KERO Changamoto za watembea kwa miguu kuvuka daraja la Kigamboni

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

april june

Member
Joined
Jul 6, 2016
Posts
8
Reaction score
1
Habari za usiku wakubwa.
Naomba Tanroads kwa kushirikiana na NSSF waangalie namna nzuri kwa wakazi wa darajani wakati wa kuvuka barabara kwenda upande wa pili baada ya kushuka kwenye daladala.

Kama umetembelea daraja la kigamboni au ni mkazi wa darajani utakuwa unalifahamu ili swala.

Hakuna alama sahihi za kuwafahamisha watumiaji wa magari kuwa ni eneo la kuvuka bali watu wenye magari wanatumia tu busara zao katika kuzingatia watembea kwa miguu wanaovuka baada ya kushuka kwenye usafiri wa daladala.

Nadhani ingeangaliwa namna nzuri ya kuweka alama maana kuna watoto wadogo wanavuka na watu wengine wenye matatizo mbalimbali, na ukizingatie ni umbali mrefu kutoka upande mmoja wa daraja mpaka upande mwingine.

Nawasilisha.
 
Ha ha ha jinsi watu wanavyopishana na magari pale mbele toll booths ni kama mazingaombwe. Sema madereva na wavukaji wanaelewana sana vinginevyo wangegongwa watu kila siku.
Hatari zaidi ni kule mbele baada ya kituo cha daladala kuna bar hivi,pale wavukaji huwa hawachukui tahadhari yoyote,ni hatari sana.
 
Uhalisia ni kuwa hakuna alama sahihi zinazozingatia watembea kwa miguu, kifupi ni kuwa… Vuka at your own risk.
 
Kati ya kituo darajani na nunge ukosahihi
Yes, ni sehemu yenye wavukaji wengi sana, ila hakuna alama ya kuwalinda wavukaji. Ni neema za Mungu tu na busara za wenye vyombo vya moto ila nje na hapo tungeshuhudia ajali nyingi sana.
 
Uhalisia ni kuwa hakuna alama sahihi zinazozingatia watembea kwa miguu, kifupi ni kuwa… Vuka at your own risk.
Kuna tuta pale lina alama, hio ndio sehemu maalum ya kuvukia. Sema watembea kwa miguu wanavuka daladala liliposimama. Hata madereva sio wote wanasimama kwenye hilo tuta kupisha watu.
 
Ukifatilia sehemu yenye tuta na kuwekewa alama za uvukaji (Pundamilia) sio sehemu ambayo watu wengi wanatumia kuvuka kwenda majumbani kwao au kupanda dalaladala.
Na kama ile ndio sehemu sahihi waliochagua kuvukia kwanini kituo cha daladala kipo sehemu nyingine tofauti na wao waliotaka watu wavukie?
Uhalisia ni kuwa, wanaona hali halisi inabidi kufanyiwa kazi kuepusha madhara makubwa ambayo hatuhitaji yatokee.
 
Hakuna kituo rasmi cha daladala pale. Daladala zinasomama sehemu yenye abiria popote pale.
Sehemu ya kuvukia ni hapo kwenye tuta na alama zipo,tatizo ni madereva na wavukaji hawazingatii sheria.
 
Back
Top Bottom