Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Leo jioni channel Ten na CCM wamezindua matangazo ya kumnadi JK huku wakichakachua aliyoyasema Dr. Slaa katika kampeni zake.
Jk anaonekana mikutano yake ya mijini mahudhurio watu wamejaa na huku mkutano ya Dr. Slaa kijijini hauna watu kabisa.
Jk akisindikizwa na muziki wa kizazi kipya anaonekana mambo ni shwari lakini huku kwa Dr. Slaa yuko kijijini ambako hata watu ni wachache..
Dr. Slaa anaonekana akitoa ahadi za kufuta kodi ili elimu na afya ziwe bure na mmoja wa mhudhuria mkutano huo ambaye yupo karibu na mtu mwenye gwanda la Chadema ambaye haonekani usoni ikithibisha ya kuwa ni picha za kuchakachuliwa tu alimwuliza swali hivi shughuli za uendeshaji wa serikali zitaendeleaje huku hakuna kodi ambayo inakusanywa.......Tangazo hili halimpi Dr. Slaa nafasi ya kujibu bali anasisitiza tu elimu na afya ndiyo vitakuwa bure ikionyesha ya kuwa hakuna uhusiano wowote ule na swali lililoulizwa....
Tangazo hilo linakwisha kwa kudai hayo yote yalikwisha kujaribiwa na yalishindikana......ikimaanisha ya kuwa huko nyuma serikali iliacha kukusanya kodi lakini iliendelea kutoa huduma za jamii bure na wakashindwa kuendesha serikali jambo ambalo siyo kweli.............................
Tatizo hapa ni kuwa mmiliki wa tangazo hili hajulikani. Kiutaratibu ni haki ya wateja wa Channel Ten kujua ni nani anayegharimia tangazo hili na kwa kiasi gani ana ubia na CCM ili kuwapa nafasi wapigakura waamue wamwamini vipi na wafahamu fedha za tangazo hilo zinatoka wapi........
Kwenye nchi zilizoendelea mmiliki wa tangazo kuonyesha uaminifu wake kwa wasikilizaji hujitokeza na kusema mimi ninaafiki tangazo hili.
Si Channel Ten au CCM ambao wapo tayari kujitokeza hadharani na kujimilikisha tangazo hilo kwa sababu limejaa madudu na linamshushia heshima yule aliyelibuni kwa sababu halisemi ukweli..........mahudhurio yote ya Dr. Slaa hakuna mahali ambapo yamekuwa kiduchu kama kwenye picha hizo.......Na hakuna mahali ambapo Dr. Slaa ameahidi kufuta kodi zote......hivyo tangazo hili linasema uongo........
Chama cho chote ambacho kitataka kuingia madarakani kwa njia ya kuchakachua hata ujumbe wa kampeni za wenziwe hakina uadilifu hata chembe na hakifai kuaminiwa na wapigakura kuliongoza taifa hili.
CCM na Channel Ten wanapaswa wajisafishe kwa kuueleza umma wa watanzania ni nani aliyecheza mchezo mchafu huu na fedha alizozitumia zinatoka wapi........vinginevyo NEC ina haki ya kulifuatilia suala hili pamoja na msajili wa vyama vya siasa...........ili kulinda utu wa mtanzania ambao una maadili yanayoeleweka ya kuheshimiana...........siyo kutungiana uongo
SOURCE: CHANNEL TEN LEO JIONI