Changamoto ya soko la bidhaa chanzo cha umasikini na ukosefu wa ajira kwa Watanzania

Changamoto ya soko la bidhaa chanzo cha umasikini na ukosefu wa ajira kwa Watanzania

Zillion

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2017
Posts
1,378
Reaction score
1,866
Asalam wanajukwaa,

Nimeona nilete kwenu mjadala wa uhusiano kati ya ukosefu wa masoko hasa kwenye bidhaa za kilimo na ukosefu wa ajira

Ukiangalia haraka unaweza usione link iliyopo kati ya umasikini wa watanzania na ukosefu wa masoko ya bidhaa zao.

Vijana wanaambiwa wafanye kazi wajiajiri kwenye kilimo, mazao yakikomaa serikali inafunga mipaka wanapata hasara kubwa na kupoteza mitaji.

Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara, wizara ya kilimo na mifugo na uvuvi ni kama wizara hizi zimeshindwa kazi au hazipo viongozi wake sio wabunifu hawana uwezo wa kutoka na kutafutia masoko wakulima
Hata korosho tu wameshindwa kuuza

Mbaya zaidi wamekuwa wakiweka urasimu mkubwa kwa wakulima wanaotaka kupeleka bidhaa nje ya nchi na wanaokuja kununua bidhaa hapa nchini, kama walivyofanya kwenye korosho.

Mfano mzuri ni serikali kuwakataza wananchi kuuza mazao yao nje ya nchi na kufunga mipaka
Huu ni zaidi ya ujuha

Binafsi sijui maafisa biashara
hivi wanalipwa kwa kazi gani
Hawa sio watumishi hewa?

Ni wakati wa serikali kutimiza wajibu wake au kuwajibishwa. Nguvu wanayotumia kukusanya kodi na kuwafunga watu kwa utakatishaji fedha, nguvu hiyo hiyo ielekezwe katika kuwatafutia masoko wakulima na kutoa ruzuku za mbolea na pembejeo muhimu za kilimo ili asilimia 75% ya wakulima wanufaike na matunda ya kodi zao.
 
Back
Top Bottom