Chanjo ya tetanus (Pepopunda) kwa wanawake

Chanjo ya tetanus (Pepopunda) kwa wanawake

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Tetanus (Pepopunda) ni ugonjwa unaosababishwa na sumu inayotokana na maambukizi ya bakteria wanaoitwa Clostridium tetani ambao hupatikana kwa wingi kwenye ardhi, vumbi na vinyesi vya wanyama.

B8502ABE-E22E-40C3-95B8-178411D9A505.jpeg

Vimelea hivi huingia mwilini kupitia sehemu za ngozi ya mwili iliyo wazi, kitendo chochote kinacho husisha ajali au matumizi ya vitu vyenye ncha kali, kutu na vile visivyo takaswa, au wakati wa kukata na kufunga kitovu cha mtoto pindi mwanamke anapokuwa anajifungua.

Tetanus (Pepopunda) husababisha kukakamaa kwa misuli ya taya na mwili mzima, pia huleta changamoto ya kupoozesha mfumo wa upumuaji, maumivu makali ya misuli, maambukizi makali ya mapafu, kuvunjika kwa mifupa kisha kifo.

Kwa kuwa mtoto anaweza kuambukizwa bakteria wanaosababisha ugonjwa kupitia kitovu wakati wa kujifungua, wanawake walio kwenye umri wa kupata ujauzito pamoja na wale wenye ujauzito tayari hushauriwa kupata dozi 5 za chanjo ya tetanus (TTV) ili kutengeneza kinga imara kwa faida yao wenyewe na watoto wanaozaliwa.

Chanjo hizi hutolewa kwenye kliniki za uzazi pamoja na wakati wowote ambao mhusika atapangiwa kuipata kwa mujibu wa ratiba, kanuni na taratibu za uchanjaji.

Huu ni mkakati wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wenye lengo la kupunguza idadi kubwa ya vifo vya watoto vinavyotokana na ugonjwa huu hadi kufikia walau wastani wa kifo kimoja kati ya kundi la watoto hai 1000 wanaozaliwa.


Chanzo: NATIONAL IMMUNIZATION SCHEDULE - United Republic of Tanzania, Recommended routine immunization
 
Back
Top Bottom