ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
"kutokana na uhalisia kwamba hali ya elimu kuzidi kuwa mbaya nchini hali hii imetokana na Changamoto zinawakabili walimu kama ifuatavyo:-
1: miundo mbinu mibovu.Hali hii husababishwa na serikali na wananchi kutotilia mkazo katika swala zima la ujezi wa vyumba vya madarasa pamoja na ujenzi wa nyumba za walimu barabara na kuhakikisha shule imepitiwa na barabara ambayo itawezesha upatikanaji wa misaada mbalimbali kiurahisi.
2: Imanipotofu miongoni mwa wanajamii.Licha hali ya kuwa watanzania wengi kwa sasa wameelimika na wanaendelea kuelimika kuna baadhi yao bado wanachukulia hali ya kuwa elimu inayotolewa mashuleni katima mfumo uliorasmi ipo kimaslahi ya mataifa mengine na haimlengi mtanzania kimaendeleo badi inamdidimiza kutokana na sababu kwamba inatolewa kwa nadharia zaidi kuliko vitendo.
3: ukosefu/posho/marupu rupu.kutokana na uchumi wa dunia kuwa mgumu kwa sasa umepelekea watu wengi kuwaza swala la pesa kwanza kuliko kazi nahatimaye watanzania kuisusa fani ya ualimu kwa kudai eti ualimu ni umasikini kulingana na kazi yenyewe na mshahara wake kwa mwalimu huyo.
4: udhaifu wa mitaala.mitaala ya elimu ya Tanzania haijaandikwa ili kumwezesha mwanafunzi kuyafahamu na kuyaelewa mazingira yake na malighafi yaliyomo katika mazingira na hatimaye kuweza kuyatumia kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,bali elimu hii inawafanya wanafunzi wakimaliza shule kukimbilia mijini kutafuta kazi kutokana na kutopatiwa elimu ya jinsi ya kuyatumia mazingira ya kijijini katika kujikwamua kiuchumi …..
Marehemu "John woka ' Alijaribu kufikisha ujumbe kwa serikali na jamii kwa ujumla kuhusu malalamiko pamoja na changamoto za walimu wanazopitia wakiwa sehemu zao za kazi.
"
" John woka sasa narekebisha Tabia/haki mnatetea walimu sijasikia/hivi vilio vya walimu mnavisikia/ Au mna hamua tu kuvichunia/Maisha yao Duni mnachekelea/wakifanya biashara ndogo mnawakemea/ mshahara mdogo ataishi vipi huyu?/ kama sio kuuza biki , pipi na ubunyu/ Watoto wenu wanatukana Darasani/wanapiga walimu hawana kitu kichwani/ Hivi matatizo haya yataisha lini/ OK let's Us go kijijini.....!!!/ Na hii inanitia uchungu kweli moyoni/ walimu watatu tu wapo shuleni/ wagawane masomo waingie Darasani/ Wakati mitaani walimu wamechazana/ Wakitoka Vyuoni Ajila hakuna/ Ngoja niweke hili swali langu bayana/ Bila walimu viongozi wangetoka Wapi?../ Nauliza sasa mbona mnanyamaza/.😮💨😮💨..nime save hiyo/ nitatabika Vip beer 🍺 ngisi na pweza/ sio siri walimu mnawaumiza/Toka Enzi za Nyerere hakuna unafuu/ Mwalimu Tazania anatembea kwa Miguu/ mimi siimbi kufurahisha Moyo wangu/ Naimba ili nitetee walimu Wangu/ Bila Wao mimi singejua kizungu/ Tusibishane this is point bwana/ Haki ya Mungu mimi naona uchungu/ jitahidini walimu malipo yenu kwa Mungu../
Hii ni verse ya kwanza katika wimbo wa marehemu john woka unaitwa "walimu akiwa amemshirikisha msanii " mkoloni" Production ikiwa ni mj records..
Lakini kubwa usililolijua wewe mdau wa muziki na mfuatiliaji wa page hii kuhusu huu wimbo ni upande wa hili beat., kwa mujibu wa kauli ya msanii dj snoks kutoka Crew ya mabaga fresh.
" kipindi hicho Master J , p funk majani & dj bonnie luv walikuwa wanashirikiana sana katika kazi na wote walikuwa ni watoto wa kishua .,
P funk alikuja katika studio za mj records na kufanya na sisi kazi kama Tatu (3) hivi..
Nyimbo iliyobeba jina la Abum " utatanishi tulimshirikisha msanii balozi, dj bonnie luv alitengeneza nyimbo moja na master jay nyimbo tatu (3).ilikuwa ni mwaka 2000 album ya "utatanishi"
Na project pili tulifanya na Master jay yenye mwenyewe bila kushirikiana na dj bonnie luv & p funk majani, kazi hizi zilifanywa na member kutoka band ya fm academia anaitwa producer " saidi commorie" alikuwa mpiga kinanda pale fm academia Enzi hizo..
Wakafanya album yetu ya pili inaitwa " nguzo " hii album yote ni mkono wa saidi commorie , baada ya hii album tukawa kama tumepotea kwenye Game ya Bongo fleva hatupo tena kwenye Main mainstream .. hadi tukafika uamuzi wa kurudi Tena kwa master jay baada ya ukimya wetu kama mabaga fresh kwa kipindi kirefu..
Tulipofika kwa master jay ndio tukafanikiwa kutoa ngoma inaitwa " tunataabika" lakini kama hatujafanya hiyo ngoma ya " Tunataabika " dhumuni yetu sisi kama mabaga fresh wakati tunaenda kwa master jay pale mj records, ilikuwa ni kufanya Rmx ya wimbo unaitwa "Tupo kamili Rmx" lakini tulipomwimbia master jay wimbo huo producer Master alikataa kabisa, lakini tulipomwimbia wito wa " Tunataabika " alitokea kupenda ile idea na akakubali lurekodi wimbo huo Tunataabika.
Ila akadai tumvumilie kwanza maana tayari kuna baadhi ya Project alikuwa anataka kufanya na Crew ya wagosi wa kaya nadhani mnakumbuka kuwa wagosi wa kaya ni sehemu ya makundi ya muziki Enzi hizo aliyofanya ama kuingia mkataba na mj records.
Muda huo ilikuwa ni saa nane mchana , master jay akatueleze turudi studio mida ya saa mbili usiku tuende tukarekodi wimbo wetu wa " Tunataabika "..
Baada ya hapo sisi tukaenda zetu maeneo ya Coco Beach kwenda kupumzika ili kusubili muda wa kurekodi ufike.., maana Enzi hizo studio za mj records zilikuwa karibu na maeneo ya Coco beach,mida ya saa mbili usiku tukasogea pale studio kama yalivyokuwa makubaliano yetu sisi mabaga fresh na master jay .
Tukaingia studio tukaaza kutengeza beat, master jay akatengeneza beat sisi tukaingiza Vocal katika ile Beat.. lakini baadae producer Master jay aliiuza ile beat . , kuna washkaji walifika pale studio kusikilizishwa beat na ikapelekea kuipenda ile beat yetu. Wale waskaji wakasema mbona hii beat kali , producer Master jay akadai Yes! Naweza kuwapa beat hiyo , nyakati hizo sisi hatupo studio. Kisha sisi hatutengenezee beat nyingine maana sisi tulikuwa tunafanyiwa bure , kwahiyo hata ile beat ilikuwa kama support yake master jay kwetu ili tuweze kurudi kwenye Main stream kwahy master jay ndio kilichomfanya ajiamini hadi kufikia kuuza beat yetu kwa msanii John woka akiwa na mkoloni na beat yetu ndio hii inasikika katika wimbo wa marehemu john woka unaitwa "walimu"
Beat halisi ya nyimbo yetu ya ngoma inaitwa" Tunataabika " ni hiyo inayosikaka katika wimbo wa marehemu john woka ft. Mkoloni " walimu"
John woka na mkoloni waliipenda ili beat na kumpelekea kuinunua kwa master jay , wakaweka vocal na mgoma ikatoka ika hit mpaka leo. Alipofika producer saidi commorie pale studio za mj records master jay alimpa said commorie zile vocal zetu na producer saidi commorie akatengeneza hii beat ambayo ndio mpaka leo imefanya ile ngoma yetu " Tunataabika " ku hit sana ,
#funguka
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
anadai original beat ya ngoma yao ya "Tunataabika " ilikuwa ni hii beat katika wimbo huu wa John woka unaitwa " walimu" sema mistake na Tamaa za producer Master jay kutoka studio za mj records, alijikuta ameingia Tamaa na kufikia uamuzi wa kuuza ile beat ya mabaga fresh , kuwabadirishia mabaga fresh beat nyingine..
Ambayo ndio hii mnaisikia katika ngoma but before