Theresia Don jh
Member
- Jul 18, 2022
- 27
- 15
Habari Tanzania, leo nina habari njema sana, lakini kabla haujajua nini hasa nataka kukueleza ni muhimu ukajua kwamba habari hii huenda unaifahamu , unaishi nayo, unaiona kwa watu wengine ama ndio kwanza, unaisikia kutoka kwangu . Natumia wino huu kukujulisha juu ya ‘AFYA YA AKILI’ .
Mwaka jana 2021 taifa letu lilipata taharuki kubwa mara baada ya taarifa zilizotolewa na shirika la afya duniani (WHO)kueleza kua zaidi ya watu milioni 7 wanamatatizo ya afya ya akili , pia ilieleza kua kati ya watu nne mmoja kati yao hua anasumbuliwa na magonjwa ya akili kama vile sonona ,bipola , fobia maalumu au msongo wa mawazo . Ni ukweli usiopingika kua katika jamii zetu , familia zetu , majadiliano yetu ni kawaida sana kuongelea kuhusu maswala kama muziki, soka, siasa , mfumuko wa bei na mengine mengi , ni nadra sana kukuta watu wakiwa wanafanya majadiliano yanayohusu afya ya akili , kitu ambacho kimefanya swala hili kua geni sana masikioni mwa watu wengi ,hii imefanya watu wengi wanaopitia changamoto za afya ya akili kutokujua dalili nyingi mpaka tatizo likiwa sugu.
Linapokuja swala la afya ya akili kila mmoja wetu anamtazamo tofauti kwani watu wengi wamekua na mitazamo tofauti kulingana na imani zao, kiwango chao cha elimu , jinsia, malezi waliyolelewa , mtindo wao wa maisha na mengineyo .Sababu za kwanini watu wengine wanapitia changamoto hizo pia zipo kwenye mitazamo tofauti.
Lakini sio siri kwamba mitazamo mingi tuliyonayo juu ya afya ya akili , na kwanini watu wanaathirika na tufanye nini kusaidiana katika janga hili imekua HASI, ukizingatia kwamba watu wengi wamepoteza maisha juu ya hili tatizo, wengine wamefukuzwa kazi ,wengine hawana mahusiano mazuri na watu wanaowazunguka kwasababu tu ya matatizo ya kitabia wanayopitia ,kuna wengine wanamakovu ya kihisia kuna waliojaribu kujiua na wakafanikiwa katika jaribu hilo athari zimekua nyingi mno.
Tumekua tukiamini haya ni matatizo yanayoweza kuwapata watu wachache tu , lakini hio sio kweli ustawi wa afya ya akili ni jambo ambalo linatakiwa kupewa kipaumbele na mtu yoyote alie hai hivyo kulinda ustawi huu ni muhimu sana kuliko tunavyofikiria.
Mitazamo hii imefanya watu wengi kutoomba msaada kutoka kwa wataalamu wa maswala ya afya pale wanapopitia pale wanapopitia changamoto tajwa kwakuhisi ‘wataonekana kama wanyonge’ ,kuna msemo maarufu wazazi hupenda kuwaambia watoto wao wakiume wakiwa wadogo kua ‘mwanaume halii’ hii imefanya wanaume wengi kuvumilia mambo mengi tangu wakiwa wadogo ,hii ni moja kati ya sababu imefanya waathirika wengi kua wanaume kwani hawaamini katika njia ya mazungumzo na mtaalamu inaweza kumfanya akapata utatuzi na ahueni kwenye tatizo lake .
Katika karne hii dunia imekua ikikumbwa na changamoto nyingi za kiuchumi ,kiafya ,kimazingira na ata kisiasa ,moja kati ya janga kubwa ni namna gani tunaanda watoto watakaokua na ustawi mzuri kimwili na kiakili , ni kawaida kumkuta mzazi akilaumu tabia za mtoto wake akiwa hajui chanzo halisi cha tatizo . Ulimwengu wa 50/50 kati ya wanaume na wanawake umepelekea wazazi kupunguza ukaribu kati yao na watoto , wakina dada wanaosaidia kazi nyumbani wanaelewa zaidi watoto kuliko wazazi wenyewe ,mtindo huu umekua ukiendelea kwenye familia nyingi sana .
Katika maeneo ya kazi ni ngumu mfanyakazi kuomba ruhusa ya kutofika eneo la kazi eti tu kwasababu ‘ana msongo wa mawazo’ kuna Ile Bosi atamuonaje ,hivyo tumekua na wafanyakazi wengi maofisini wako na changamoto za kiakili kwa sababu binafsi , hivyo wanatimiza wajibu tu ,akili zao zikiwaza changamoto nyingine kabisa walizoacha kwenye familia zao .
Ripoti nyingi huonyesha kadri mtu anavyokua na furaha ndivyo uchapakazi wake hua mzuri zaidi na zaidi.
Wanafunzi wetu wanaenda shule lakini akili zao hazipo , uwepo wa madarasa ,vitabu na walimu sio nyenzo pekee zinazoweza kumfanya mwanafunzi akafanya vizuri kitaaluma kwani umakini, usikivu na utunzaji kumbukumbu unahitajika lakini je mazingira yanayowazunguka wanafunzi wetu kwanzia nyumbani na ata shuleni umewalinda vipi kiakili ili wasipitie msongo wa mawazo ,sonona na mengineyo katika kipindi hichi muhimu maishani mwao.?Kuna watoto wengi wanaopitia matatizo ya kitabia kama vile ‘attention deficiety disorder (matatizo ya kukosa umakini) na wamekua wakiitwa ‘watukutu’ bila kupewa msaada wa kisaikolojia wengine wamekua wahalifu ,wakatili, wanatumia uraibu kwa kupitiliza na ndoto zao kuzima kama mshumaa ,je tujiulize tumepoteza wazalishaji wangapi kwenye jamii kwasababu walichukuliwa kama watukutu?
Mwanzo kabisa nilikuahidi habari njema ,niko hapa kukujuza ni nini tufanye sisi kama jamii ili tusaidiane pale tunapopitia matatizo haya ya afya ya akili ambayo kiukweli ni kilio hasa kwa karne hii ambayo dunia inabadilika na hivyo sisi pia lazima tubadilike kwani tukiishi kama walivyoishi mababu zetu karne ya 19 hatuwezi kutoboa , kitu cha kwanza ni sisi kukubali kwamba hili ni janga na tunatakiwa kulikabili kama tunavyokabili majanga mengine kama njaa, mafuriko, ukame na magonjwa , tutumie kelele kama tunazopiga wakati wa ushindi wa timu zetu pendwa zinapopata matokeo mazuri , tupaze sauti serikali isikie na watu wenye moyo wakutoa wajitokeze kulitatua tatizo hili ,wataweka wataalamu sehemu mbalimbali za nchi yetu ,kwani wataalamu wengi wako mijini na hawajafika nchi nzima kwa uchache wao .
Tupige kelele wataalamu wasogee tuwaone, tuwafate kwaajili ya huduma , lakini pia haya yote ni ndoto kama matatizo yetu tutaendelea kuyaficha kwa kuhisi ‘watanionaje’ unaemwogopa atakuonaje jana usiku alijifunika shuka akagugo ‘njia nne za kutatua stress’ . Hili swala tukizidi kuliongelea watu wataliona ni kawaida na watajitokeza haswa kupata msaada .Tusijifiche ndani , tuanze kuongelea mambo haya tukiwa sehemu zetu za starehe au ata ukiwa na marafiki .
Ni hayo tu niliyokuandalia siku ya leo naamini utakapopona wewe utasaidia mtu mwingine pia , hadi wakati mwingine
Wako Mtiifu,
TEE.

Upvote
4