KERO Changamoto ya kukatika katika umeme kila siku baadhi ya nyumba mtaa wa Zavala-Kwambiki Chanika Ilala, Dar es Salaam

KERO Changamoto ya kukatika katika umeme kila siku baadhi ya nyumba mtaa wa Zavala-Kwambiki Chanika Ilala, Dar es Salaam

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi naishi mtaa wa Zavala - Kwambiki kata ya Buyuni Chanika Ilala Dar es salaam. Nyumbani kwangu na baaadhi ya nyumba za majirani zangu tumekuwa tukipata tatizo la umeme kukatika katika kila siku ikifika saa moja usiku mpaka saa nne usiku kuanzia mwaka jana 2024 mwezi wa Tisa. Nili-report taarifa hii TANESCO kitengo cha huduma zaidi ya mara tano.

Baada ya kuwasumbua sana juzi ndio wakaja watu wa kitengo cha Emergency kutoka TANESCO -kituo cha MAGENGE wakaishia kuangalia tatizo wakadai ni tatizo ni Low Voltage tukauliza kwanini sisi tu ikiwa baadhi ya majirani hawakutwi na tatizo hili?

Wakajibu shida hata meter zetu tunazotumia ni tofauti haziwezi kuhimili umeme ukiwa mdogo ndio maana unakatika katika sana.

Meter yangu ni kampuni ya INHIMETER ambazo namba za mwanzo ni 40 ila zile zinazohimili zinaanzia na 30.

Kiongozi wao akawa anaongea na mtu mwingine kwenye simu akimuelezea kuhusu Low voltage na suala la changamoto za meter hizo baadae akasogea pembeni yasisikike maongezi yao.

Akarudi kueleza nitapigiwa simu na watu wa TANESCO wakaondoka tatizo likiwa bado halijatatuliwa na mpaka leo ikifika mida hiyo ya saa moja mpaka saa nne usiku inabidi watu wawashe tochi na vitu vyote vinayotumia umeme vizimwe maana umeme unawaka, unakatika, unawaka unakatika zaidi ya mara 40 maana hata taarifa ya habari hatuangalii, watoto wanaojisomea ndio wanatumia tochi au mishumaa kusomea.

Je, TANESCO wanatusaidiaje kuhusu hili? Kama changamoto ni meter zinazoanza na 40 zina matatizo hayo kwanini walitupa ikiwa wanajua umeme wa eneo letu meter zinazostahimili ni zile zinazoanza na 30?
 
Poleni hapo inabidi muendelee kuwasumbua hata ikibidi muende ngazi za juu na kutoa hayo maelezo
Jaribu kushirikiana na viongozi wako wa mtaa muone mnamaliza vipi shida yenu
 
Back
Top Bottom