KERO Changamoto ya maji sehemu ya Usagara (Nyang'omango), tunatumia yaliyotuama pamoja na mifugo

KERO Changamoto ya maji sehemu ya Usagara (Nyang'omango), tunatumia yaliyotuama pamoja na mifugo

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hapa ni MWANZA, Wilaya ya Misungwi eneo la Kata ya Usagara, Kijiji Nyang'omango, Kitongoji cha Nyaruhama katika eneo hili kuna tatizo kubwa la maji safi na salama Wananchi wanatumia maji yaliyotuama ambapo mifugo kama Ng'ombe, mbuzi, kondoo hutumia pia.

Hili tatizo limekuwa la muda mrefu kiasi kwamba Wananchi wamekata tamaa, Mbunge wa Misugwi ndugu Mnyeti ni kama hili eneo amelisusia kabisa, sioni juhudi zozote za makusudi za kunusuru Wananchi na hili tatizo.

Mkaka 2024, TIA Campus ya Mwanza walifungua tawi maeneo haya ila Wanafunzi wanataabika mtaani na ukosefu wa maji safi na salama mpaka kuathiri usomaji wao chuoni wapo, wengine wamelazimika kupanga maeneo ya mbali kama Buhongwa ili kukwepa changamoto hii.

Mamlaka husika zishughulikie tatizo hili haraka iwezekanavyo.

NB:
Hizi picha ni maji wala sio maziwa ambayo Wananchi wa eneo husika wanayatumia, na ieleweke kutoka Mwanza Mjini City Center mpaka hapa ni around 20 km, ila huduma za msingi zinakosa hii ni aibu kwa mamlaka husika.

20250120_145614.jpg

Pia lipo tatizo jingine ambalo Wizara ya Ardhi na mamlaka ya ardhi Wilayani waliangalie kwa jicho la pili, kuna eneo la makazi ya watu waliwauzia watu binafsi kuchimba moramu, hii imeacha hilo eneo likiwa hatarishi kwa watoto make mvua zikinyesha maji hutuama na kusababisha hatari, juzi nimeshangaa wanazunguka nakuandika stop kwenye nyumba za watu wakati matatizo ya msingi kama kuuza maeneo kiholela hawashugulikiwi.
 
Back
Top Bottom