Chanjo zawadi ya mtoto, haki ya mtoto dhidi ya kuhara !!

ETT

Member
Joined
Jul 23, 2017
Posts
28
Reaction score
26
Nawasalimuni wote JFDoctors!!!

Somo la 1;Chanjo dhidi ya kuhara!!
Utangulizi
Chanjo, ni muhimu kwa mtoto kwani huandaa kinga ya mtoto mapema, na hivyo kumuepusha na maradhi ambayo yatamkabili siku za mbeleni ndani ya umri wa miaka 5,Chanjo imepunguza sehemu kubwa ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka 5(under five death) !!kwa 81% mwaka 2010

Chanjo ya kuhara!!
Chanjo ya kuhara inaitwa rotavirus vaccine(rotarix), na kuhara kusababishwa na virus aina ya rotavirus!!
Dalili ya kuhara!!
-kutapika
-homa
-kuharisha (maji)
Chanjo hii hutolewa kwa dosi mbili na huanza wiki ya 6 Tangy mtoto kuzaliwa!!
√Dose ya kwanza mtoto hupewa Kuanzia wiki ya 6 na mwisho wiki ya 15 haizidi hapo
√Dose ya pili huanza wiki 4 baada ya ile ya kwanza yaani wiki ya 10 na mwisho wiki 32!!

Chanjo hizi hutolewa katika vituo vya afya nchini
MZAZI; ni jukimu lako hutambua majira na nyakati ambazo unatakiwa kumpeleka mtoto kuhudhuria kituo cha afya kupata chanjo kwa wakati

Kwa kufanya hivi utakuwa umelinda uhai wa mtoto!!

Hii ni kwa wale ambao hudai kuwa hawana MBs za kuingia YouTube [emoji1]
Lakini bado unaweza ingia hapa kwa maelezo zaidi na ukapata masomo mengi zaidi...!!!

Asanteni karibuni kwa nyongeza !!
 
Duh.... mi nimechelewa afu now nina mtoto wa mwaka na miez miwili.... ananisumbua saaana..


Anaharisha now ni wiki ya pili.... sometime kinyesi cha njano....

Mara chache anatapika.... na joto kali saaaana.

Kaenda hospital kalazwa... wakampa ors... panadol na dawa ya kuzuia kuharisha... ila mpaka now hakuna dalili njema yoyote....

Wengine wanasema anaota magego ndio maaana yuko ivyo...
Wengine wanadai ana mdudu sijui minyoo sugu....
N.k

The badlucky ni kwamba dogo hapend kula hata kidogo na analia lia hovyo.

Msaaada kimtindo.
 
Aisee ni muhimu, tena ngoja nimuwahishe wangu ile ya miezi tisa
 
Reactions: ETT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…