Changamoto za Ajira Portal

amina sana kaka tusichoke kusaidiana kaka.

Huu ni moja ya udhaifu wangu kiongozi napenda sana kusaidia kiasi kwamba mwisho wa siku najikuta napoteza marafiki.

Kuna mtu alikuwa anahitaji vitabu humu JF akatangaza kila kitabu atatoa elfu 10 alitaka vitatu.

Nikamtumia vyote vitatu na vingine vya nyongeza whatsapp na kumwambia uliweka offer ya elfu 30 kwa vitabu vyote hivyo ila mie utanilipa 10k tu au ninunulie bando la 10k tigo mwezi mzima aisee, jamaa anaanza vijisababu mara sijaenda ATM mara hivi mwisho wa siku hata nikimsalimia kwamsg anasoma tu hata salamu hajibu.

Mpaka leo nimemnyamazia tu. Binadamu hao.
 
Huu ni moja ya udhaifu wangu kiongozi napenda sana kusaidia kiasi kwamba mwisho wa siku najikuta napoteza marafiki.

Kuna mtu alikuwa anahitaji vitabu humu JF akatangaza kila kitabu atatoa elfu 10 alitaka vitatu...
Kaka pole sana kwa maswaibu waenga walisema ubinadamu kazi sana ipo siku uyo jamaa atakwama mana umemsaidia na kumtatulia matatizo yake lakini si kwamba matatizo kwa binadamu yanaisha kamwe mungu atakulipa kwa namna nyingine ila usichoke kusaidia kaka, kama mtu ana shida na hilo jambo lipo ndani ya uwezo wako saidia tu kaka mungu atakulipa kwa namna nyingine.
 
Nafahamu kuwa wema kamwe hauozi kiongozi. Tuko pamoja weekend njema aisee...!
 
Professional qualification ni professional za field aliesomea kwa mfano watu wa accounts watajaza CPA, watu wa procurement watajaza CPSP etc, kitu kama hicho
 
Professional qualification ni professional za field aliesomea kwa mfano watu wa accounts watajaza CPA, watu wa procurement watajaza CPSP etc, kitu kama hicho
Yes!! Boss na maengineer wapo huko huko. Katika ile option pale kuna VETA, NIT, kwenye course name kuna Driving license na professional driving manake nini hizo options kuwepo pale??

Af pia hivi udereva tuna ucategorize vipi?? Kama Academic au Professional??
 
Msala utakuja hapa mkuu vyuo vya mtaani havijawekwa kwenye system. Pale pana board ambazo zinatambuliwa na serkali (Zaidi). Ambapo kwa mambo ya udereva kuna VETA na NIT.

Ila nahisi kuna namna nyingine. Manake wengi wamesomea mtaa tu.
 
Hivyo hivyo vyuo vya mtaani vinakuwa vimesajiliwa na VETA kutoa hayo mafunzo kwa hiyo kama ni kujaza udereva uliosomea katika Chuo kingine kilichosajiliwa na VETA unajaza tu VETA nadhani inakuwa haina shida kiongozi.
 
Professional.
 
Ipo category inayosema OTHERS so nime pick iyo others nikaweka driving licence nikaatach na chet changu cha mtaani .

Swali langu ni kuwa je kwa kuchagua iyo driving licence natakiwa niweke licence au cheti?

Pili je hii profesional si itanitambulisha kama driver? wakat mm profesional yangu ni transport officer
 
Hivyo hivyo vyuo vya mtaani vinakuwa vimesajiliwa na VETA kutoa hayo mafunzo kwa hiyo kama ni kujaza udereva uliosomea katika Chuo kingine kilichosajiliwa na VETA unajaza tu VETA nadhani inakuwa haina shida kiongozi.
Hahahaha usirahisishe saaaaana dereva aliesoma veta na aliesoma chuo cha mtaani kitaaluma wanatambulika tofauti. Kaz zikijaga zile za mkazo wanasema uwe na chet cha VETA au Cha NIT. Sasa ukipeleka cheti cha victoria driving school lazma wakukatae. Ni vinatambulika na VETA but hawana maana kua ndo VETA mkuu.

Mm dereva wa mtaani najijua [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]. Acha tuweke tu others
 
Hapa naona kujisajili hii ajira portal umekuwa ugonjwa wa taifa juz nmehangaishwa na dada flani siku nne mfululizo nikimuelekeza umiza sana kichwa na mim uwa sikubali kushindwa kumbe watu wa procurement wana maboard yao wanabidi wakajisajili na yeye bado ajajisajili yupo ananihangaisha tu
 
Wameleta mfumo wa kujisajiri mtandaoni mfumo ambao umekua na usumbufu mkubwa na hivyo kuzidisha ugumu wa ajira badala ya kuleta ufanisi

Moja ya kero ni pale ukishajaza namba yako ya NIDA unaanza kuulizwa maswali uliyoulizwaga miaka ya nyuma kipindi ulipojiandikisha NIDA! wakati namba ya NIDA inabeba maswali na mashaka yote!

Then unaulizwa ni wapi makao yako ya kudumu, ukiandika sehemu unayoishi sasa unapigwa X ukiandika ulipoishi zamani kipindi unakata NIDA unapigwa X...!

Unajaza kuwa kwa sasa upo mkoa wa Dar es salaam ,ukiingiza na wilaya sehemu uliyojaza mkoa inafutika!ukisema u submit/save unaambiwa hujajaza jina la mkoa!

Mara unaulizwa jina la kati la mama mzazi, kwa kweli kwa hali hii ukijumlisha na shida ya mtandao wetu bongo inakua ni mateso makubwa.

Tuombe kama kuna namna basi utaratibu wa awali utumike candidates watumie njia ya posta direct kuomba nafasi zilizotangazwa kwa mwajiri, iwe idara za serikali, mashirika ya umma hata serikali kuu. ule ulikua utaratibu mzuri na usiochelewesha.
 
mkuu wala usiangaike mwambie aende kwenye ofisi zao za bodi ya manunuzi kwa watu wa manunuzi hawana longolongo ni registration tu ndo inayotakiwa tofauti na waasibu mpaka upate CPA ila uyo dada aende akajiandikishe then aweze kujaza iyo ajira portal
 
Mnaturudisha Zama za zamani. Ulimwengu upo Kwenye Mapinduzi ya Viwanda Awamu ya 4 (Fourth Industrial Revolution-4IR) nyie mmeng'ang'ana na Makaratasi na P. O Box tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…