SoC02 Changamoto za Elimu ya Tanzania

SoC02 Changamoto za Elimu ya Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

leekingroy

Member
Joined
Jan 6, 2016
Posts
5
Reaction score
2
UTANGULIZI

ELIMU YA TANZANIA
Elimu ya Tanzania ni elimu ya kumjenga mwanafunzi kitaaluma ila sio kujitegemea. Asilimia kubwa sana ya wanafunzi wa Tanzania hawatumii elimu waliyo ipata katika masomo yao kujinufaisha katika maisha baada ya kuhitimu elimu katika ngazi yoyote ile.

Elimu ya VITENDO ni elimu yenye kumjenga zaidi mwanafunzi ili aweze kujiandaa katika kukabiliana na maisha bila ajira kipindi akiwa katika harakati za kutafuta ajira. Elimu ya sasa haimjengi kijana katika kutumia akili na ujuzi kujikwamua katika kukabiliana na changamoto za maisha.

KASORO ZA ELIMU YA SASA
Elimu ya sasa kwa nchi yetu ni elimu iliyo jikita kwenye nadharia na si vitendo. Hii inapelekea wanafunzi wengi kukariri nadharia zilizo andaliwa na walio fanya vitendo zaidi na kuandika nadharia hizo katika machapisho ya vitabu.

Elimu yetu inamjenga mwanafunzi katika kutimiza wajibu na sio kujituma kiakili katika kutimiza jambo la kitaaluma ambalo litamsaidia katika kujiengua katika maisha au kujijenga kitaaluma katika kutoa huduma katika jamii inayo mzunguka.

Elimu ya nchi yetu haimpi nafasi mwanafunzi kuhoji mazingira yanayo mzunguka, bali inamfanya akariri yale yanayo endelea bila kuhoji kwanini yanaendelea na yanaendeleaje na kwa namna gani yanatendeka. Elimu yetu inamfanya mwanafunzi akariri nadharia ya vitu vilivyo katika maandishi zaidi na sio kuona jinsi vilivyo kwa uhalisia wake.

CHANGAMOTO ZA ELIMU YA SASA
Madhara ya Elimu ya sasa iliyo jikita katika nadharia inajionyesha dhahiri katika maisha ya vijana wa kitanzania ikiwemo vijana wa elimu ya juu (chuo kikuu) ambao nintegemezi katika maendeleo ya taaluma walizo somea. Wanafunzi wengi hawatumii elimu yao kufanya mabadiliko yenye tija na kuleta mabadililo katika nchi kwa kuwa Elimu yao haija waruhusu kuwa wabunifu au kufanya maboresho kwenye chapisho zilizopo.

Vitabu vinavyo tumika katika utoaji wa Elimu ni vitabu vilivyo fanyiwa utafiti wa kimatendo na kupata nadharia ambayo ni maboresho ya machapisho yaliyo pita. Katika hali ya kawaida, Tanzania hakuna mwanafunzi aliye chapisha machapisho yenye kuboresha nadharia zilizopo katika maktaba za mashule au vyuo kwa kuwa Elimu aliyo ipata haimpi nafasi ya kuchambua machapisho yaliyopo na kuyafanyia mabadiliko, badala yake sekta ya elimu inasubiri machapisho kutoka nje ambayo yamefanyiwa mabadiliko ya uchambuzi kutoka kwa wanafunzi wa elimu sawa na tulio nao katika nchi yetu.

Elimu yetu haimpi mwanafunzi nafasi ya kutambulika kimataifa, mwanafunzi anapo maliza elimu yake ya juu hata lugha inakuwa changamoto. Kama lugha tu inakuwa changamoto, je? Mtaala aliyo somea nadharia itampa changamoto sana katika nafasi za kazi.

Mpaka leo vijana wengi hawajui namna ya kutumia mifumo kama ya kuombea ajira za serikali yaani Utumishi Ajira Portal na Tamisemi na mifumonya ajira za NGO na sekta binafsi, hii inatokana na akili kutokuwa inatumika wakati akiwa darasani.

Vijana wengi hawatambui namna mifumo inafanya kazi kwa kuwa wamezoea kupewa maelezo bila kufanya vitendo. Vijana wengi haswa wenye elimu ya juu hawajui namna ya kujituma katika kuboresha taaluma iliyopo kwa kutoa mifumo mipya yenye kuinua elimu ya nadharianya sasa katika ngazi zote za elimu. Vijana wanajua kutumia mitandao ya kijamii zaidi ila hawajui kutumia Kompyuta kwa manufaa yao ya baadae katika kujikwamua kwa taaluma ya kutenda.

NINI KIFANYIKE KUBORESHA ELIMU
Elimu ya nchi yetu inatakiwa iwe elimu yenye kumjenga mwanafunzi katika kuelewa mifumonya kila kilichopo kinavyo fanya kazi. Kuweka mifumo ya utendaji zaidi itajenga tija na ufaulu kwa wanafunzi kutokana na mwanafunzi kuelewa nadharia iliyopo katika vitendo. Mwanafunzi anapo tenda zaidi, nadharia inaeleweka zaidi kwa kuwa taaluma inabaki katika akili ya mwanafunzi.

Mfano mzuri wa nadharia ya vitendo ni mtoto mdogo kujifunza kula chakula peke yake baada ya kuona kitendo cha kula kutoka kwa mtu mwengine. Dhana hiyo inaonyesha kwamba vijana wetu tukiwajengea nadharia ya vitendo zaidi, nchi yetu tutapata wataalamu wenye kujua jambo kwa kina kwa kuwa watakuwa wamefanya vitendo katika taaluma zao na kuweza kuleta mabadiliko hata katika suala la uchambuzi.

Katika maktaba zetu, hakuna kitabu cha Profesa wa kitanzania kinachotumika darasani kama sehemu ya mtaala, bali vitabu vilivyopo ni nakala za vitabu vilivyo andaliwa na wanafunzi wa nje ya nchi katika maabara ya mbali. Hii inapelekea hata mwanafunzi wa elimu ya juu kushindwa kujiongeza kitaaluma kwani anategemea machapisho ya mwanafunzi wa zake aliye na ujuzi wa vitendo alivyo weka katika nadharia.

Nchi yetu ikiwekeza kwenye nadharia ya vitendo kuanzia elimu ya awali mpaka elimu ya juu, tutajenga taifa lenye vijana wabunifu, lenye vijana wachakarikaji, vijana wenye kuchambua nadharia na kuboresha mifumo au kuweka mipya yenye kuleta tija katika nchi yetu. Vijana wa sasa wengi wapo mitaani kujihusisha na shughuli ambazo haziendani na taaluma zao kwa kuwa taaluma aliyo somea haimsaidii kujijenga au kujenga nchi wala kuleta mabadiliko katika taaluma aliyo somea.

SULUHISHO
Elimu ya Tanzania imetujenga hata sasa tumekuwa watu wazima na kujituma katika kuijenga nchi yetu, ila haijatujenga kujituma kitaaluma badala yake kutimiza taaluma iliyopo ya kigeni. Elimu yetu haitupi nafasi ya kubuni miundombinu yetu wenyewe yenye kuleta mabadiliko katika soko la dunia na katika sayansi ya afya au teknolojia na maarifa.

Tunatumia na kutegemea kilichopo tayari, ambacho hakina manufaa kwetu katika kujinasua kwenye ushindani wa kitaaluma duniani. Tanzania hatujawahi shiriki katika matamasha ya teknolojia kwa kuwa hatuma teknolojia yetu wemyewe bali tunatumia zilizoletwa na wageni, hata zikiwa na kasoro tunashindwa zitatua kasoro kwa kuwa taaluma yetu inatuzuia kuweza kufanya maboresho au mabadiliko.

Viongozi wa serikali yetu, suala la Elimu ya nchi yetu bila kuiboresha, hata maendele yanasuasua kwa kukosa wataalamu ambao wanaweza kuchambua jambo kwa kina kwa kulielewa wakiwa ngazinya elimunya awali mpaka kufikia chuo kikuu. Tuinuke na kubadili mfumo wetu wenye kuleta tija ya maendeleo na kuinua uchumi kwa kuwa na teknolojia yetu na machapisho yetu tofauti katika fani tofauti.

Ifahamike kwamba mataifa yaliyo endelea yana teknolojia zake ambazo zinatofautiana. Na hiyo ni kutokana na elimu waliyo wapa vijana wao katika kutoa mchango wa kuboresha miundo mbinu sio katika uchumi pekee, bali hata katika sekta ya usalama wa nchi, na masuala ya ufanyaji kazi kwa watumishi wa nchi katika sekta zote, za kibinafsi au kiserikali.

msingilib.jpg

MITIHANI%20YA%20DARASA%20LA%20SABA%20MORO%202.jpg

image-6606.jpg
 

Attachments

Upvote 0
Back
Top Bottom