Dom boy
Member
- Jan 24, 2018
- 99
- 64
Katika hali ya mazoea ya muda mrefu, imeshakuwa ni jadi kwa vitafunio hivi wakati wa chai kufungwa ndani ya magazeti unapokwenda kununua kwa baadhi ya watayarishaji, mfano mama lishe.
Nionavyo mimi iko haja ya hao waliodumu katika utamaduni huu wabadike, gazeti toka kiwandani mpaka limfikie muuzaji huwa limeshapita sehemu nyingi, na kwa hali hii sina uhakika na usafi wa gazeti hilo, itapendeza sana kama itabuniwa njia mbadala ya vifungashio hivi.
Je Maafisa Afya wana mtazamo gani juu ya kulinda afya ya mlaji.
Nawasilisha.