Rasi ya Korea ilikuwa
koloni la
Japan kuanzia
1910 hadi
mwaka 1945. 1945 kwenye mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia
jeshi la Urusi liliwafuata Wajapani
kaskazini mwa
rasi na
Wamarekani waliingia
kusini. Korea ikagawiwa.
Mwanzoni kulikuwa na majadiliano ya kuunganisha Korea tena lakini
Vita Baridi ilileta uadui kati ya pande hizo mbili. Kila moja ilianzisha
serikali ya pekee katika kanda la
utawala wake kufuatana na
itikadi yake. Warusi walitaifisha tasnia na
ardhi wakaacha serikali ya
kikomunisti katika kaskazini na Wamarekani waliacha
uchumi wa
kibepari na serikali iliyochaguliwa katika kusini. Kila upande ulikandamiza vikali wafuasi wa itikadi ya kinyume.
Hapo mwanzo wa Korea Kaskazini (mwanzoni chini ya Warusi) na Korea Kusini (mwanzoni chini ya Marekani) waliokuwa maadui tangu mwanzo.
Mwaka 1950 dikteta wa kaskazini aliamua kuunganisha Korea kwa njia ya vita. Mwezi wa Mei
1950 jeshi la kaskazini lilivamia Korea ya Kusini likateka mji mkuu wa Seoul na kusukuma watetezi hadi kusini ya
rasi ya Korea.
30 Julai 1950 Baraza la Usalama la UM iliamua kuingilia kijeshi dhidi ya uvamizi kutoka Korea Kaskazini. Azimio hii lilipita kwa sababu Umoja wa Kisovyeti (=Warusi) hukuhudhuria kikao hivyo ulishindwa kupiga
veto yake. Jeshi lililoingia kwa niaba ya Umoja wa Mataifa liliunganisha vikosi kutoka nchi 22, jumla askari 500,000 na wengi wao kutoka Marekani.
Vita iliendelea hadi 1953. Korea ya Kaskazini iliweza kudumu kwa sababu ya msaada wa kijeshi wa China iliyoleta
askari milioni moja Korea. Katika vita hii watu wengi waliuawa na hasa kaskazini iliharibika sana . Si rahisi kutaja idada ya wahanga wote, lakini makadirio yanataja karibu milioni 4 watu raia na wanajeshi hadi milioni 1 pande zote mbili.
Soma hapa:
Vita ya Korea - Wikipedia, kamusi elezo huru