Changamoto za Kupata Ujauzito kwa Wanawake Wenye Umri Zaidi ya Miaka 35

Changamoto za Kupata Ujauzito kwa Wanawake Wenye Umri Zaidi ya Miaka 35

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Moja ya sababu inayoleta matatizo ya kuzaa pale umri unapokua mkubwa ni kupevushwa yai mara chache kuliko kawaida.

Kadiri wanawake wanapoendelea kukua mizunguko yao ya hedhi inaanza kubadilika na mayai kushindwa kupevushwa kwa wakati. Idadi ya mayai na ubora wa mayai unapungua, mwanamke anapofika umri kati ya miaka 30 mpaka 40. Utafiti unaonyesha ubora wa mayai unaweza kuongezwa ihali idadi yake haiwezi kuongezeka.

Virutubisho vya “myo-inositol”, asidi ya foliki na “melatonin” vimeonyesha kuongeza ubora wa mayai na kazi za mfuko wa mayai.

Sababu nyingine zinazofanya kupata ujauzito baada ya miaka 35 kuwa vigumu ni pamoja na:

Maambukizi au upasuaji uliosababisha kovu kwenye tishu maeneo yanayozunguka mfuko wa mimba,mirija ya falopiani au mlango wa kizazi cha mwanamke.

Ugonjwa wa “endometriosis”.

Uvimbe katika mfuko wa uzazi.

Upungufu wa uteute ndani ya mlango wa kizazi.

Magonjwa ya kudumu/sugu kama shinikizo la damu au kisukari.

Kuharibika mimba pia ni tatizo kubwa kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35. Hii inasababishwa na ongezeko la mabadiliko ya jenetiki za uumbaji. Wanawake wenye umri kati ya miaka 35-45 wana nafasi kati ya asilimia 20-35 ya mimba kuharibika

Ni nini nifanye niongeze nafasi ya kuzaa baada ya umri wa miaka 35?

Kujaribu kujifungua baada ya miaka 35 linaweza kuwa jambo la kuelemea, lakini kuna mambo mengi ya kufanya kukusaidia kushika ujauzito haraka.Yafuatayo ni mambo ya kukumbuka:

Andaa ratiba ya kuonana na mtaalamu wa uzazi – wewe pamoja na mshauri wako wa afya mnaweza kupitia historia ya matibabu yako, matibabu ya sasa na maisha yako kwa ujumla. Kwa kufanya hivi, kunasaidia kuyagundua matitizo na wasiwasi wowote hasa unapojiandaa kupata ujauzito baada ya miaka 35.

Wanawake wenye umri mkubwa wanachukua mda kupata ujauzito – kuwa na imani pale unapochelewa kupata ujauzito, kumbuka wastani wa namba ya kupata ujauzito kwa wanandoa walio na umri zaidi ya mika 35 ni 1-2 kwa mwaka.

Mwanamke aliye na afya kimwili,kiakili na kihisia anaweza kupata ujauzito – pombe,sigara na matumizi ya kahawa(vinywaji vyenye kafeni) zinaweza kupunguza nafasi ya wewe kupata ujauzito. Pia kuwa na uzito mdogo au mkubwa sana inaweza kuingilia ufanyaji kazi wa homoni.

Angalia ishara za mwili wako zitakazo kusaidia kujua wakati gani ni wa kufanya ngono ili kupata ujauzito – rekodi jotoridi la mwili na majimaji ukeni ili kujua muda muafaka wa kufanya ngono.

Ishara hizi zitakusaidia kujua ni wakati gani yai linapevushwa ndani ya mwili wako na kama yai lako linapevushwa kwa wakati.

Mtembele mshauri wako wa afya kama hujafanikiwa kupata ujauzito baada ya miezi sita ya kufanya ngono – Kutana na mshauri wako wa afya kujadili uwezekano wa kupima uwezo wako wa kupata ujauzito. Kwa wakati huu unaweza kumtembelea mtaalamu wa maswala ya uzazi.

Tumia kirutubisho chenye myo-inositol (virutubisho vinavyotumika kutibu watu wenye uvimbe kwenye mfuko wa mayai) kukusaidia kuboresha mayai yako.
 
Natumaini utatuletea na matatizo ya mwanaume yanayoweza kumzuia mwanamke wa umri huo kupata mimba. Kwa sababu ukweli ni kwamba, mama anavyoendelea kuzeeka, baba haendelei kuwa kijana.

Pia kuna wababa wenye unhealthy lifestyles kama kuvuta sigara, ulevi uliopitiliza, kutofanya mazoezi na ulaji mbaya (manyama kwa pombe kwa wingi, vinywaji baridi vibaya kama soda, nk) vinavyopunguza uwezo wa baba kutunga mimba, ikiwemo uwezo wa kutoa spermatozoa za kutosha na zenye nguvu ya kutosha.

Pia vitu hivyo huleta magonjwa mengi ikiwemo, saratani, kisukari, magonjwa ya moyo, kupuguza nguvu za kiume na mengine mengi. Kwa mfano, kama baba alianza kuvuta, kunywa pombe na mambo mengine ya mtindo hovyo wa maisha akiwa kijana, wengine huanza mapema zaidi, hicho ndicho kipindi cha matatizo kujitokeza!

Hivyo muhimu kuyaeleza yote haya, kabla hatujatoa hitimisho. Wako wamama wengi waliozaa watoto wazuri tu baada ya miaka 35, hivyo tatizo haliwezi kuwa la mama peke yake. Tueleze.
 
Natumaini utatuletea na matatizo ya mwanaume yanayoweza kumzuia mwanamke wa umri huo kupata mimba. Kwa sababu ukweli ni kwamba, mama anavyoendelea kuzeeka, baba haendelei kuwa kijana....
Nguvu za kiume,tofauti na nguvu/uwezo wa kuzalisha.

Nguvu za kiume: Hii dhana hutumiwa kama kushndwa kistahimil tendo mda mrefu au kidogo kupita maelezo.(inahusishwa na hofu,chakula,vivywaji au asili).

Nguvu/uwezo wa kuzalisha: Dhana hii huchukuliwa kitendo cha kutoa mbegu yenye uwezo wa kutunga mimba(bila dosari za mikia mifupi ya shahawa, shahawa zisizoweza kufika ktk ovar ya ke. Na mengine meng ya kitaaalamu).

NB : MTU anaweza akawa na nguvu za kiume(sex mda mrefu/wastan ) lakin akawa hana uwezo/nguvu za kudhalisha kama mwanaume.

Kwahyo KIBABU CHA MIAKA 70 KINAWEZA PIGA GOLI MOJA,KIKATUNGA MIMBA.

Mtoa mada ,nadhan amejikita kueleezea upande unaoteseka zaid ILI KUUUSADIA.
 
Nguvu za kiume,tofauti na nguvu/uwezo wa kuzalisha.

Nguvu za kiume: Hii dhana hutumiwa kama kushndwa kistahimil tendo mda mrefu au kidogo kupita maelezo.(inahusishwa na hofu,chakula,vivywaji au asili)...
Siyo, sikukataa maelezo kuwa mama wa 35 ni shida kuzaa na pia hata akizaa, mtoto aweza kuwa na shida. Hiyo haimaanishi kuwa baba hawezi kuwa na shida ikiwemo umri!

Tumeshuhudia wangapi wanakufa kifuani kwa wanawake? Lakini pia mara nyingi tu mama ameshindwa kupata mimba na kulaumiwa , kumbe shida ni ya mwanaume; matatizo yako kote kote! Na hao vibabu wanaotia mimba ni wangapi?

Na wale wanaooa wengi "husaidiwa" na wenzao! Pande zote mbili ziangaliwe!
 
Siyo, sikukataa maelezo kuwa mama wa 35 ni shida kuzaa na pia hata akizaa, mtoto aweza kuwa na shida. Hiyo haimaanishi kuwa baba hawezi kuwa na shida ikiwemo umri! Tumeshuhudia wangapi wanakufa kifuani kwa wanawake? Lakini pia mara nyingi tu mama ameshindwa kupata mimba na kulaumiwa , kumbe shida ni ya mwanaume; matatizo yako kote kote! Na hao vibabu wanaotia mimba ni wangapi? Na wale wanaooa wengi "husaidiwa" na wenzao! Pande zote mbili ziangaliwe!
And by the way, sigara mbali na impotence, pia huleta infertility kwa wanaume!
 
Siyo, sikukataa maelezo kuwa mama wa 35 ni shida kuzaa na pia hata akizaa, mtoto aweza kuwa na shida. Hiyo haimaanishi kuwa baba hawezi kuwa na shida ikiwemo umri! Tumeshuhudia wangapi wanakufa kifuani kwa wanawake? Lakini pia mara nyingi tu mama ameshindwa kupata mimba na kulaumiwa , kumbe shida ni ya mwanaume; matatizo yako kote kote! Na hao vibabu wanaotia mimba ni wangapi? Na wale wanaooa wengi "husaidiwa" na wenzao! Pande zote mbili ziangaliwe!
Uko sahihi ndugu,asante kwa kunielewesha.
 
And by the way, sigara mbali na impotence, pia huleta infertility kwa wanaume!
God helps us.

Maana nasikia ,wanaopata moshi wa sigara(bila kuvuta) kutoka kwa mtu anayevuta sigara,huwa anapata madhara Mara 2 zaid ya mvuta sigara mwenyewe.
 
Vipi mwanamke ambaye hakuwahi kupata hedhi tangu anabaleha hadi sasa ana miaka 29 tatizo linaweza kuwa nini
 
Back
Top Bottom