mohammed Arafatt
Member
- Jul 28, 2022
- 7
- 4
Si kila tajiri amesoma na si kila maskini ndivyo alivyopangiwa na Mungu bali utajiri hupatikana kwa jitihada za mtu katika maisha yake haijalishi hujaingia darasani ila una nini kichwan kwako? Hivyo basi hata umaskini hutawala maisha yetu kwakuwa wazemne na watu wenye fikra fupi katika kutafuta riziki.
Si kila aliyesima aliambiwa atumie ujuzi aliopatiwa darsani pekee ili kufanikiwa.Mawazo haya ndiyo chanzo kikuu cha umaskini kwa wale wote waliopata Elimu kutegemea ujuzi wa darasani pekee yaweza kuwa ni Ualimu,Uasibu,Uandishi wa habari, Udaktari na udereva huku wakiwa wamesahau uti wetu wa mgongo kwa Taifa na si kitu kingine bali kilimo
Katika shule moja ya sekondari iliyopo mkoani mara iliyojulikana kwa jina la TUPENDANE. Ikiwa ni siku ya jumatatu mida ya saa 6 mchaa wanafunzi wote walikuwa katika vipindi siku hiyo kidato cha nne "B" kulikuwa na kipindi cha Kiswahili ambachobkilihoji kwamba 'Baada ya kumaliza elimu yako unataka kuwa nani?'
kipindi kilikuwa kama hivi
Leo kila mmoja atsema anahitaji kuwa nanu katika maisha yake,nikianza na Amina"Alisema mwalimu Zamaradi" Amina alisimama kwa kujiamini nakusema, Mimi nikimaliza elimu yangu napenda kuwa rubani wanafunzi wenzake waliguna na wengine kucheka kwa kebehi na kusema fizikia yenyewe tu juzi kapata 20, Nyamazeni, kila mtu atasema kazi aipendayo "alisema mwalimu" kipindi kikaendelea kila mwanafunzi alitaja kazi zenye hadhi ya juu zinazoendana na mionekano yao, Lakini kabla mwalimu hajamaliza kipindi aliwaasa kwamba ili kupata yote hayo wayatakayo itawwbidi wasome kwa bidii na kumtanguliza Mungu ghafla mlango wa darasa ukawa unagongwa.
"Ingia" Alisema mwalimu
''Shikamoo mwalimu" Aliamkia Atupele
"Marhaba Atupele huu ni muda gani na unatokea wapi?" Aliuliza mwalimu
"Nilikua najisikia vibaya mwalimu, nikaombq ruhusa nikanywe dawa nyumbani"Alisema Atupele
"Sawa nenda ukakae" Alisema mwalimu
Wanafunzi wakaanza minong'ono tena,Huku wakisema Mwalimu Atupele naye atuambie anahitaji kuwa nani katika maisha yake?
Mwalimu alivyosikia hivyo alimsimamisha Atupele na kumwambia aje mbele kujieleza, Bila kisita Atupele alisimama kwa kujiamini na kwenda mbele ya darasa kila mmoja alikuwa nashauku ya kujua Atupele anataka kiwa nani, Kutokana kwamba Atupele alitokea katika familia tajiri sana na inajulikana kila mahali.
Mimi Atupele juakuu katika maisha yangu natamani kuja kuwa mkulima mkubwa ambaye nitajulikana ndani na nje ya nchi.Naamini nitakuwa tajiri mkubwa duniani kama Bilget na Utajiri wangu utapita familia yangu,Alivyomaliza kuongea alirudi kukaa kila mmoja alistaajabu kusikia hivyo,Mwalimu hakusema lolote alibeba vitabu vyake na kurudi ofisini.
Siku zilienda Atupele alimaliza chuo na kujikita katika maswala ya kilimo bila kujali familia yake kumtenga maana kuna imani kwamba katika familia tajiri akitokea mmoja anayejihusisha na ukulima huyo anatabiri Umaskini (sikweli) Siku zilivyozidi kwenda kuna Ugonjwa ulijitokeza ambao ulipewa jina la Mbarazi.
Ugonjwa huu ulitesa wengi bila kujua chanzo chake, Watu walikufa kila kukicha ,viongozi wa nchi hawakujua tatizo na chanzo cha ugonjwa huo, Waliugua walitoka vidonda mwili mzima baada ya wiki vile vidonda vilitengeneza usaa na kuoza, Madaktari walitaabika, Raisi alishika tama hakujua chakufanya maana kama fedha zimetumika nyingi katika kitibia watu lakini ilishindikana.
Lakini mtu aliyekuwa na utatuzi wa tatizo hilo alipatikana, Raisi alisikia fununu hizo kwamba kuna binti aitwaye Atupele anaweza kuwa msaada katika taifa, Raisi hakuchelewa alimtafuta Atupele popote alipokuwa, Lakini kwa kipindi hiko Atupele alishaondoka mjini akawa ni mtu anayeishi vijijini, Alitafutwa na akapatikana na kupokea wito wa raisi na kwenda ikulu, Pindi wakiwa Ikulu viongozi wote walikuwepo kumsikiliza Atupele kwa kile atakachokisema kama msaada kwa nchi, Kama kawaida yake alisimama kwa kujiamini na kusema Mungu ametuumba sisi Binadamu na mimea tofauti tofauti iliyopo duniani.
Hakuwa mjinga bali alijua faida ya mimea, Nchi hii Mungu ametubariki utajiri ametubariki kuwezesha teknolojia ya viwanda lakini viwanda hivyo tunasindika nyama na samaki tu, tukiamini kwamba mboga za majani ni 'Umaskini mtupu' , Tazama kila siku mnahamasisha watu kula mlo kamili je mshawahi fikiri mlo kamili unaenda pamoja na mboga za majani kama mchicha,figili na chaenizi?
Au nyama na samaki pekee ndio mlo kamili? Tatizo au Ugonjwa huu unasababishwa na ukosefu wa Vitamini "A" ambao unapatikana kwa kula mboga mboga. Hivyo basi kila mmoja anatakiwa kuanzia leo atumie mboga hizo kama dawa na kinga ya ugonjwa huo na Elimu hii itolewe kwa watu wote ila zaidi ni kwa matajiri kwani takwimu zinaonyesha kwamba watu wengi walioathirika na ugonjwa huu ni matajiri ambao wanamtazamo kuwa mboga za majani ni mboga za watu maskini.
Watu wote pale walishangaa kuwa matumizi ya mboga mboga ndiyo utatuzi wa tatizo lao Raisi alimshukuru sana Atupele na kutaka kumpa pesa kwaajili ya matumizi yake ila Atupele alikataa katakata akasema "Utajiri na fedha nitaupata shambani". Akaondoka akiwa peke yake huku akiamini kwamba Taifa lake litaanza kuwajali na kuwathamini wakulima wote ambao kwa kipindi cha nyuma walinyimwa haki na hata kuonekana ni watu warudishao nyuma maendeleo ya Taifa.
Ila baada ya hapo serikali ilianza kutoa ruzuku katika maswala ya kilimo upande wa pembejeo, Viwanda viliongezeka kwakuwa serikali ilihamasisha vijana kuingia katika kilimo. Pia pato la taifa likapanda kwa kasi mno kutokana kwamba mipaka ya nchi ilifunguliwa ambapo wananchi walikuwa na uhuru wa kuuza mazao yao nje ya nchi kwa bei wazitakazo.
Kila mmoja alimuheshimu Atupele kwa maono yake ya mbali, kama isingekua yeye Taifa lingeangamia watu wangepoteza maisha, Uchumi ungezidi kupolomoka siku hadi siku. Serikali haikumuacha hivihivi ilimzawadia hekali 30 za mashamba na kumuandikia kitabu cha kumpongeza kilichopewa jina la "SHUJAA WA TAIFA LETU".
Haikuishia hapo Atupele aliingia katika orodha ya matajiri duniani ambapo alikuwa tajiri wa pili dunia nzima,Aliosoma nao walishangaa kumuona Atupele akifanikiwa siku hadi siku wao wakibaki katika maisha ya kawaida na kazi za Udaktari, Uwalimu na wengine Wahasibu.
Somo la kilimo lilianza kufundishwa kila shule kianzia msingi hadi Elimu ya juu,Atupele alijivunia sana kwa kuwa alibadili fikra za wengi na kuwahishemisha wakulima wote duniani, Alipofika miaka 75 alifariki dunia ambapo aliacha watoto 4 na mume wake kipenzi Nelson, Huku akiwa ameacha kitabu cha maisha yake kilichoitwa "CHANZO CHA UTAJIRI WANGU"

Upvote
1