๐จ๐๐๐๐ก๐๐ข ๐ฌ๐ ๐ฆ๐๐ฅ๐๐ง๐๐ก๐: ๐จ๐ฅ๐จ๐ฆ๐ ๐๐ ๐๐ง๐จ๐ฃ๐๐๐ ๐๐๐๐ก๐๐ ๐๐ ๐ ๐๐๐๐ข?๐ค๐ณ
Na,Fred Ma โ๏ธ
Baruapepe: fredmaofficial@gmail.com
Instagram: instagram .com/fredmaofficial
Ingawa maendeleo ya chanjo ya saratani ya mRNA kutoka Urusi yanaonekana kuwa hatua kubwa katika tiba ya saratani, kuna masuala muhimu ya kisayansi na kiufundi yanayohitaji kuzingatiwa kabla ya kutangaza mafanikio ya mwisho.
Hatua hizi zinahitaji kutathminiwa kwa uangalifu ili kuhakikisha usalama,ubora na ufanisi wake unakidhi viwango vya kimataifa.
Licha ya changamoto nyingi za kisayansi zinazogubikwa katika tangazo hilo kutoka Urusi,leo nitaangazia changamoto moja tu,nayo ni;
๐จ๐จ๐๐ฒ๐ฝ๐ผ ๐๐ฎ ๐จ๐๐ต๐ฎ๐ต๐ถ๐ฑ๐ถ ๐ ๐ฑ๐ผ๐ด๐ผ ๐๐ฎ ๐๐ถ๐๐ฎ๐๐ฎ๐ป๐๐ถ ๐ ๐ฝ๐ฎ๐ธ๐ฎ ๐ฆ๐ฎ๐๐ฎ:
Hadi hivi sasa, ripoti nyingi zimejikita kwenye majaribio ya awali ya kimfumo (preclinical trials) bila kutoa data za kina kuhusu usalama, ubora na ufanisi wa chanjo hiyo katika majaribio kwa binadamu kitaalamu โClinical Trials.โ
Data kutoka katika hatua hizo za โClinical Trialsโ ndizo hasa huonesha uwezo wa dawa ama chanjo hiyo dhidi ya ugonjwa uliolengwa.
Tumaini lolote la mafanikio linapaswa kutegemea uchambuzi wa data za majaribio yaliyodhibitiwa na kuwasilishwa vizuri na kupitia mchakato wa mapitio ya wenza wa kitaalamu (peer review).
Na ndiyo maana kwa kuzingatia hayo niliyoyaandika hapo juu, unaweza kuona licha ya tangazo hilo la Urusi juu ya kugundua kwa chanjo hiyo ya saratani, wataalamu wengi wa saratani duniani (Oncologists) wamegubikwa na โUshaukuโ na โUkushuku.โ
๐งUshauku wao unasukumwa na hamu yao ya kuona wagonjwa wa kansa wanaowahudumia, wanaondokana na mateso makali wanayoyapitia kwa kupatikana chanjo ama tiba ya kweli.
๐คAidha,ukushuku wao unatokana na ukweli kwamba, tangazo la upatikanaji wa chanjo dhidi ya saratani kutoka Urusi, linakosa sapoti ya data za kuaminika na za kina za kisayansi sanjari na utaratibu wa ugunduzi na uendelezaji wa chanjo (dawa).
1.Mtaalamu wa magonjwa ya saratani kutoka hospitali ya Artemis,India,Dkt.Gaurav Dixit anasema,
โMpaka sasa tunazo chanjo kadhaa dhidi ya kansa ambazo husababishwa na virusi (saratani za maambukizi ya virusi).
Sina hakika kama wao (Warusi) wanazungumzia kugundua chanjo dhidi ya kansa fulani mahususi au kansa zote kwa ujumla.
Binafsi ningependa kusubiri kwanza data za mwisho zikitoka kuliko kuwa na bashasha katika hatua hii ya sasa. โ
2.Naye mkuu wa kitengo cha saratani ya binadamu kutoka Taasisi ya Taifa ya Kansa Delhi,India, Dkt.Pragya Shukla anasema,
โMimi ningependa kwa sasa kuchukua msimamo wa โsubiri na tazamaโ.
Ni mapema mno kushangilia na kusema chochote.
Kugundua chanjo dhidi ya kansa zote duniani ni โchanga la machoโ kwa sababu kila kansa ina sababu tofauti na mtindo tofauti wa ukuaji wake (etiopathogenesis).โ
Dkt.Pragya anazidi kushuku kwa kusema,
โLakini hata kama ni kweli, haielezwi vizuri ni katika hatua gani ya majaribio chanjo hiyo ipo.
Kwa kawaida huchukua miaka walao 10 hadi 15 kuifanya chanjo yoyote ipatikane sokoni.โ
๐ฅKuhusu shauri la miaka mingapi chanjo huchukua kutoka kugunduliwa mpaka kuingia sokoni,kwa mtazamo wangu,sio lazima iwe miaka 10 na zaidi kama alivyotazama Dkt.Pragya Shukla.
Kwani,tumejifunza kutoka kwenye upatikanaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona (COVID-19) ambao haukufuata mtindo ulizoeleweka wa miaka 10 hadi 15 kwa sababu ya matumizi ya teknolojia ya mRNA ambayo Urusi inanadi pia kuitumia.
3.Aidha,mtaalamu wa saratani kutoka hospitali ya Medanta, India, Dkt.Satya Prakash Yadav anashuku kwa kusema,
โUtafiti juu ya chanjo ya kansa umekuwa ukiendelea kwa miaka 25 sasa.
Lakini,kiukweli,hakujapatikana chanjo โbabalaoโ mpaka sasa.โ
4.Ukushuku huo haukuishia nchini India tu,bali umetapakaa duniani kote.
Kwani huko Ireland,gwiji na jalimu wa Kingamaradhi (Immunology) kutoka Chuo kikuu cha Trinity College Dublin,Profesa Kingston Mills aliliambia jarida la Newsweek kwamba,
โBado tutaendelea kuwa wakushuku wa taarifa hiyo ya chanjo kutoka Urusi mpaka pale ambapo tutaziona data za majaribio kwa wanadamu (Clinical Trial Data).โ
Jalimu anazidi kudadavua na kusema,
โMpaka sasa sijaona taarifa yoyote kuhusu jambo hilo katika majarida ya kisayansi.
Kwani,kupitia majarida ya kisayansi ndiko ambako mwanayansi utaanza kuona na kusoma taarifa kama hizi za mafanikio na matumaini makubwa kwa umma.
Sasa mimi sioni chochote kuhusu jambo hilo.โ
Je,kwa maelezo haya ya jalimu Prof.Kingston, tuipuuze taarifa hiyo kutoka Urusi?
Jalimu anasisitiza,hapana! tusiipuuze kabisakabisa, akisema,
โLakini,hii haina maana kwamba wanasayansi wa Urusi hawajawahi kugundua chanjo kadhaa dhidi ya kansa,kwani shauri la chanjo dhidi ya kansa ni la kweli.โ
๐Hitimisho:
Ingawa matumaini yako juu, ukosefu au upungufu wa data thabiti unapaswa kutufanya kuwa waangalifu zaidi.
Ulimwengu wa kisayansi unahitaji ushahidi madhubuti wa kisayansi ili kuthibitisha kama chanjo hii ni hatua kubwa au hadithi nyingine ya matumaini ya muda mfupi tu.
โ๏ธTupe maoni yako,umeelewa nini?