Changamoto za Ajira Portal

Habari wakuu?

Najaribu kuweka namba ya NIDA katika account yangu ya Ajira Portal lakini inaishia ku-load bila mafaninikio.

Mara ya nne leo inazunguka tu na kuniambia 'please wait'

Naomba msaada.

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo hilo wanalo, tena ni baada ya kubadili system yao, wamekuwa hovyo sn malalamiko yamekuwa mengi toka kwa watu mbalimbali
 
 
Nimekwamia hapa na mimi kwa kweli , Tena leo hii , Mwenye kujua hili suala. Hii screen inaendelea kuwepo hata baada ya kumaliza kujibu maswali na ku-save. Na hata nikijaribu kuapply kazi narudishwa hapa kwamba sijaweka NIN. Msaada. Natumia PC

View attachment 1446967
 
Habari wakuu?

Najaribu kuweka namba ya NIDA katika account yangu ya Ajira Portal lakini inaishia ku-load bila mafaninikio.

Mara ya nne leo inazunguka tu na kuniambia 'please wait'

Naomba msaada.

Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
sikia ndg yangu sijajua uko wapi?kama uko dar nenda pale kivukoni ukifika ulizia ofisi za utumishi wata kuelekeza ziko wapi?ila kwa jibu la haraka haraka ukitaka kuweka ( NIN) yako kwenye ukurasa wako ktk utumishi inabidi upate line yenye mtandao wenye nguvu utaona fasta na utajikuta unacheka mwenyewe na kuona ulikuwa unapoteza mda bureeee.
 
Habari zenu wakuu, mimi ni muathirika wa hili janga la ukosefu wa ajira linalotusumbua vijana wa kitanzania kila uchwao, nimekuwa nikifanya bidii za kutafuta kazi bila kuchoka kwani naamini kuwa mtafutae huwa hachoki.

Sasa niende moja kwa moja kwenye hoja, ni kwamba serikali kupitia Utumishi wana system yao inayoitwa Ajira portal ambayo inampa mwananchi nafasi ya kuomba kazi za serikalini.

Kwakweli system hii tangu ifanyiwe marekebisho imekuwa moja kati ya system mbovu ambazo nazijua, kila ninapoomba kazi za serikalini kupitia Ajira portal naambiwa failed huwezi kuomba kazi hii kwakuwa hujakidhi vigezo, wakati ukweli ni kwamba nimekidhi vigezo vyote wanavyotaka na pia vigezo vinavyotakiwa kwenye kazi husika.

Jambo hili limekuwa sugu kiasi cha kwamba si mimi peke yangu ninayeilalamikia system hii bali tupo wengi na hata tunapowatumia msg kupitia namba walizoweka hawajibu lakini tunapowapigia simu wanatoa majibu mepesi as if system haina tatizo lolote.

Tunaomba wahusika waliangalie hili mapema au kama sivyo basi tutaamini kuwa jambo hili ni mpango mkakati wa wahusika kupeana kazi kwa kujuana.

Nawasilisha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…