Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
CHANZO CHA LAANA YA WATU WA UKOO WENU KUFA MAPEMA KABLA YA UZEE. UKOO WENU KUKOSA WAZEE.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuna baadhi ya familia au koo ni Jambo la kawaida watu Kufa kabla ya Uzee. Yaani unakuta asilimia tisini ya watakaozaliwa kwenye familia au ukoo huo watakufa wakiwa chini ya miaka 60. Wengi wanakufa wakiwa na Miaka 30-50 hapo.
Koo au familia yoyote ambayo watu wake wanakufa kabla ya Uzee yaani kabla ya Miaka 60 au sabini hivi IPO kwenye koo zenye Laana ya kutoishi Miaka mingi.
Fikiria unaanzisha familia Leo unamiaka 30 alafu kumbe umebakiza Miaka 15 ufe ukiwa na Miaka 45 yaani bado mdogo Kabisa. Ni wazi utakuwa umeacha familia katika wakati Mgumu iwe kiuchumi, kimalezi ambapo bado watakuwa wanakuhitaji.
Zifuatazo ni Sababu za ukoo wako watu wake Kufa mapema na kusiwepo na Wazee;
1. Ushirikina na Uchawi.
Familia na koo nyingi za kishirikina na kichawi hazinaga Wazee wengi.
Ushirikina unafupisha maisha yako na kukuletea Laana ya Kifo cha mapema ndani ya kizazi chako.
Waganga wakienyeji kamwe hawakuambia Jambo hili lakini kadiri unavyokuwa mshirikina ndivyo unavyopunguza siku za kuishi kwako mwenyewe na kizazi chako. Unaweza usinielewe lakini Kwa waganga na Wachawi na Sisi makuhani tunalielewa Jambo hilo kwani lipo wazi kabisa.
Kwenye Koo za kichawi ni Jambo la kawaida kukuta kibibi au kibabu kimoja pekee ndio kipo na kimegoma Kufa lakini wenzake wote wamekufa mapema Kabisa kabla ya kufikisha Miaka 60. Kinaua ndugu zake na watoto wa ndugu zake, watoto wake na wajukuu zake.
Kumbuka unapoenda kwa mganga hakuna Jambo lolote wanalotaka viumbe wa rohoni, Majini na pepo wachafu zaidi ya damu(uhai wako au wa uhai wa Mtu) hiyo kukuagiza masharti mengine kama sijui Kuku, sijui mbuzi, au Njiwa au masharti mengine ni geresha tuu. Ukweli ni kuwa wanamega sehemu ya uhai wako. Ubaya unakuja ni pale hawakuambii UKWELI wote.
2. Baba na Mama Kushindwa Kuwapa watoto maadili Mema
Watu wengi hawajui kuwa kitendo cha Wazazi kushindwa kutoa malezi yenye maadili kwa watoto ni moja ya chanzo cha Laana ya Kufa Mapema na ukoo wenu Kukosa Wazee.
Ukitaka ufa mapema Dekeza watoto wako. Kwanza wao wenyewe utashuhudia wakifa mbele ya macho yako wakiwa bado wadogo na zaidi wewe mwenyewe utakufa kabla ya Miaka 60.
Kwa Sisi ambao tumetoka familia zenye wazee wengi Sana. Miaka sitini ni wajomba zangu ambao bado ni vijana Kabisa wenye nguvu Kabisa. Yaani ni Miaka michache Sana.
Kidogo nguvu zinaanza kupungua mtu Akiwa na Miaka 80 hapo ndio nilikuwa nauona Uzee kwa Bibi na Babu zangu.
Torati inasema, waheshimu Baba yako na Mama yako ili siku zako zipate kuwa Nyingi. Tunazungumzia siku nyingi yaani Uzee.
Na heshima inayozungumziwa hapa ni heshima ya HAKI na KWELI. Sio mzazi ni mpumbavu anaabudu mizimu na mashetani alafu wewe ati umheshimu. Nope!
Hivyo ni jukumu la mzazi kumlea mtoto wake kwa maadili Mema ya HAKI na KWELI ili mzazi awe Mzee na ili mtoto awe Mzee.
Hakuna umuhimu wa Baba au Mama yako kuendelea kuishi ikiwa hakukanyi unapokengeuka. Yaani huyo mzazi hana umuhimu wowote wa kuendelea kuishi ikiwa Hana maadili Mema.
Kwa bahati nzuri nature inajua nini chakufanya.
Mzazi unaona mtoto anafanya wizi, anadhulumu watu, anatiatia Mimba watoto wa watu huko. Upo Kimya huchukui Hatua zozote.
Watu wanakulalamikia kuhusu Tabia mbaya ya mtoto wako. Unamtetea au pengine humtetei lakini huchukui Hatua.
Nakuambia unakaribisha Laana ya Kifo cha mapema sio kwako tuu Bali kwa ukoo wako wote.
Soma Kisa Hiki;
1 Samweli 2:32-33
32. Nawe utayatazama mateso ya maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hapatakuwako mzee milele.
33. Tena mtu wako, ambaye sitamtenga na madhabahu yangu, atakuwa mtu wa kukupofusha macho, na kukuhuzunisha moyo; tena wazao wote wa nyumba yako watakufa watakapokuwa watu wazima.
Unaweza kuanzia 1 Samweli 2 yote upate Kisa chote.
Muhtasari wa Kisa hicho ni kuwa Kuhani Eli alikuwa akiwadekeza watoto wake. Alishindwa kuwalea vizuri wawe na maadili Kiasi kwamba watoto wake wawili ambao ni Finehasi na Hofni walikuwa wakisumbua majirani na waumini waliokuwa wanakuja kutoa dhabihu au kusali au kwa huduma zozote kutoka kwa Eli Babayao ambaye ni kuhani. Wakawa wanazini na waumini. Wakawa wanakula Sadaka lakini Eli licha ya kulalamikiwa na jamii kwa Muda mrefu akawa Kimya.
Ndipo hiyo Laana ikatoka.
Baba ni lazima ukemee Tabia mbaya za watoto. Na kama litoto halisikii lifukuze hapo nyumbani na hata likiwa mbali liambie Kabisa wewe sio mtoto wangu kuonyesha umechukizwa na Tabia za kipuuzi za huyo mtoto.
Kunyamaza tafsiri yake ni kukubaliana na matendo ya huyo mtoto.
Mtoto kuwa na Pesa au umaarufu haina maana wewe kama Baba ushindwe kutimiza majukumu na wajibu wako kama Mzazi.
Kemea,karipia na weka vikwazo ili kumrudisha mtoto kwenye Mstari
Huo ndio Ubaba.
Baba unapokuwa dhaifu unatengeneza mazingira ya kizazi unachoenda kukianzisha au ulichokianzisha Kupata Laana zisizo na Sababu.
Baba lazima ukisema Tarehe Fulani mwezi Fulani watoto wangu nataka niwaone hapa. Watoto wafanye hivyo asiwepo wa kuleta nyenyenye! Asiwepo wa kutoa kisingizio hata kimoja.
Lakini Moja ya dalili kuwa wewe sio Baba au mwanaume ni kushindwa kuitiisha familia uliyoitoa kwenye korodani na kiuno chako. Na hiyo ni dalili wewe mwenyewe hukujitiisha, hukuniheshimu.
Ulishindwa kufanya majukumu yako tangu watoto wakiwa wadogo Leo hata useme njoo hakuna hata Panya atakayekusikiliza akaja.
Baba unatelekezwa na watoto kama Mtu mwenye LAANA bhana!
Zingatia; Ubaba sio kutia Mimba na kuzaa kama Panya Buku au Nguchiro anavyofanya. Ubaba ni KUBEBA Majukumu ya Mungu katika Maisha yako kwenye jamii inayokuzunguka.
1. Tafuta mwanamke wa kufanana nawe.
2. Mtiishe. Hakikisha anatiii na kukusikiliza.
Usizae na mwanamke kama hakutii.
3. Zaa watoto.
4. Shirikianeni na Mkeo kulea watoto na kuwatiisha.
Yaani lazima watoto wafuate maelekezo yenu. Mtoto ambaye atakengeuka muwekeenk vikwazo vya kutosha kulingana na kukengeuka kwake.
5. Saidieni jamii
6. Saidieni watoto wenu kwa pamoja wapate wenza Sahihi.
7. Wapeni wajukuu Historia zenye Tija kwao na kuwafanya wawe Mashujaa na wenye maadili
8. Kikaribisheni Kifo mkiwa mmejiandaa vyema na mkiwa hamna mlilobakiza Duniani.
9. Pumzikeni Kwa Amani Kama ma-legendary
Acha nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon master
Kwa sasa Dar es salaam