#COVID19 Chanjo: Wanaopotosha Kuwajibishwa kwa Vifo wanavyoendelea Kusababisha

#COVID19 Chanjo: Wanaopotosha Kuwajibishwa kwa Vifo wanavyoendelea Kusababisha

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa mujibu wa Waziri Mollel:

1. Suala la ugonjwa wa Corona na tahadhari zake zikiwamo chanjo ni suala la kisayansi ambalo si kila mtu anaweza kuwa na ujuzi nalo.

2. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna watu bila ya kuwa na ujuzi nalo wamelivalia njuga na kuendelea kupotosha watu.

Kwa mujibu wa Waziri Mollel watawajibishwa wote wanaosababisha wengine wasio na hatia kuendelea kufa kwa upotoshaji wao kuhusiana na Ugonjwa huu.

Habari njema hii na inyumbulike kuwafikia wote wakiwamo waliowahi kuupotosha umma wakati wowote na kwa namna yoyote kuhusiana na ugonjwa huu na kupelekea vifo.
 
Waziri kavurugwa nini. Naomba niulize; vifo vimeanza mwaka huu punde baada ya chanjo kuja??

Waziri yuko vizuri.

Wote waliotupotosha na nyungu, maombi, michai chai, malimao, mikaratusi nk hata kama wako Chato, ni wa kulala nao mbele.

IMG_20210725_012351_122.jpg

Walituchelewesha sana!
 
Kwa mujibu wa Waziri Mollel:

1. Suala la ugonjwa wa Corona na tahadhari zake zikiwamo chanjo ni suala la kisayansi ambalo si kila mtu anaweza kuwa na ujuzi nalo.

2. Ni bahati mbaya sana kuwa kuna watu bila ya kuwa na ujuzi nalo wamelivalia njuga na kuendelea kupotosha watu.

View attachment 1895602

Kwa mujibu wa Waziri Mollel watawajibishwa wote wanaosababisha wengine wasio na hatia kuendelea kufa kwa upotoshaji wao kuhusiana na Ugonjwa huu.

Habari njema hii na inyumbulike kuwafikia wote wakiwamo waliowahi kuupotosha umma wakati wowote na kwa namna yoyote kuhusiana na ugonjwa huu na kupelekea vifo.
Kwanini waziri Gwajima haja wajibishwa, na alishiriki mauaji kipindi cha Mwenda zake?
Kwanini Jafo hayuko magereza. Kwanini Mollel yuko uraiani
 
Kwanini waziri Gwajima haja wajibishwa, na alishiriki mauaji kipindi cha Mwenda zake?
Kwanini Jafo hayuko magereza. Kwanini Mollel yuko uraiani
Hata dk Molleli mwenyewe alihusika kupotosha kipindi hicho
 
Kwa hiyo waliochanjwa hawafi sio!
 
Huyu Mollel ni "kichaa". Si yeye aendelee na kupima hizo chanjo na wanasayansi wake? Infact hicho ndicho Gwajima anachouliza.

Anachokifanya sasa ni kuthibitisha tu kwamba hawajawahi kuzifanyia utafiti hizo chanjo
 
  • Thanks
Reactions: mmh
Vitu vyengine vya kipumbavu yani nguvu zote zimeelekezwa kwenye hivyo vichanjo(chache) hali ya kuwa suala la level seat na kuvaa barakoa tu limewashinda, chanjo M1 tu (kwa watu M60) tunaangaika nazo na bado tunahitaji kuongeza nguvu ya kuwamasisha watu kwa hizo chanjo M1 tu halafu ajabu ndio tunaona hizo ndio tumaini letu na kusahau kabisa suala la kuchukua tahadhari za kujikinga na corona maana tumeshafeli huko na kuona hivyo vichanjo ndio vitasaidia.

Juzi kati nipo kwenye daladala mama mmoja katoka kudugwa chanjo yupo ndani ya daladala hana hata barakoa ndio kwanza anajipongeza kuwahi kuchanjwa.
 
Kwanini waziri Gwajima haja wajibishwa, na alishiriki mauaji kipindi cha Mwenda zake?
Kwanini Jafo hayuko magereza. Kwanini Mollel yuko uraiani

Kuwawajibisha Wanaopotosha na waliopotosha ni hatua njema sana.

Nani watakumbwa kwenye kokoro hilo, hilo ni jambo la baadaye.

Corona: Orodha ya wahanga, sampuli

Hatuko vibaya. Tulikubaliana kuwawajibisha wote waliosababisha ndugu zetu wengi kufa vifo ambavyo vingeweza kuepukika.
 
Hata dk Molleli mwenyewe alihusika kupotosha kipindi hicho

Uzalendo ni kukomaa na ukweli hata kama na wewe unakuhusu.

Mollel ni mzalendo kweri kweri. Isiishie kwa Gwajiboy peke yake. Hii ngoma hadi Chatto.
 
Vitu vyengine vya kipumbavu yani nguvu zote zimeelekezwa kwenye hivyo vichanjo(chache) hali ya kuwa suala la level seat na kuvaa barakoa tu limewashinda, chanjo M1 tu (kwa watu M60) tunaangaika nazo na bado tunahitaji kuongeza nguvu ya kuwamasisha watu kwa hizo chanjo M1 tu halafu ajabu ndio tunaona hizo ndio tumaini letu na kusahau kabisa suala la kuchukua tahadhari za kujikinga na corona maana..
Tuna watawala wa ajabu sana Nchi hii. Clueless. Mostly hawa bado wanaamini katika "kujifukizia" ila hizi ngojera wanaziimba kumfurahisha madam President ambaye yeye kwa sasa priority yake ni kutalii nje ya Nchi.
 
Wizara ya afya kwanza kabisa inatakiwa kuwa mstari wa mbele.
Wao wanapotosha wananchi.
Kwa kutokutoa taatifa muhimu ya vipimo, wagonjwa, vifo na waliopona.
Kila mkoa uwe na free Covid-19 Test ili watu wajitokeze.

Hata hili la kutoa chanjo hakuna mahali wanatoa kadi au maandishi ya kuonyesha umechanjwa! Sasa hu ni utaratibu wa wapi!??
 
Serikali haina dhamira ya dhati kupambana na ugonjwa huu ambao death toll yake hakuna asiyeiona:

1. Waliopotosha ugonjwa awamu ile ndiyo wale wale ambao leo eti ni vinara wa kupambana nao.
2. Mikusanyiko ya watu ikiwamo mbio za mwenge, makanisani, misikitini, kwenye mabasi, masokoni, magulioni nk iko pale pale na bila tahadhari zozote kuchukuliwa.
3. Hakuna takwimu zinazotolewa kuhusiana na ugonjwa huu kiasi haieleweki tuko wapi na tunakwenda wapi.
4. Haupo mkakati wowote ulio wazi wa kupambana na ugonjwa huu.
5. Kupimwa Corona inaendelea kuwa ni kwa pesa na si kidogo.
6. Waathirika wa ugonjwa huu wanajigharimia wenyewe matibabu.
7. Serikali haitambui kuathirika kwa watu na ugonjwa huu ndiyo maana ya kuwaongezea tozo na kodi zaidi ndani ya janga hili.
8. Serikali inatoa chanjo bila kuzingatia masharti wala vigezo vyovyote kinyume na maelekezo ya mtengeneza chanjo.

#COVID19 - Chanjo isiwe Siasa, Vigezo na Masharti vizingatiwe

Badala ya kuwahami watu chanjo na Corona kwa serikali amekuwa ni mwendelezo wa siasa.
 
Back
Top Bottom