JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Takwimu za Mimba za Utotoni na Ripoti za Matukio ya Ukatili Mkoani Katavi kwa Mwaka 2024
Muda: Januari – Oktoba 2024
Waliotoa taarifa za kufanyiwa ukatili
Wanawake - 2,740
Watoto (Wasichana) - 614
Wanaume - 981
Watoto - 231
Mimba za Utotoni
Watoto (Miaka 10 - 14) - 50
Watoto (Miaka 15 - 19) - 12,688
Chanzo: Madawati ya Polisi
Mkoa wa Katavi bado unakabiliwa na changamoto ya mimba za utotoni ambapo kwa kipindi cha mwezi januari hadi Oktoba 2024 jumla ya wanawake 62,265 walikua wajawazito kati ya hao watoto ni 50 wenye umri wa miaka 10-14
Takwimu hizo zimetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela wakati akitoa taarifa ya mkoa katika Kikao cha 23 cha Kamati ya Ushauri ambapo amesema mbali na umri huo pia Watoto 12,688 wenye umri wa miaka 15-19 walikuwa wajawazito.
Naye, Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amekiri kuwa kuna mmomonyoko wa maadili, amewataka washiriki wa kikao hicho kushirikiana kwa pamoja kupinga ukatili ikiwemo mimba za utotoni.
Amesema taarifa za Madawati ya Polisi zinaonesha kuna ukatili kwa Wanawake na Wasichana, Watoto wa kiume, ubakaji, ulawiti, mapenzi ya jinsia moja, mimba za utotoni na migogoro ya Kijamii.