Elections 2010 Changia kesi dhidi ya Mahanga vs Mpendazoe

nitachangia yoyote anayetetea haki

Fred ntakuchangia, na hata wa CCM wanaoona haki yao imeppokwa

Acid
Wewe Acid mchangie tu Mpendazoe , lakini acha uzandiki wako! Haki gani ya wana CCM imepokwa kama mgombea wao ndiye aliyeshinda ubunge? Hivi kwa akili yako kwanini Mahanga wa CCM asishinde jimbo la Segerea kama Rais Kikwete wa CCM alimshinda Slaa kwa mbali kwenye jimbo hilo, na kwa upande wa madiwani CCM imepata kata 6 dhidi ya 2 tu za Chadema? Hivi hata kama Mpendazoe wa Chadema alimshinda Mahanga kwa jumla ya kura 4,500 kwenye kata za Segerea, Kimanga, Tabata na Kipawa kwa sababu zinazoeleweka, alipata akili wapi za kumdanganya kwamba angeweza kumshinda Mahanga kwenye ngome ya CCM na ngome ya Mahanga kwenye kata za Buguruni, Vingunguti, Kiwalani na Kinyerezi, ambapo huko kwenye kata hizo nne Mahanga alimshinda kwa jumla ya kura 9,000? Hivi nyie hamjui kwamba kata hizo za Buguruni, Vingunguti na Kiwalani wapinzani wa karibu wa CCM ni CUF siyo Chadema? Huo ushindi wa Chadema huko ungetoka wapi? Kama Mahanga anajua kuchakachua alishindwaje kuchakachua kwenye kata yake ya Segerea hadi diwani akawa wa Chadema? TAFAKARI!
 

You can fight Quality (a person) but you can't fight Facts!!!!!!! End
 
Any feedback zimeshafika ngapi.... (transparency is the key.....)
 
And those are facts that even God knows!

Mkuu be careful kumtaja Mungu kwenye masuala ya siasa, unless wewe ndiye Mahanga mwenyewe as such you are absoutely sure na unachokiongea.
 
Mkuu be careful kumtaja Mungu kwenye masuala ya siasa, unless wewe ndiye Mahanga mwenyewe as such you are absoutely sure na unachokiongea.
I have known him for the last 40 years. While I may not know some of his trivial personal issues, and I would not advocate for him in these, I know ALL his main political and social issues and ambitions, just as he knows mine (though myself I am not a politician as such). But I am particularly sure of these current political and social propaganda being perpetuated against him, and that were started by some sections of the local media (kwa sababu za makundi ya kisiasa ndani ya CCM). And these propaganda have negatively affected even his constituents. And all these just during the last two years or so! Inakuwaje huyu mtu ambaye miaka miwili, mitatu tu iliyopita alipokuwa naibu waziri wa miundombinu alikuwa anasifiwa na kila mtu kwa juhudi na harakati zake za kukagua barabara mbovu nchi nzima na kupambana na makandarasi wabovu - akionekana kwenye vyombo vya habari kila mara akiwa amekwama na gari lake kwenye barabara mbovu huko Singida, Kigoma, Musoma, Mbozi, Mbinga, Rukwa n.k. ghafla leo anaonekana "mavi"! Kweli vyombo vya habari vinaweza kumjenga mtu leo na kesho vikammaliza! Bahati inayomsaidia Mahanga yeye ni mpambanaji, in the real sense of the word - He is consistent and insistent in his chosen belief and political path, and as such he has lots of sympathizers and well wishers, as many or more than you people "his self-imposed enemies". For some of you I would only admit his one mistake (from your viewpoint): HE IS A CCM MEMBER AND NOT CHADEMA! That "mistake"' you can pursue. Otherwise Mahanga will surely prevail even in these current political machinations! Time will tell!
 
Any feedback zimeshafika ngapi.... (transparency is the key.....)

Mpendazoe atatoa initial feedback Dec 11, 2010 pale segerea. Karibu. kama hautakuwepo, nitakuwekea hapa jamvini jioni baada ya mkutano huo. Usikonde
 

There is no need of urguing. Mahanga hata wana CCM wenzake pale segerea, hasalimiani nao. Tena angejua, ndio waliosaidia kushindwa kwake.

Kuhusu ufisadi wa mahanga na open spaces, hakuna siri chini ya jua. Tutayaona kwa macho yetu. Hata Lowasa alikana kuhusika na Richmond!! Mahanga hata aoge maji toka mbinguni, hawezi kutakata!
 
Kutopendwa na mtu mmoja au wachache ni jambo la kawaida. Hata wewe una maadui! Kama kuna mwana CCM ana kinyongo na Mahanga kwa sababu binafsi, inawezekana. Lakini hii haina maana kwamba wote wako hivyo. Asingepata kura zote hizo. Mahanga bado anapendwa sana. Huyu ndiye Dereck Bryson wa Dar es Salaam - anakuwa sasa mbunge kwa miaka 15 Dar es Salaam. Kuhusu hivyo viwanja unavyodai amepora, hebu taja namba au maeneo vilipo hivyo viwanja ili watu wakuamini. Hawezi kupora viwanja vilivyoko hewani! La sivyo, na wewe utakuwa tu another FISADI WA UZUSHI!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…