Wamba de Wamba
Member
- Sep 2, 2013
- 16
- 2
Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Naibu waziri wa Elimu,Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Elimu,Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu.
Naamini kwa hivi sasa moja ya mambo makubwa yanayotikisa sekta hii ni namna ya kuinua taaluma katika Taifa letu hili.Ipo mipango mingi kedekede ambayo mumeiweka na inahitaji utekelezaji. Moja wapo ni huu mkakati uliozinduliwa majuzi "MATOKEO MAKUBWA SASA KATIKA SEKTA YA ELIMU". Siko hapa kuubeza mkakati huu kwani sijaona kufanikiwa k wala kufeli kwake. Wasi wasi wangu mkubwa sana katika Taifa letu siku zote ni juu ya hawa washika dau walioko chini ambao ndiyo watekelezaji wakubwa. Mengi tumeyaona yamekuwa yakipangwa lakini yanapofika ngazi za chini mfano Halmashauri ndiyo hapo upotoshaji unapoanzia yaani kuna watu hata hamwamwogopi Muumba wa mbigu wapowapo tu kwa lengo la kupotosha mambo. Wakuu wa Idara katika Halmashauri nyingi hawapatikani katika njia sahihi, wengi wao ni ile hali ya uswaiba.
Ebu nirejee sasa kwenye kiini cha changamoto niloitaja hapo juu hususani baada ya kufika wilaya ya Magu nakukuta sintofahamu katika kada ya Elimu ya sekondari.Japo ambalo lilinishitua sana ni kile kitendo cha Ofisi ya SEKONDARI kuwa inahamahama mara leo ipo mtaa wa National, mara kesho ipo mtaa wa Nyanguge (Karibu na Guest ya Shinyanga) na leo ipo mtaa wa Itumbili. Je kesho itakuwa wapi? Tutaambiwa imepelekwa Ibidanja. Lakini hapa tatizo ni nini na kwa maslahi ya nani na mbona hivyo? Majibu yapo peupe kwa kila yeyote mwenye dhamana akifika pale ataambiwa hata na Mwananzengo.
Japo jingine la kushitusha na la ajabu ni kile kitendo kilichofanyika katika Shule ya Sekondari Magu ambayo ni Shule pekee ya A' LEVEL katika halmashauri hii. Shule hii inao walimu wenye shahada za awali zaidi ya robo tatu na wenye Shahada za uzamili wawili kwa mujibu wa takwimu zilizo hivi sasa. Isitoshe pia Wilaya hii iko na walimu wenye shahada za awali wengi tu kama zilivyo wilaya zingine hapa nchini. Pia wilaya hii inao wakuu wa shule wengi tu wenye shshada za awali. Jambo la kushangaza ni, baada ya mkuu wa shule alokuwepo mwanzo kuhamishwa kupelekwa jiji la mwanza kwa kazi nyingine, Halmashauri imeamua kupeleka mkuu wa shule mwenye kiwango cha DIPLOMA. Hivi hapa tunajenga au tunabomoa???? Ukweli bila kuficha, kilichofanyika hapa ni uswaiba mkubwa. Halafu si shule hiyo tu na hata shule za O'LEVEL, HALMASHAURI IMEFANYA UTEUZI WA WAKUU WA SHULE WENYE NGAZI YA DIPLOMA, HIVI TUNAJENGA AMA TUNABOMOA?
Wiki jana katika semina ya walimu wa Sayansi inayofanyika Mwanza, alisikika Afisa Elimu wa Mkoa akisema " Kwani kuwa n a Masters ndiyo lazima uwe Mkuu wa Shule". Hapa kuna jambo si bure ( inferiority complex).
Ndugu zangu, wenye dhamana , munayaona hayo. Je tutafanikiwa n a mkakati wetu huo wa big results??. Ebu fikeni halmashauri hii mjionee matatizo yaliyopo hususani kwa halmashauri yaenyewe na wakuu wa shule wanaojiita miungu watu.
Mwisho, naomba kuwasilisha changamoto hii ili ufatiliaji wake ufanyike.