Chanjo ni dhidi ya Waafrika? Namba Hazidanganyi!

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Takwimu zilizopo hadi sasa zinaonesha Bara Asia kwa idadi kuchanjwa zaidi wakati Afrika tukivuta mkia.

Kwa wastani wa watu kwa bara, Amerika Kaskazini wanaongoza, wakifuatiwa na Ulaya. Sisi kama ilivyo ada tukiendelea kuvuta mkia:

IMG_20210623_211238_107.jpg

Si kuwa Africa wanajivuta bali nchi zilizoendelea kwa ubinafsi wao, zimedhihirika kujivutia chanjo kwao zaidi.

Kwa mtaji huu ni wazi kuwa zile tantalira zetu za kubeza wafadhili wa chanjo na hata chanjo yenyewe, zilikuwa nyimbo nyingine kama michiriku tu.

Kwamba sasa hivi tuko hapa kuwa kote duniani, wagonjwa wengi wanafanana kwenye jambo moja - "kuwa walikuwa bado hawajapokea chanjo" inapaswa kutufikirisha:

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.

Kukubali mapungufu yetu ni kitendo tu cha maendeleo. Hayupo binadamu aliye mkamilifu. Ilikuwa kama pata potea tu. Tukawa tuli bet fyongo.

Ni wazi kuwa, hata kama ilikuwa kwa nia njema, kuinyanyapaa chanjo tulikuwa tumepotea maboya na kuuvaa mkenge vilivyo.

Ni muhimu Mama Samia sasa akajitokeza bila kuchelewa mno kuisafisha hali nzima ya hewa kuhusiana na chanjo hizi, kazi inapoendelea.

Kutereza si kuanguka, Mola na akampe ujasiri.
 
Kwa nilichoshuhudia na ninachoendelea kushuhudia katika viwanja vya mpira huko Ulaya ktika mashindano haya yanayoendelea... Covid ni kitu kinachofikirisha sana.....
 
Kwani tume ya mama ya wataalamu wabobezi wa afya inasema je, hadi hekima yetu kuishia kwenye viwanja vya mpira kuliko runinga tu?
 
Takwimu zilizopo hadi sasa zinaonesha Bara Asia kwa idadi kuchanjwa zaidi wakati Afrika tukivuta mkia.

Kwa wastani wa watu kwa bara, Amerika Kaskazini wanaongoza, wakifuatiwa na Ulaya. Sisi kama ilivyo ada tukiendelea kuvuta mkia:

View attachment 1827941

Si kuwa Africa wanajivuta bali nchi zilizoendelea kwa ubinafsi wao, zimedhihirika kujivutia chanjo kwao zaidi.

Kwa mtaji huu ni wazi kuwa zile tantalira zetu za kubeza wafadhili wa chanjo na hata chanjo yenyewe, zilikuwa nyimbo nyingine kama michiriku tu.

Kwamba sasa hivi tuko hapa kuwa kote duniani, wagonjwa wengi wanafanana kwenye jambo moja - "kuwa walikuwa bado hawajapokea chanjo" inapaswa kutufikirisha:

Huo ndiyo ulio ukweli mchungu.

Kukubali mapungufu yetu ni kitendo tu cha maendeleo. Hayupo binadamu aliye mkamilifu. Ilikuwa kama pata potea tu. Tukawa tuli bet fyongo.

Ni wazi kuwa, hata kama ilikuwa kwa nia njema, kuinyanyapaa chanjo tulikuwa tumepotea maboya na kuuvaa mkenge vilivyo.

Ni muhimu Mama Samia sasa akajitokeza bila kuchelewa mno kuisafisha hali nzima ya hewa kuhusiana na chanjo hizi, kazi inapoendelea.

Kutereza si kuanguka, Mola na akampe ujasiri.
Pia wanaongoza kufa kwa Covid ndio hao hao waliochanjwa kwanza na sio Waafrika wa bara la Afrika, wacha wachanjwe halafu wawe wanalazimishwa kuchanjwa kwa awamu na awamu zijazo itabidi mlipie mliochanjwa hakutakuwa nabure au kubembelezana tena sababu usiponunua chanjo ya awamu nyingine utashindwa kuhimili kuishi kwa vile kuishi kwako kutategemea chanjo, wenzenu wanawaingiza choo cha kike, huko mbeleni wao watatajirika zaidi kwa kuwakamua waliochanjwa.
 
Mkuu wewe ni mtalaamu wa afya au zile zile zetu za vijiweni?
 
Kwa nilichoshuhudia na ninachoendelea kushuhudia katika viwanja vya mpira huko Ulaya ktika mashindano haya yanayoendelea... Covid ni kitu kinachofikirisha sana.....
Baada ya kukamilisha chanjo wanaruhusiwa kukusanyika.
 
Back
Top Bottom