KERO Changamoto ya Taa za kuongoza magari Stendi ya Nata (Mwanza) kutofanya kazi, lini zitatengenezwa?

KERO Changamoto ya Taa za kuongoza magari Stendi ya Nata (Mwanza) kutofanya kazi, lini zitatengenezwa?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Hizi taa za kuongoze magari zilizopo maeneo ya Kituo cha Magari cha Nata hapa Mwanza ni changamoto kubwa, hazifanyi kazi na zimekuwa zikisababisha foleni zisizo na sababu.

Eneo hilo limekuwa korofi kwa muda kutokana na kuwa chanzo cha ajali nyingi kwa kuwa kila anayepita hapo analazimika kutumia uzoefu huku kukiwa na msongamano wa magari.

WhatsApp Image 2024-10-06 at 10.47.41_21750da5.jpg

WhatsApp Image 2024-10-06 at 10.47.39_7451dda7.jpg
Hali hiyo pia ni kero kwa wanaovuka wakiwemo Wanafunzi ambao wanakuwa wengi wakati wa asubuhi na jioni.

Kutokana na changamoto hiyo watembea kwa miguu wanalazimika kujikusanya katika kundi ndipo wavuke ili kupunguza hatari ya kugongwa hali inayowafanya wachelewe katika shughuli zao huku ikielezwa kuwa askari wa usalama wa barabarani hawapatikani kwa muda wote katika maeneo hayo.

Tatizo kama hilo ni kama la Barabara ya Nyerere na barabara ya Hospitali ya Bugando nazo haziwaki hali ambayo inazidi kusababisha mtafaruku kwa madereva wa vyombo vya usafiri kila wakifika maeneo hayo.

WhatsApp Image 2024-10-06 at 10.47.39_209030a4.jpg
 
hata taa zikiwepo hiyo sehemu ina changamoto ya foleni
ofisi nyingi za mabasi zipo hapo, ni njiapanda ya kwenda bugando na mjini na kuelekea nyegezi
hapaku dezainiwa vizuri
 
Back
Top Bottom