Changamoto za elimu tanzania- nafasi ya serikali na jamii yake

Nagarica

Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
12
Reaction score
4
Ni janga la kitaifa...na dalili ya kifo cha Taifa...
Haya ndiyo maneno niliyomjibu binamu yangu miaka mitano (5) iliyopita alipokuwa akinipa matokeo ya mtihani wa Taifa Kidato cha nne Tanzania kwa njia ya simu nikiwa nipo safarini. Kipindi hicho ni takribani asilimia 26 ya Watahiniwa walifeli.

Miaka mitano (5) baadae yaani mwaka 2012..matokeo ya Mtihani waTaifa wa kidato cha nne yanatangazwa, safari hii ni 52% Wamefeli..kwa mara nyingine tena napokea matokeo kupitia mtu yuleyule kwa njia ya simu..Safari hii anaanza kwa kusema, " Kaka kile kifo cha Taifa kimekaribia sana sasa ni mara mbili ya ile asilimia ya miaka 5 iliyopita, najua hukumbuki.." Kwa kauli hii nakumbuka kauli yangu mwenyewe. Safari hii sikushtushwa na haya matokeo kwa sababu zifuatazo;

1. Walimu ni kada ambayo kila kukicha thamani yake inashushwa na serikali yetu kwa kauli za kisiasa za kukejeli Walimu hasa wanapodai stahili zao

2. Kila kukicha ualimu unabakia kuwa ni alternative ya wale ambao hawakufanya vizuri sana katika mitihani yao ya Taifa, hivyo hawakupata nafasi katika ndoto zao.

3. Maslahi mabovu wanayolipwa walimu yanakatisha tamaa

4. Mazingira magumu ya kazi, hata sehemu nyingine hawana pahala pa kuishi wala mawasiliano..cha kujiuliza ni kwamba mbona mitihani inafika? Huduma zinashindikanaje?

5. Uhaba wa kupindukia wa Wawalimu hasa vijijini huku kukiwa kuna mlundikano wa Walimu mijini..mfano shule kijijini ina walimu wawili..nyingine mjini ina Walimu zaidi ya thelathini

6. Malezi ya kibwenyenye tunayotoa kwa Watoto wetu..na hivyo kutowafundisha stadi za maisha na umuhimu wa kujituma katika elimu

7. Usimamizi mbovu na ukaguzi usio wa kutosha kwa shule zetu

8. Elimu kutokupewa kipaumbele cha kutosha na serikali na badala yake kuangalia mianya ya kujiimarisha kisiasa..mfano; kilimo kwanza; utakuwaje na kilimo bora kwa watu wasiosoma?

9. Na mengine mengi.


USHAURI;
Katika yote niliyoyataja kufanya kinyume chake ni kuleta tija. Huo ndio mtazamo na ushauri wa bure kwa serikali na jamii nzima ya Watanzania katika kurekebisha msiba huo unaonyemelea Taifa.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…