#COVID19 Chanjo ya Corona ni hiari au lazima?

#COVID19 Chanjo ya Corona ni hiari au lazima?

Queen Esther

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
2,206
Reaction score
1,464
Wajumbe GT's hamjambo?

Mwenye ufahamu anieleweshe; chanjo ya ugonjwa wa Corona 19 ni lazima au la?

Nimeuliza hivyo kwasababu zifuatazo:-
1. Kila mtu anaongea lakwake watu wanashindana kwa kuwafokea Watanzania.

2. Kama chanjo ipo na ukichanjwa hupati, kwanini waliochanjwa wasifurahie maisha na kuwaacha wasiochanjwa? Hofu inatoka wapi wakati umeshajizindika chanjo?

3. Nani atakuwa na uhakika dawa inayochanjwa Ulaya ndiyo hiyo hiyo na Africa?

4. Kwanini chanjo ya Ukimwi mpaka leo haijapatikana? Corona hata mwaka bado imepatikana? Flu imekuwapo miaka yote na inaua huko mamtoni zaidi? Kwanini leo ugonjwa huu unafanywa siasa ya dunia? Nani yupo nyuma ya hili?

Trump alikuwa na mtazamo tofauti ikawa tabu!

Mwenye uelewa anisaidie tuache ushabiki vizazi vyetu vinatutegemea.

Queen Esther
 
Sio lazima, kila nchi itafanya uamuzi wake. Ila wanaweza kusema mtu asiyechanjwa asiingie kwao. Itakuwa uamuzi wako kusafiri au kubaki nchini kwako.

Aidha, hamna chanjo ni 100%. Kwa sababu hiyo ni bora wote wachanjwe ili pasitokee uambukozaji hata wa bahati mbaya. Vile vile hata kama utakataa kuchanjwa halafu ukaugua wengine watawajibika kukuuguza kwa gharama kubwa.

Upatikanaji wa haraka wa hii chanjo unatokana na rasilimali kubwa zilizowekezwa kwenye hizo chanjo. Aidha, ikumbukwe kuwa teknolojia zilizopo sasa hivi hazikuwepo hapo kabla.

Flu ina chanjo. Ukimwi kwa kiasi kikubwa umedhibitiwa ingawa bado chanjo inatafutwa. Ukweli ni kuwa mashirika ya madawa hayaoni umuhimu kuwekeza kwenye kutafuta chanjo dhidi ya magonjwa kama Ukimwi, Ebola, malaria n.k. ambayo hayaathiri kwa kiasi kikubwa nchi za magharibi kwa sababu hailipi kwao. Uwezo wetu wa kuzinunua ni mdogo mno kiasi cha wao kuweza kurudisha gharama walizoingia. Watu peke yao wenye uwezo wa kuwekeza kwenye huo utafiti bila kujali kama watapata faida au la ni watu kama Bill Gates ambao tunawatupia madongo.

Amandla...
 
2. Kama chanjo ipo na ukichanjwa hupati, kwanini waliochanjwa wasifurahie maisha na kuwaacha wasiochanjwa? Hofu inatoka wapi wakati umeshajizindika chanjo?


Queen Esther
Nimependa swali lako hili maana limekuwa swali langu nalojiuliza kila nikisikia Habari kuhusu hii chanjo ya korona. Mara usikie kwamba atakayechanjwa chanjo ya korona atapewa na cheti na mtu hatasafiri kuelekea nchi za ng'ambo Kama Hana cheti.

Swali, Kama huko watakuwa wamechanjwa, ukaenda na Korona yako, utawaambukiza waliochanjwa? Kama ndiyo, inamaana chanjo hiyo haitakuwa effective asilimia mia?
 
Ni hiari ila kunaweza kukawekwa restrictions nyingi mara baada ya watu wengi katika Nchi husika au duniani kupata kinga hiyo. Kwa mfano Nchi A kupiga marufuku wageni kutia mguu kwenye Nchi yao ambao hawana uthibitisho wa kupata hiyo chanjo hiyo.
 
Hahaha chanjo ya nini tena 5G au 6G Chid boy?!

Mara mseme hakuna covid,mara mseme inaletwa na 5G, sasa chonjo ya nini kwa kitu kisicho kuwepo?!
 
Ni hiari ila kunaweza kukawekwa restrictions nyingi mara baada ya watu wengi katika Nchi husika au duniani kupata kinga hiyo. Kwa mfano Nchi A kupiga marufuku wageni kutia mguu kwenye Nchi yao ambao hawana uthibitisho wa kupata hiyo chanjo hiyo.
Hii itakuwa ni kama vile zile chanjo za smallpox ambazo huwezi kwenda nchi za ulaya bila kuchanjwa.
 
Haya maisha lazima chanjo hautaki mkono wa chuma unakuhusu.
 
Hata katika baadhi ya Nchi pia wanadai kunaweza kukawekwa internal restrictions kama kuzuiliwa kwenda movies, clubs, kazini etc kama huna uthibitisho wa kupata chanjo. Hii itasaidia kufanya wengi waikubali chanjo hiyo ili kuepuka kutengwa kinamna.
Hii itakuwa ni kama vile zile chanjo za smallpox ambazo huwezi kwenda nchi za ulaya bila kuchanjwa...
 
Kama hatutapata hiyo chanjo basi utalii nchi utakufa.
 
Back
Top Bottom