SoC01 Chanzo cha Elimu kutuweka masikini

SoC01 Chanzo cha Elimu kutuweka masikini

Stories of Change - 2021 Competition

_pirate

New Member
Joined
Jul 16, 2021
Posts
4
Reaction score
11
Uchumi ni jumla ya shughuli zote za binadamu zinazolenga kutosheleza mahitaji yao. Namueleza mchumi kama mtaalamu ambaye kesho atajua kwanini vitu alivyotabiri jana havijatokea leo. Mjasiriamali hujifunza zaidi kwenye makosa kuliko kwenye mafanikio.

Uvumbuzi ndiyo msingi mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi.

Mafanikio ya mkakati wa maendeleo ya kiuchumi ni lazima yalenge kwenye kuongeza ujuzi katika nguvukazi ya eneo husika. Kuwa na nguvukazi kubwa bila ujuzi na utaalamu ni sawa na kazi bure.

Uhalisia ni kwamba biashara na uwekezaji ndio ishara kuu za uchumi na masoko ya hisa. Kama unataka kujua ni wapi masoko ya hisa yamewekwa, angalia matumizi ya biashara, mfumuko wa bei, kiwango cha riba na mapato ya uzalishaji.

Biashara ndogondogo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wetu. Kutoka kwenye biashara hizi ndipo ajira hupatikana.

Ni ukweli kwamba elimu ni msingi wa maisha, lakini siku za hivi karibuni elimu imekuwa ni kama haina maana. Wasomi wamekuwa ni wengi lakini ajira hakuna, tena sio ajabu unamkuta mtu na degree yake lakini anauza maziwa.

Hata viongozi wakubwa tu wa serikali wanasema hadharani kwamba vijana tusome lakini tukijua kua serikalini hakuna ajira, tutajiajiri wenyewe.

Jambo hili linauma sana, mtu unatumia karibu miaka 20 kumaliza mpaka elimu ya chuo kikuu lakini mwisho wa siku unaambiwa ujiajiri, sasa hapo kuna umuhimu gani wa kusoma, endapo ukijiajili unakuwa sawa tu na mtu aliyekuwa mtaani kwa miaka yote. Si bora miaka yote hio ungebaki mtaani unajipanga na maisha. Hata hivyo unaambiwa ujiajiri lakini huambiwi ni wapi utapata mtaji wa kujiajiri.

Zifuatazo ni njia 5 ambazo shule inatuweka katika umasikini bila kujijua:

1: Shule haitufundishi kuhusu maisha. Tunatumia miaka mingi shuleni bila kufundishwa jinsi ya kufikiria kupata fedha, afya ya kiakili, kodi, usimamiaji wa muda katika maisha, matumizi ya wema n.k

2: Shule inataka kutuweka kwenye madeni. Mwanafunzi wa miaka 20 anaweza kupata mkopo wa 100% kwaajili ya masomo ya chuo kikuu, lakini hawezi kuomba mkopo wa milioni 1 aanzishe biashara, kwani hana ujuzi wowote ule.

3: Shule inatuadhibu kwa kufeli. Kufeli ni nafasi ya kuanza tena, tena kwa umakini zaidi.

4: Shule inatufundisha kuweka fedha kwenye akaunti za akiba (saving account), badala ya kutufundisha namna ya kuwekeza.

5: Shule inatufundisha kuwasikiliza wakubwa. Badala yake inabidi kuwa mwangalifu ni sehemu gani unapata ushauri. Hauwezi kuchukua ushauri kutoka kwa watu ambao hawajawahi kufanya unachotaka kukifanya.

Naweza kusema kwamba, kama haumiliki hata kipande kidogo cha biashara, hauna njia kuelekea kwenye uhuru wa kiuchumi.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom