A
Anonymous
Guest
Mimi ni mwenyeji na mkali za Dodoma, niende moja kwa moja kwenye mada yangu, kama inawezekana Waziri wa Maji aivunje Bodi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kutokana na kushindwa kukidhi utoaji huduma bora wa wateja wake.
Haiwezekani Wananchi tuna shida ya maji maeneo mengi lakini wao wapo tu na hawaoneshi jitihada za kuokoa changamoto tunazopitia, kama wanachukua hawasemi wala kuweka wazi kinachoendelea, hivyo wengi wetu tunabaki katika hali ya sintofahamu na kuteseka tukihaha kutafuta maji.
Mamlaka hii imeshindwa kusambaza maji, huduma hiyo imekuwa changamoto kwa kiwango cha juu, kibaya zaidi watoa huduma wao hawataki hata kupokea simu, unaweza kupiga weee mpaka ukachoka.
Najua mji unazidi kukua, watu wanaongezeka hivyo, uhitaji wa maji nao unazidi kuwa mkubwa, basi wafanye jambo, Waziri yuko Bungeni very comfortable wakati maji hayapo mtaani.
Kutuambia watu wameongezeka kisha hakuna njia mbadala zinazochukuliwa inakuwa haina maana.