Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
TATIZO LA MAJI LITAISHA KWA NAMNA HII
Chanzo Cha Picha: Freepik
Tatizo la maji katika nchi yetu hii ya Tanzania ni changamoto kubwa inayokabili nchi, Mijini na vijijini. miundombinu ya maji safi na salama isiyo na ubora ni moja ya sababu kuu. Maeneo mengi hayana mabomba ya maji ya kutosha au yaliyopo ni madogo, na yanayotegemewa mara nyingi hayafanyi kazi ipasavyo. Vyanzo vya maji vya asili kama mito na visima vimeharibika kutokana na shughuli za kibinadamu kama ukataji miti na uchimbaji madini, Mabadiliko ya Tabia Nchi kama upungufu wa mvua, hali inayosababisha ukosefu wa maji safi kutokana na Mito mingi kukauka.Chanzo Cha Picha: Freepik
Mabadiliko ya tabianchi yameathiri upatikanaji wa maji. Ukame na mabadiliko yasiyotabirika ya hali ya hewa yamepunguza kiwango cha mvua kwa kiasi kikubwa sana, hivyo kupunguza upatikanaji wa maji. Katika baadhi ya maeneo, watu hulazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji, jambo ambalo linaathiri sana afya na ustawi wa jamii, hususan wanawake na watoto.
Kwa miaka Mingi tumekuwa tukiangalia Namna moja tu ya kupata maji kupitia Vyanzo vya asili kama Mito na visima ambapo vyanzo hivi vikikumbwa na adha basi maji yanakuwa ya shida na mgao, na Serikali Pamoja na wadau mbalimbali wa maji wamekuwa chini sanaa kuangalia namna nzuri ya kukabiliana na tatizo hili, Mwisho wa siku husingizia Mvua hakuna mara hiki mara kile.
Mapendekezo yangu Juu ya Janga hili la taifa, ili ifikapo 2025 basi Tanzania tuwe na Maji ya kutosha kwaajili ya matumi ni kama Yafutayo
1: Kujenga matanki makubwa na mengi ya kuhifadhi maji
2: Kutumia Technolojia ya kutakatisha maji ya Chumvi/Bahari na kuwa maji safi
---------------------------------------------------------------------
1: UJENZI WA MATANKI MAKUBWA
Ujenzi wa matanki haya makubwa ya kuhifadhi maji unaweza kusaidia kumaliza na kukabiliana na tatizo la maji nchini Tanzania kwa njia nyingi.
Chanzo cha Picha: Mtandaoni
Pili, matanki hayo makubwa yanaweza kujengwa karibu na maeneo yenye uhaba wa maji, hasa vijijini na maeneo ya mijini yenye msongamano mkubwa wa watu na matumizi ya maji. Hii itapunguza umbali na muda unaotumiwa na watu, hasa wanawake na watoto, kutafuta maji, na hivyo kuboresha afya na ustawi wa jamii, na pia Kuchangia bei ya maji kushuka.
Tatu, matanki ya maji yanaweza kusaidia katika kuhifadhi maji safi kwa matumizi ya nyumbani, kilimo, na mifugo. Hii itaimarisha usalama wa chakula na kuleta ustawi wa kiuchumi kwa jamii, kwani maji ni rasilimali muhimu katika kilimo na ufugaji.
Uwekezaji katika matanki makubwa ya maji na Ujenzi wake ni hatua muhimu kuelekea suluhisho la kudumu la tatizo la maji Tanzania, Kama ilivyo kwa Matanki ya kuhifadhi mafuta badi tuwe na matanki makubwa zaidi kwaajili yam aji kwa mikoa yenye Msongamano wa watu
2: TEKNOLOJIA YA KUTAKATISHA MAJI YA CHUMVI/BAHARI NA KUWA MAJI SAFI
Mfumo unaotumia kutakatisha maji ya bahari kuwa maji safi unaitwa "mchakato wa kusafisha maji ya bahari" au "desalination”. Teknolojia hii inajumuisha njia mbalimbali, lakini njia kuumbili ni:
Chanzo cha Picha: Shutterstock
- Reverse Osmosis (RO) - Mfumo huu hutumia shinikizo kubwa kusukuma maji ya bahari kupitia membrani maalum inayochuja chumvi na uchafu mwingine, hivyo kutoa maji safi ya kunywa.
- Distillation - Njia hii inahusisha kuchemsha maji ya bahari na kukusanya mvuke wake, kisha kuupooza ili kuwa maji safi. Chumvi na uchafu mwingine huachwa nyuma kwenye mchakato wa kuchemsha.
Chanzo Cha Picha: Mtandaoni
- Saudi Arabia - Inaongoza duniani kwa uzalishaji wa maji kupitia desalination.
- United Arab Emirates (UAE) - Ina mitambo mingi ya desalination kwa ajili ya mahitaji ya maji.
- Kuwait - Karibu maji yote ya matumizi ya nyumbani yanatokana na desalination.
- Qatar - Hasa inategemea desalination kwa ajili ya maji safi.
- Bahrain - Inatumia desalination kwa kiasi kikubwa kuzalisha maji safi.
- Oman - Ina mitambo mingi ya desalination inayozalisha maji kwa matumizi ya nyumbani na viwandani.
- Israel - Imekuwa mstari wa mbele katika kutumia desalination kwa maji safi.
- Australia - Maeneo kama Perth yanategemea desalination kwa maji safi.
1. Distillation (Thermal Desalination):
- Gharama za awali za ujenzi: Hizi zinaweza kuwa juu zaidi, kati ya $2,000(TZS 5.2M) hadi $10,000(TZS 26M) kwa kila mita moja ya ujazo wa uwezo wa uzalishaji wa maji kwa siku (m³/day) Yaani sawa Na Lita 1,000 za maji au Uniti 1.
- Gharama za uendeshaji: Hizi zinaweza kuwa kati ya $1.00(TSZ 2000) hadi $3.00(TSZ 7,000) kwa kila mita ya ujazo ya maji inayozalishwa, kutokana na matumizi makubwa ya nishati ya mafuta au umeme.
- Gharama za awali za ujenzi: Hizi zinaweza kuwa kati ya $1,000(TSZ 2.6M) hadi $5,000(TSZ 13M) kwa kila mita moja ya ujazo wa uwezo wa uzalishaji wa maji kwa siku (m³/day). Kwa mfano, mtambo wenye uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 50,000 Yaani Lita Milioni 50 kwa siku unaweza kugharimu kati ya $50 milioni(TZS Bilioni 131,750,000,000) hadi $200 milioni.
- Gharama za uendeshaji: Hizi ni kati ya $0.50 hadi $2.00 kwa kila mita ya ujazo ya maji inayozalishwa. Gharama hizi zinajumuisha nishati, matengenezo, na uendeshaji wa kila siku.
Chanzo cha Picha: Mtandaoni
Upvote
11