Bwana Mpanzi
JF-Expert Member
- Jun 28, 2019
- 200
- 195
Kitalu ni sehemu ya maandalizi ya mimea au kiumbe kabla ya kuanza kujitegemea.
Inawezekana kuwa hili neno limetokana na kilatini cha "Seminarium" ikiwa ni mahala pa kukuza vijana kwa ajili ya kuwaandaa kuwapeleka masomo ya ngazi za juu yaani kusomea daraja au sakramenti takatifu Upadri.
Kwa ukweli sio kila mche au mmea unaanzia kitaluni, sio lazima inaweza kutegemea tabia ya mmea au muda wa ukuaji wa mmea mfano bamia. Kilimo cha bustani ni kundi kubwa sana la mimea na muhimu kulielewa na kulijua vizuri,nitaelezea mbeleni kidogoo hapa.
Tunaweza kugawanya makundi ya vitalu kama ifuatavyo:
1/ Vitalu vya Tuta au ardhini (Visivyohamishika)- Hapa msingi mkuu ni kuwa hivi vitalu ndio kundi kubwa hapa tunaelewa miaka na miaka tumekuwa navyo, unaandaa kituta wastani ni upana wa mita 1,urefu unaweza chagua na mwinuko wa tuta ni sm 15 mpaka 20 zinafaa sana.
Hapa utahitaji sehemu ambayo udongo hautuhamishi maji na mambo ya msingi pamoja na msingi wa ulinzi iwe kwa wadudu au binadamu.
Uzuri wake ni nafuu kuandaa na hahihitai elimu kubwa sana kuandaa.
Shida ni magonjwa,wadudu,upungufu wa lishe na uharibifu kutoka kwenye mifugo au binadamu.
2/ Vitalu vya Trey au Udongo maaumu (Vinavyohamishika)- Hapa unahitaji elimu kidogo ya kutunza na kuandaa.
Mahitaji
Unahitaji kuwa na trey na hizi zinatofautiana kutokana na matundu yake inaweza kuwa chini ya 100 mfano 75 au 100+ yaani 120 au 200 yaani 205 na kadhalika,matundu yanavyozidi kuwa mengi ndio ukubwa wa matundu unapungua (Large the size of the holes small the number and small the number of the holes Large the size)
Udongo
Hapa mara nyingi hutumika udongo maalumu yaani wenye kuupa mmea lishe salama. Mara nyingi huwa ni mchanganyiko wa vitu tofauti vyenye tabia ya kutunza maji kwa muda maalumu. Lugha ya kitaalamu ni Media.
Kutokana na masuala ya kiteknolojia vyanzo vya media vinaweza kuwa vya kawaida yaani kutengeza nyumbani au kiwandani,nyumbani unaweza tumia pumba za mpunga au Malanda ya mbao, rahisi sana hii ila lishe kidogo haitakuwa sawa utahitaji kuupa mmea mwenyewe kwa kila hatua ya mche.
Kiwandani wametoa media kutoka katika vyanzo mbalimbali mfano Nazi kwa hapa Tanzania ni Pangani na Kule Ng'apa lindi wamechakata ganda la nazi maarufu kumbi la nazi na kutoa Cocopeat, hii ni media maarufu nchin kwa wakulima.
Lakini pia kuna kitu kinaitwa Peatmoss, hapa sasa nitaomba ruhusa nimalizie nyakati zijazo na changamoto za kitaluni.
Nyakati njema wakulima na wote wana Maendeleo.
View attachment 1798762View attachment 1798763