alwatanpeks
New Member
- Aug 16, 2021
- 3
- 0
Juhudi za ulimwengu kuudhibiti ugonjwa wa Covid-19 zimeendelea kuenea ulimwenguni kote baada ya mataifa kuanza kutoa chanjo zitakazowaweka wananchi wake salama dhidi ya maambukizi ya virusi wanaosababisha ugonjwa huo.
Tanzania ni miongoni kwa mataifa ambayo tayari yamepokea chanjo kupitia mpango wa Covax na wananchi kote nchini wanapokea chanjo hiyo kwa hiari na hadi sasa hakuna ripoti zozote za mtu aliyepata madhara baada ya kuchanja.
Hiyo inaonyesha kwamba chanjo ni salama na hazina madhara yoyote. Jitihada zinahitajika zaidi kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo ili watu waelewe zaidi kwanini ni muhimu kwao kuchanja.
Kwa bahati nzuri, serikali imeweka bayana kwamba chanjo ni hiari ya mtu. Anayetaka achanje na asiyetaka asichanje. Hilo limeachwa kuwa ni suala binafsi na mtu yoyote halazimishwi kuchanja wala kuzuiwa.
Hata hivyo, licha ya serikali kutoa mwongozo huo, kumekuwa na mazingira ya unyanyapaa kwa watu ambao hawajachanja hasa kwenye ofisi za taasisi mbalimbali kwa madai kwamba wataambukiza wengine.
Kwa bahati mbaya zaidi, waliochanja ndiyo wamekuwa na hofu zaidi kiasi cha kuwalazimisha ambao hawajachanja kwenda kufanya hivyo ili wasije kuwaambukiza wao licha ya kwamba wamechanja.
Ni kweli, kama tunavyoelezwa na wataalamu, hata waliochanja wanaweza kuambukizwa Covid-19 lakini haiwezi kuwa na madhara makubwa kama yanayotokea kwa ambao hawajachanja, lakini, hakuna sababu ya kuanza kuwanyanyapaa wasiochanja.
Kama nilivyosema awali, elimu bado inahitajika ili kuongeza msukumo wa watu kwenda kuchanja, pengine bado hajajua hatari iliyo mbele yao. Watu waliochanja ndiyo wenye nafasi nzuri zaidi ya kuelimisha kwa kutoa ushuhuda wa baadhi ya dhana zilizojengeka hasa kuhusu madhara ya chanjo.
Wakitimiza wajibu huo, watakuwa wamesaidia juhudi za serikali za kuelimisha jamii kuhusu kampeni ya kuchanja inayoendelea nchi nzima na mwisho wa siku lengo la kulinda afya za Watanzania litakuwa limetimia.
Nimesikia baadhi ya ofisi zinataka wafanyakazi wake wote wachanje, yaani suala la chanjo kwao ni lazima na siyo hiyari ya mfanyakazi. Baadhi yao wamechanja ili kulinda kazi zao lakini kwa hiari yao hawataki chanjo.
Sasa, utaratibu kama huo ni mbaya kwa sababu watu hao hawawezi kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kuhusu chanjo hiyo. Ni vizuri ofisi husika ikaweka utaratibu wa kutoa elimu kwa wafanyakazi wake kuhusu chanjo.
Katika hili, Spika wa Bunge, Job Ndugai alinukuliwa akisisitiza wabunge wote kuchanja huku akisema “hiari haina maana kuambukiza wengine”. Kauli hiyo inaonyesha wabunge hawana hiyari katika suala la chanjo.
Ni vizuri tukawekana sawa, “hiari” maana yake nini? Watu gani ambao wana hiari katika suala la chanjo? Mahali gani au wakati gani hiari ya mtu inaondolewa na kutakiwa kuchanja? Kwanini suala hili lilifanywa kuwa hiari?
Majibu ya maswali hayo yatatusaidia kuelewa maana ya hiari na kuondoa sintofahamu ambazo zinaendelea kwenye jamii zetu kuhusu chanjo. Ni muhimu wote tukawa na uelewa wa pamoja kuhusu mambo yanayotuhusu.
Kwa upande mwingine, wapo baadhi ya watu wenye ushawishi katika jamii ambao wamekuwa wakihamasisha wananchi kutochanja kwa madai kwamba chanjo zina madhara na kwamba kuendesha kampeni ya chanjo ni kuwatia hofu wananchi na athari zake ni kushuka kwa uchumi.
Sula hili nalo libaki katika msingi wa “hiari”, watu watumie fursa hiyo kutochanja na siyo kuhamasisha wengine kufanya hivyo. Mpaka serikali imeruhusu chanjo, maana yake imejiridhisha kwamba iko salama kwa afya za wananchi wake.
Kwa bahati mbaya, wanaopinga wanazungumza kwa nadharia tu bila kuwa na ushahidi wa kisayansi kuhusu madhara ya chanjo ambayo yanaweza kuhatarisha maisha ya mtu anayepokea chanjo.
Wataalamu wameeleza mara kadhaa kuhusu tafiti zilizofanyika kuhusu chanjo hasa ile ya Johnson Johnson ambayo ndiyo inatolewa nchini na siku za nyuma iliwahi kuripotiwa kusababisha changamoto kadhaa.
Ili kuondokana na mvutano wa hizi pande mbili, tuilinde sana hiari iliyopo ili kila mmoja asimamie anachokiamini bila kuathiri wengine. Hilo likifanyika, litarahisisha maisha ya Watanzania hasa katika kushughulikia suala la chanjo.
Elimu zaidi kuhusu chanjo itolewe na kila mtu mwenye nafasi hiyo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia hadi taifa. Wanasiasa walisichukulie jambo hili kisiasa kwa sababu linahitaji utaalamu wa kisayansi, wawaache wataalamu wafanye kazi yao.
NB: MAKALA HII IMECHAPISHWA GAZETI LA MWANANCHI - 17/08/2021.