Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Magonjwa ya kuhara husababishwa na vimelea vya aina mbalimbali.
Vimelea vya Rotavirus huchangia kwa kiwango kikubwa katika magonjwa ya kuhara kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Kwa Mujibu wa Takwimu za WHO, zaidi ya Watoto 525,000 Duniani wenye Umri chini ya Miaka 5 hupoteza Maisha kila Mwaka kutokana na Ugonjwa wa Kuharisha unaosababishwa na Rotavirus.
Nchini Tanzania takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa magonjwa ya kuhara yasababishwayo na rotavirus yalichangia asilimia 30 - 50 kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano waliolazwa kwa ugonjwa wa kuharisha.
Ugonjwa wa kuhara unaosababishwa na vimelea vya Rotavirus huenezwa kwa njia ya kula au/na kunywa maji yaliyochafuliwa na kinyesi chenye virusi hivyo.
Dalili zake-
Ugonjwa huu hukingwa kwa chanjo mbili za Rotavirus zinazotolewa wiki ya 6 na wiki ya 10.
Namna nyingine ya kuwakinga watoto dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu ni Kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita pamoja na Kuimarisha usafi wa mazingira na kunawa mikono kwa maji safi na sabuni.
Chanzo: Mpango wa Taifa wa Chanjo Tanzania

- Kuharisha
- homa
- Kutapika,
- Dalili za kupungukiwa maji na chumvichumvi mwilini
- Mtoto akiharisha sana hulegea ikifuatiwa na Degedege na kupoteza fahamu
- Upungufu mkubwa wa maji na chumvichumvi mwilini husababisha kifo.