KERO Changamoto ya usajili Chuo Kikuu Dodoma

KERO Changamoto ya usajili Chuo Kikuu Dodoma

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Joseph isuna

New Member
Joined
Jun 20, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Naomba nifikishe changamoto ya wanafunzi wanaorudi masomoni baada ya kurejea chuoni.

Tunapitia magumu sana wakati wa kufanya usajili, kwani viongozi wengi hawawajibiki kabisa kutokana na kukosa mfumo maalumu unaoweza kujiendesha, mwanafunzi anaweza kuandika barua leo lkn mpaka kuja kuipata anakuwa amefanya kazi ya ziada.

Miezi mitatu sasa nimeandika barua zaidi ya nne lkn hakuna hata moja nilioweza kupata majibu. Muda mwingine unaambiwa haionekani, maana yake imepotea.

Nashauri ujumbe huu ufikie kwa Viongozi wasiowajibika kwani wanatengeneza sura mbaya na wimbi la kukosa wanafunzi bora wakati wa udahili kwa sababu mwanafunzi anapokuwa anakosa huduma mahususi sidhani kama anaweza kuishawishi jamii inayomzunguka kuweza kujiunga na chuo hicho specifically Udom.
 
UDOM gani ambayo usajili unaandika barua mkuu? Usajili unafanyika kupitia mfumo wa Sr2 labda kama una ishues nyingine
 
Back
Top Bottom