KERO Changamoto ya maji Kanindo Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana

KERO Changamoto ya maji Kanindo Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Changamoto yetu kubwa kutoka Mtaa wa Kanindo Kata ya Kishiri Nyamagana Mwanza ni suala la maji hakuna kabisa.

Wakazi wa maeneo haya wanapata sana tabu ya kupata maji hata ya kunywa. Mradi wa maji ushakamilika huu mwaka sasa wananchi hawajui ni nini changamoto haswa bomba za maji kutosambazwa mitaani.

Ilifika hatua baadhi ya wananchi walikusanyika na kutaka kuchanga pesa wasogozewe maji ila wakasema maji yapo karibuni kuwafikia, sasa ni zaidi ya miaka miwili

Hivi ni baadhi ya vyanzo nya maji wanayotegemea.

m1.jpg
m2.jpg
m3.jpg
m3.jpg
m4.jpg
m5.jpg



=======================

Hapa kwetu Mwanza kuna miradi ya maji kadhaa lakini ninachojiuliza mbona kero za uhaba wa maji bado ni nyingi? Mfano kwa Wananchi wa Mtaa wa Kanindo, Kata ya Kishiri Wilayani Nyamagana.

Wananchi wa huko wengi wao hawana huduma ya maji ya bomba (MWAUWASA), hali hiyo inawafanya kutumia maji ya kisima kama mbadala.

Hali ya ukosefu wa maji si tu kwa wasio na mabomba bali hata kwa wenye mabomba kwani nao wameyaacha mabomba yao yakiwa makavu na kupanga foleni kisimani kusubiri maji ya kununua ambayo si salama.

Ameeleza kwa muda mrefu sasa toka wameanza kupaza sauti zao kuhusu kero hiyo lakini wamepewa majibu yasiyoleta utekelezaji huku wakizidi kuumia kwa kutumia maji yasiyo safi na salama ambayo hata wanyama wamekuwa wakitumia pia.

Pia, soma: MWAUWASA: Tumeandaa Mradi wa Tsh. Bilioni 8.4 kufikisha Huduma ya Maji maeneo ya Kishiri na jirani ambayo hayana huduma hiyo.
27f0dbaa-b95d-49c6-9599-3258308c3c52.jpg

d1d611de-d8a7-44b8-be75-de72d1fe633f.jpg

a6880dee-b5da-4b7d-b202-dcbe1da02bd2.jpg
 
Mwauwasa washasema hakuna shida ya maji mwanza, labda kwa mtu mmoja mmoja
 
Back
Top Bottom