Changamoto za kiuhasibu na kikodi kwa kampuni nyingi za clearing and forwarding Tanzania

Changamoto za kiuhasibu na kikodi kwa kampuni nyingi za clearing and forwarding Tanzania

Joined
May 22, 2017
Posts
51
Reaction score
21
Kutokana maarifa pamoja na uzoezi wa zaidi miaka saba (7) tulionao kwenye eneo la Uhasibu(Accountancy) na kodi (Tax consultancy) nimebaini changamoto ambazo kampuni nyingi za CLEARING & FORWARDING zinakumbananazo na kupelekea madeni makubwa kikodi na hatimaye kufa au kuendeshwa kwa kusuasua:

Msingi wa changamoto hizi ni uhasibu na kodi (Tax and accountancy challenges), kama ifuatavyo:
✅kuchanganya fedha za kuendeshea kampuni na fedha za wateja (Commingling company’s operation account and client trust account), Hii ni changamoto kubwa sana na inatokea Karibia kampuni zote za Clearing and forwarding hususani kampuni ambazo hazina Mifumo ya kiuhasibu na wataalamu wakihasibu wenye sifa sitahiki na wenye kuweza kushauri kutengenesha fedha za kuendeshea kampuni na fedha zinazopokelewa kutoka kwa wateja ili kuepusha makosa ya kiuhasibu ambayo mara zote hupelekea kodi kubwa baada ukaguzi wa hesabu kutoka TRA (After TRA’s examination or Auditing of financial reports).

✅Kutothamini na kufuata ushauri wa kitaalamu, Hii pia ni changamoto kubwa sana kwenye tasnia ya Clearing and forwarding kwa sababu wengi wa wamiliki wa biashara hizi wamekua hawathamini eneo uhasibu na kodi kwa kutofanya uwezekaji wowote au kutolichukulia eneo la uhasibu na kodi kwa umuhimu unaotakiwa kama misingi mikuu kwenye uhai wa biashara yaani kitaalamu ongoing concern of business ili kujihakishia uwepo wa biashara ni lazima kuingia gharama kwa kupata wataalamu sahihi kwenye eneo la uhasibu na kodi vilevile kulipa kipaumbele eneo hili.

✅Kupata elimu kupitia ushauri wa wataalamu kabla na baada ya kufungua biashara ya Clearing and forwarding,watu wengi huwa wanawiwa kufungua na kufanya biashara ya tasnia hii kwa kufikiria na kuzingatia zaidi faida ya kifedha zaidi bila kuwa na elimu ya kutosha katika maeneo muhimu kikodi na uhasibu.

✅Kutozingatia matakwa ya sheria ya wakati na uwasilishwaji wa ritani mbalimbali za kikodi (Due date and submission of tax returns), wamiliki wengi wa kampuni za Clearing and forwarding wamekuwa na mazingatio madogo sana kwenye kujua umuhimu wa sheria mbalimbali za kodi kama vile “Income tax act” hasa kwenye maeneo yanahusu muda wa kuwasilisha ritani na adhabu za kuchelewa kuwasilisha au kutowalisha kabisa ritani na hatimaye kupelekea madeni makubwa yanatokanayo na adhabu mbalimbali za kukiuka sheria hii ya kodi(Income tax act)

✅Kutotoa nyaraka za biashara kwa wateja, wamiliki wengi wa kampuni za Clearing and forwarding wamekua na changamoto kubwa sana ya kutotoa risiti za kielekroniki (EFD receipt, VFD receipt or Fiscalized invoice),wakidhani wanakwepa kodi kwa kutotoa risiti za mauzo jambo ambalo si kweli kwasababu shughuli za Clearing zina mfumo wa TANCIS ambao unarekodi idadi ya kazi(Consigments) zilizofanyika ndani ya mda fulani hivyo mara nyingi baada ya mwaka wa kodi kuisha na kufanyiwa ukaguzi, TRA hugundua mapufu ambayo hupelekea adhabu kubwa na hatimaye kampuni kuwa na madeni makubwa ambayo yanaathiri uendeshaji wa kampuni na kupelekea kufa au kuendeshwa kwa kusuasua sana.

✅Kukosa mfumo na kutunza nyaraka za biashara, Hii pia ni changamoto kubwa sana kwa kampuni nyingi za Clearing and forwading kwa sababu ili kuweza kuandaa hesabu za kampuni ni lazima kuwe na mfumo mzuri pamoja na utunzaji mzuri wa nyaraka mbalimbali za biashara,kutokana na ukweli kwamba kampuni nyingi zinakosa sifa tajwa hapo juu hupelekea uandaji wa hesabu za mwaka husika wa kodi za kampuni kuwa na makosa mengi hatimaye kupelekea makapuni mengi kuwa na madeni makubwa ya kodi baada ya ukaguzi wa TRA.

✅Kukosa mipango ya kikodi na kiuhasibu (Tax and Account planning), makumpuni mengi kutokana kutozingatia kada ya utaalamu wa kodi na uhasibu yanajikuta yakifanya biashara pasina kuzingatia wala kujua madhara yoyote ya maamuzi ya uongozi kwenye uhasibu na hatimaye kupata madhara kutengeneza madeni makubwa ya kodi.

✅Kukosekana uwazi wa uendeshaji wa makampuni ya Clearing and forwarding, hii pia ni changamoto kubwa kwa uongozi au wamiliki wengi wa kampuni hizi wamekua wakificha au kuzuia taarifa muhimu kwa wahasibu kutokana na uelewa mdogo hasa wakati wa uandaji wa hesabu za kampuni na hatimaye kupelekea assessment za madeni makubwa ya kodi baada ya ukuguzi wa TRA ambao huwa wanagundua mambo mbalimbali ambayo huongeza mzigo mkubwa wa kodi.

Kwa ushauri zaidi kuhusu huduma zetu wasiliana nasi kupitia:
Simu:0712685025/0783262125
Barua Pepe:momsconsultingltd@gmail.com

#Miongozo ya kitaalamu kwa Usalama na ukuaji wa biashara
#Momsconsulting
#Consultant_Silwano
 
Back
Top Bottom