#COVID19 Chanjo zimefika hapa msikitini leo

#COVID19 Chanjo zimefika hapa msikitini leo

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Leo mida hii ya swala ya adhuhuri afisa chanjo amefika msikitini tunapo swalia, nahisi atakuwa sio muislam maana kipindi tunaingia kuswali yeye alibaki nje.

Baada ya swala watu wachache wamejitokeza kuchanja hasa idadi kubwa ikiwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 50+ na vijana wachache.

Nadhani serikali inawajibika vilivyo kuwafikishia wenye nchi huduma ya chanjo mpaka kwenye nyumba za ibada, hii imekaa vizuri sana na vibaya kwa wale wasiohitaji huduma hii ya chanjo.

Jamani ndugu watanzania jitokezeni mkachanjwe ili kujikinga na uviko19...serikali inawajali na kuwapenda sana..haiwezi kutulisha matangopori mabosi wake..ila mimi sijabahatikiwa kuchanja kwa sababu naogopa sindano..labda ingeletwa chanjo ya vidonge.
 
Nitaweka video mtandao wa halotel ukitulia.
 
IMG_20210519_190156.jpg
 
Natamani CCM wangeendelea na msimamo wao wa kukataa chanjo....
 
Nijuavyo mimi hizo chanjo zinahitaji ubaridi sana, sasa nimewaona wanaojizumgusha nazo kwenye madeli, sijui kama zinabaki na ubora ule ule kwenye barafu
 
Kuna mahali ilikuwa siku kuu ya watoto, na watoto walipangiwa kushinda pale, kiongozi wa shughuli hiyo akatangaza anaomba wazazi waachie watoto washinde pale wakati shughuli inaendelea.

Muda kidogo shughuli ile inakaribia kwisha kiongozi mwingine akatangaza kuwa kwa siku hiyo watu wachanjo wanashinda pale hivyo, watu wajitokeze kuchanja.

Shughuli ilipokwisha, wazazi baadhi waliondoka na watoto wao, huku wakisikika wakisema usalama umepungua kwenye sehemu salama kimwili na kiroho. Funzo, mpagilio wa matukio ni muhimu sana kuzingatia mazingira ya wakati huo.
 
Leo mida hii ya swala ya adhuhuri afisa chanjo amefika msikitini tunapo swalia,nahisi atakuwa sio muislam maana kipindi tunaingia kuswali yeye alibaki nje...
Unafam expression ya spike protein gene on human cell?
 
Kuna mahali ilikuwa siku kuu ya watoto, na watoto walipangiwa kushinda pale, kiongozi wa shughuli hiyo akatangaza anaomba wazazi waachie watoto washinde pale wakati shughuli inaendelea...
Kwa hiyo hata huku kwenye nyumba za ibada inabidi watu wapewe taarifa mapema..sio kushtukiza mara paap mzigo huo hapo.
 
Leo mida hii ya swala ya adhuhuri afisa chanjo amefika msikitini tunapo swalia, nahisi atakuwa sio muislam maana kipindi tunaingia kuswali yeye alibaki nje.

Baada ya swala watu wachache wamejitokeza kuchanja hasa idadi kubwa ikiwa ni wazee wenye umri zaidi ya miaka 50+ na vijana wachache.

Nadhani serikali inawajibika vilivyo kuwafikishia wenye nchi huduma ya chanjo mpaka kwenye nyumba za ibada, hii imekaa vizuri sana na vibaya kwa wale wasiohitaji huduma hii ya chanjo.

Jamani ndugu watanzania jitokezeni mkachanjwe ili kujikinga na uviko19...serikali inawajali na kuwapenda sana..haiwezi kutulisha matangopori mabosi wake..ila mimi sijabahatikiwa kuchanja kwa sababu naogopa sindano..labda ingeletwa chanjo ya vidonge.
mkuu ulivyoanza kwa mhimizo huo, sikutegemea kama ungekula kona mwishoni kwa kisingizio cha kuogopa sindano. 😀😀 Asante kwa mwaliko lakini ......mh!
 
Back
Top Bottom