii ni kutokana na utandawazi.
Badala ya kuwaandama wahitimu wajiajiri bila kujua usuli wao wa kiuchumi wa familia zao kwanini tusiangaliekuwawezesha wahitimu kwa mikopo ya riba nafuu kwa wahitimu waliokosa ajira kwani kama wamewezeshwa kusoma kwa miaka kadhaa kwanini wasiwezeshwe kujiajiri kabla hawajakabwa na majukumu yam taani huku deni la bodi hya mikopo ya elimu uya juu likiwatandia kama wingu la mvua.
Ukosefu wa ajira kwa wahitimu umerudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu kwani wahitimu wamekuwa wakiathirika na matatizo mbalimbali haswa msongo wa mawazo kwani nguvu, juhudi na muda mwingi waliotumia kujidhatiti kwenye masomoni sawa na mbegu walizorusha kwenye miamba.
Ukosefu wa ajira kwa wahitimu pia umesababisha vijana wengi kukata tamaa na elimu kwani wanajua pia huku nako hakuna mwanga.
Picha kutoka mtandaoni.
Ni hayo tu machache kutoka kwangu jicho la mwandishi, natumaini nakala hii itasaidia kuchochea maboresho katika nchi yetu ili kuhakikisha masuala tofuati ya elimu na ajira yanatatuliwa katika nchi yetu.

Upvote
2