Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Chanzo muhimu cha maji kwa wakazi wa Manispaa ya Arusha kimefungwa. Chanzo hicho chenye uwezo wa kutoa lita za maji 110,000 ( Mita za ujazo 110) kwa saa kimefungwa baada ya maji yanayotoka hapo kuwa na madini mengi ambaye yanaathiri mifupa.
Source: ITV
Hata hivyo, maji hayo yamekuwa yakitumika kwa muda mrefu na wakazi wa Mji wa Arusha. Wakazi wengi wa Arusha huwa na meno yenye rangi ya brown ambayo ni moja ya athari za madini hayo. Athari nyingine za amdini yaliyo kwenye maji hayo ni kupinda kwa mifupa tatizo ambao baadhi ya wakazi wa Arusha huwa nalo na kusababisha wengine kufanyiwa upasuaji kuvunjwa miguu.
Miji wa Arusha, hasa sa maeneo ya Njiro kwa kawaida huwa na upungufu mkubwa wa maji na hufikia hata miezi mitatu bila kupata maji ya bomba; kufungwa kwa chanzo hicho kunaweza kusababisha wakazi wa baadhi ya maeneo hasa Njiro kutopata maji ya bomba kabisa.
Ajabu ni kuwa haikuelezwa hatyua mbadala za kukabiliana na upungufu utaojitokeza kwa kufungwa kwa chanzo hicho.