Habari JF!
Najua wahusika wanapitaga pitaga mara moja kusoma pumba zinazoandikwa humu JF, kuna nyingine zinakuwa nzuri wanazifanyia kazi ila nyingine ni pumba kabisa wanaziacha.
Pumba yangu ya leo baada kula kushiba, naishauri ajira portal ifanye upgrading ya website yao, itafute wataalam ambao wata design website ambayo itakuwa na mambo yafuatayo.
1. Kuonyesha mchakato wote wa ajira yaani kama application imepokelewa au rejected, idadi ya waliotuma maombi, screening yaani kama application imefanyiwa uchambuzi na kufanyiwa screening, ionyeshe kama MTU ameitwa kwenye interview au ametemwa na idadi ya walioitwa kwenye interview.
2. Portal iwe na uwezo wa ku-screen application based on skills za MTU maana kuna watu wameishia form 4 wanaskills za kufanya kazi za degree na kuna wenye degree wana uwezo wa kufanya kazi za diploma kwa sasa system inakagua ile education level uliojaza tu kama hai-match na tangazo unatemwa.
Lengo la system siku zote ni kuleta haki na usawa wala isiwe bias ndio maana kwny soka Siku hizi kuna VAR ili kuleta mambo sawa
Asanteni, kama nimetema pumba naomba mnisamehe nilishawahi ugua kichaa kidogo nikapona.