Changamoto za Mtandao wa TTCL kwa wateja wake

Changamoto za Mtandao wa TTCL kwa wateja wake

Buza Kwa Mpalange

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2020
Posts
268
Reaction score
156
Hatimaye TTCL wameanza kukosa ubunifu kabisaaa

👉Now wapowapo tu ubunifu ni 0.05%. Badala ya kuumiza kichwa kuboresha huduma, wameenda kumsainisha Nandy kwenye lebo yao ya Rudi Nyumbani Kumenoga ili wazurure kufanya shoo mikoani.

👉Unapiga menyu yao ya kuangalia salio. Ujumbe unakuja kuletewa masaa mawili mbele au usipate kabisa.

👉Mteja kwao wanatuona fala tu. Ukipiga simu ni mwendo wa Ok, yes, poa, rudinyumbani kumenoga

👉Mb zinaisha fasta mpaka basi

👉Vocha ni janga la kitaifa

Hazipatikani ng'ooo yaani unaweza ukazitafuta kwenye maduka hata 30 na ukaja kuzikosa kabisa.
 
MD kapewa kada wa chama pendwa ubunifu utatoka wapi sasa?
 
Walimtoa MD ambaye amekulia TTCL, mwenye PHD ya Telecom Engineering toka Japan wakamweka kada wa chama aliyeshindwa hata kwenye kura za maoni unategemea nini?
 
@TTCL Customer Care njoo hapa, utoe ufafanuzi juu ya haya!
 
Shirika la hoyo kabisa

Na hivi jiwe kafa nalo litakufa kifo cha mende maana jiwe ndio alikuwa analibeba akawalazimisha watumishi watumie laini zao huku vocha kuzipata n mbinde

TTCL wanaishi karne ya kumi na tisa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mmeletewa nandy
Mnamtaka nani tena

Ova
 
Hatimaye TTCL wameanza kukosa ubunifu kabisaaa

👉Now wapowapo tu ubunifu ni 0.05%. Badala ya kuumiza kichwa kuboresha huduma, wameenda kumsainisha Nandy kwenye lebo yao ya Rudi Nyumbani Kumenoga ili wazurure kufanya shoo mikoani.

👉Unapiga menyu yao ya kuangalia salio. Ujumbe unakuja kuletewa masaa mawili mbele au usipate kabisa.

👉Mteja kwao wanatuona fala tu. Ukipiga simu ni mwendo wa Ok, yes, poa, rudinyumbani kumenoga

👉Mb zinaisha fasta mpaka basi

👉Vocha ni janga la kitaifa

Hazipatikani ng'ooo yaani unaweza ukazitafuta kwenye maduka hata 30 na ukaja kuzikosa kabisa.
Naomba ubadilishe title mkuu, iwe hivi, madhara ya TTCL kukosa ubunifu yazidi kuzorotesha shirika, mie sidanganyi, nimetupa line yao na wala sitaki kuisikia, period...
 
TTCL acheni usanii nitahama huu mtandao soon. jumamosi iliopita nilichuna vibaya vocha za ttcl. nilipiga simu customer service nikaambiwa nitume serial no kisha within 24hrs tatizo litakuwa solved. sasa inaenda wiki kila nikijaribu kupiga simu kuulizia naambiwa kuna changamoto, sijui nitatumiwa msg. tatizo kama hili lishawahi kunikuta huko nyuma na sikupata voucher yangu lakini nikapuizia. This time msiposolve hii issue nahama
 
Back
Top Bottom